PreGE2025 Kesi iliyofunguliwa na Saidi Issa na wenzake wawili (2) dhidi ya CHADEMA yaahirishwa. Jaji ashindwa kufika mahakamani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
889
Reaction score
2,863
Wakuu,

Siku ya leo ndo ile siku ambayo Mahakama itaanza kusikiliza kesi ya CHADEMA baada ya kushtakiwa na wanachama wao wa Zanzibar kwamba wanatumia mali za chama vibaya

==============
Alichoandika Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche

Kesi ya kina Said Issa ni Kesi ya kisiasa kujaribu kuzuia chama chetu kufanya shughuli zake halali..
Jaji aliepanga Kesi leo anakosaje kuwepo mahakani siku ya Kesi tena Kesi muhimu kama hii kwa Nchi?

Jaji aliefanya maamuzi ya haraka na kutoa maamuzi tena bila hata upande wetu kuwa na uwakilishi wa wanasheria!!

Mahakama ya Tanzania isikubali kutumiwa na wanasiasa ambao wameshindwa kufanya kazi za siasa za kushawishi umma.

==========================
Shauri ambalo limetoa zuio kwa Chadema kufanya siasa limeahirishwa ikidaiwa Jaji ana majukumu mengine

Kesi namba 8323/2025 ambayo imetoa zuio la muda kwa Chama cha Chadema kufanya shughuli zozote zile kiutendaji na oparesheni mpaka pale kesi ya msingi iliyofunguliwa itakapoanza kusikilizwa, imeahirishwa mpaka Julai 10, 2025 kutokana na Mh. Jaji Hamidu Mwanga anayesikiliza kutokuwepo.

Katika kesi hiyo ambayo imetajwa leo June 24, 2025 kwa ajili ya kusikilizwa, ilifunguliwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar, Saidi Issa Mohamed na wenzake wawili (2) dhidi ya Baraza la Wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA.

Akizungumzia shauri hilo baada ya shauri kuahirishwa Wakili Utetezi, Hekima Mwasipu amesema kuwa Jaji hajatokea Mahakamani ikidaiwa kuwa yupo na majukumu mengine.

Ikumbukwe Shauri hilo lilikuja kufuatia maombi yaliyowasilishwa Mahakamani hapo na Mawakili wa waleta maombi wakiongozwa na Wakili Gido Thomas Simfukwe ambao waliiomba Mahakama kuweka zuio hilo hadi kesi ya msingi itakapoanza kusikilizwa.

Kwenye kesi ya msingi waleta maombi wamewasilisha madai kuwa CHADEMA imekuwa ikiitenga Zanzibar katika masuala mbalimbali ikiwemo mgawanyo wa raslimali fedha n.k .

Your browser is not able to display this video.

Pia soma Pre GE2025 - Mnyika ashangazwa na kitendo cha Jaji kutokufika mahakamani
 
Your browser is not able to display this video.
Alichoandika Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche
Kesi ya kina Said Issa ni Kesi ya kisiasa kujaribu kuzuia chama chetu kufanya shughuli zake halali..
Jaji aliepanga Kesi leo anakosaje kuwepo mahakani siku ya Kesi tena Kesi muhimu kama hii kwa Nchi?

Jaji aliefanya maamuzi ya haraka na kutoa maamuzi tena bila hata upande wetu kuwa na uwakilishi wa wanasheria!!

Mahakama ya Tanzania isikubali kutumiwa na wanasiasa ambao wameshindwa kufanya kazi za siasa za kushawishi umma.

#NoReformsNoElection itaendelea kwasababu ndio takwa la Wananchi.

Shida ya CHADEMA ni kutofanyia ushauri kwa wakati mnaopewa humu. Huyo hakimu yupo kwa ajili ya kuidhoofisha CHADEMA hivyo harakati za kupambana nao zinatakiwa kuwa za papo kwa hapo. CHADEMA imfungulie kesi huyo hakimu, na hao viongozi kutoka Zanzibar ilmradi nao wapate usumbufu wa kwenda mahakamani kusikiliza kesi Yao. Similar CHADEMA imfungulie kesi yule hakimu na mawakili wa serikali kwa kuchelewesha kesi ya Tundu Lissu ilmradi kwa majina Yao na wao wapate usumbufu wa kwenda mahakamani kusikiliza kesi zao. Kwa kesi hizi lazima watumishi wa mahakama wataanza kuwa na adabu. CHADEMA isikubali Kila siku TU yenyewe ndio inakuwa mhanga wa kupelekwa mahakamani na kuzungushwa kwa kupigwa tarehe.
 
Kauli ya katibu Mkuu kupitia ile barua ya chama , sio kwa bahati mbaya , japo anaweza kutumia maneno ya kiutuuzima
 
Chadema ifunguke kesi kwenye mahakama zipi? Hizi hizi zinazoendeshwa kwa memo? Ni kupoteza muda tu.

Chadema inazuiwa kuendesha harakati zake kwa kutumia kesi za kubumba ktk mahakama za mchongo
 
Chadema ifunguke kesi kwenye mahakama zipi? Hizi hizi zinazoendeshwa kwa memo? Ni kupoteza muda tu.

Chadema inazuiwa kuendesha harakati zake kwa kutumia kesi za kubumba ktk mahakama za mchongo
Sasa ipi njia ya kupambana na mifumo ya hovyo kama hiyo
 
We jamaa!! Kwenye mahakama hizi hizi na majaji hawa hawa!? CDM wanapaswa kufanya yote ili kushawishi umma tu. Nje ya hapo watakuwa wahanga siku zote. Waendelee kudili kuelimisha umma kwani yawapatayo kama taasisi ndio yanayowaumiza watanzania wote individually
 
Sasa ipi njia ya kupambana na mifumo ya hovyo kama hiyo
Ni kwa kuchapana na kuuana tu. Baada ya hapo ndiyo tutapata katiba mpya itakayoua mifumo kandamizi.

.Maana prof. Anna Tibaijuka alishasema, "kupata katiba mpya ktk mazingira ya amani tutasubiri sana"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…