Kesi dhidi ya Mbowe: Ushahidi wa Luteni Denis Urio ni muhimu sana

Ndugu zangu!

Kwa wale tunaofuatilia kwa ukaribu hii kesi pendwa, tutakumbuka maelezo muhimu kutoka kwa mashahidi wa pande zote mbili.

Kwenye kesi ya msingi, tulisikia ushahidi wa ACP Kingai akimtaja Luteni Denis Urio kuwa alitumika kama mtego kwa sharti la kuripoti kila hatua.

Kwa maelezo yake, Urio alihusika 'kumtafutia' Mbowe wasaidizi aliowahitaji. Ikawa hivyo.

Hapa tulitegemea kuwa Urio 'amemchoma' kwa kuripoti mipango yake inayoitwa ya ugaidi.

Lakini kwenye ushahidi wa kesi ndogo uliotolewa na Komandoo Ling’wenya (mtuhumiwa), yeye kamtaja Urio kuwepo kwenye moja ya mahabusu za hao wanaoitwa magaidi na amemshuhudia akipitia mateso kama hao wengine.

Hii inatupa mwelekeo gani? Kwanini mtu aliyetajwa kufanikisha ukamatwaji wa magaidi naye anakula kichapo?

Urio yupo upande gani?

Japo si mmoja wa mashahidi katika hii kesi ya msingi, lakini sasa ni rasmi ameingizwa na itabidi apande kizimbani.

Ushahidi wake unaweza kutusogeza hatua nyingi kuelekea kuufahamu ukweli, tunamhitaji Luteni Denis Urio kizimbani bila kukosa.

Ncha Kali.
Kupitia kesi hii ya ugaidi, wale walioitwa wasiojulikana zamani zile za utawala wa "Chato Village Champion" sasa wameanza kujulikana.
 
Huyo Denis hawezi kuwa shahidi wa utetezi ni msaliti na ametumika kutoa maelezo ya uongo ktk kuwachoma wenzake...

Labda Awe shahidi upande wa walalamikaji/ polisi...

Ni shahidi wa polisi obviously, ila sababu za kutekwa na kuswekwa mahabusu ni zipi?
 
Mawazo yangu Mawili ya Tofauti

1. Urio yupo upande wa Mashitaka (Shahidi mhimu) Isipokuwa ndani ya misheni Ilitakiwa pia Ateswe ili ionekane kuwa Ni mmoja ya watu waliokuwa kwenye Chain 1 ili kuwapoteza uelekeo wenzake.. Kwenye kesi ya Msingi huyu Ataibuka na kumaliza utata.. Sishangai kabisa Coz Kuna watu huwa wanafungwa Gerezani na kupitia mateso Tena makubwa ili tu Kukamilisha Misheni.. Siyo Rahisi Urio awe Shahidi upande wa Mbowe.

2. Lakini kama Yupo upande wa Utetezi yaani Kwa Mbowe Huenda Alitumika upande wa Selikali Kama Agent na Aliponogewa na Misheni Akaachana na Selikali naye Akajiunga Rasmi na Wanaoitwa Magaidi Kufanya Uhaini. Ngoja tuendelee kusubiri.
 
Hii kesi ikiendelea ni aibu kwa serikali na ikifutwa na DPP ni aibu kwa serikali. Aibu haikwepeki kwa serikali kwa njia yoyote ile, yani kunyoa au kusuka hawapendezi.
Hii ya JWTZ na Policc u drop kwa maana kuwa
1. Hao ni askari walioachishwa kazi hivyo si askari tena.
2. Askari akikwapua simu ya mtu uraiani au akifanya kosa polisi watakula naye. Court Marshall akifanya makosa ya kijeshi.

Fikirishi/Za kunyapia
Hao Komandoo walitengenezwa ili kummumaliza Uhuru lkn imeonekana wategaji hawakuwa makini ni terms au Komando wamekuwa double agents.
Game NZITO
 
Huyu dogo mpuuzi alitaka kupabda haraka vyeo kubumbulua deal ugaidi mjinga....ametumika kama toulet paper sasa kasaliti watu wenye lengo ulinzi Mbowe yeye alitaka kick hakuna kesi hapo attentipn nchi imehama sababu tip kijinga ndio maana nae kala kichapo ili kujirodhasha mjinga huyu Urio
Kwani huyo Urio bado ni muajiliwa wa jeshi au na yeye alishafukuzwa?
 
swala la Police kuwateka na kuwatesa Makomandoo wa JWTZ, ambao wana Mahakama, Mahabusu na Police wao (Military Police MP, Martial Courts, Martial Lock Ups) zao pindi wanapotenda kosa. Police walipata baraka kutoka wapi??? Kwa CDF Mabeyo au IGP Sirro au Rais???
Hapa mkuu kiri huelewi. Komandoo akiasi au kufukuzwa na akatenda kosa atashughulikiwa hata na sungu sungu achilia mbali polisi jamii
 
Hii kesi ikiendelea ni aibu kwa serikali na ikifutwa na DPP ni aibu kwa serikali. Aibu haikwepeki kwa serikali kwa njia yoyote ile, yani kunyoa au kusuka hawapendezi.

Pili, swala la Police kuwateka na kuwatesa Makomandoo wa JWTZ, ambao wana Mahakama, Mahabusu na Police wao (Military Police MP, Martial Courts, Martial Lock Ups) zao pindi wanapotenda kosa. Police walipata baraka kutoka wapi??? Kwa CDF Mabeyo au IGP Sirro au Rais???

Tatu, swala la usalama wa washtakiwa na mashahidi kwa hatua ya hii kesi ilipofikia, hatua gani zimechukuliwa kuwa hakikishia wana usalama huko mahabusu walipo hifadhiwa na pindi wanapo safirishwa kwenda mahakamani??? Tumeona wakisafirishwa kwa gari bovu lililogoma kuwaka mahakamani, je ikitokea msafara wao nje ya mahakama au barabarani kuvamiwa na watu wasiojulikana na kumiminiwa mzigo wa risasi ili kuficha aibu, hilo jambo litachukua taswira gani mbele ya dunia???

Swali la kizushi;

CDF wetu angekua ndio yule mwamba wa Guinea, bwana Kanali Mamady Doumbouya angekubaliana na mwenendo huu wa kulinajisi jeshi la nchi kwa kuwateka Makomandoo na kuwafanya waliofanywa (Kupigwa, Kuteswa na Kuchomwa bisibisi za makalioni)???
Hata Cdf Mwamunyange Davis asingeruhusu huu upumbavu
 
Endeleeni kuomboleza siku Hukumu yake ikitoka mtajua kuwa mlikuwa hamjui
 
Ndo akili zako za kibavicha zinavyokwambia?

Unafikiri maadili ya vyombo vyetu vya ulinzi ni kama hapo kwenu Bavicha?

Kwa taarifa yako, si Mara ya kwanza kwa vyombo vya ulinzi kushughulikia wahalifu kwenye nchi!

Fuatilia historia ya nchi hii utajua hata mwaka 1981 wanajeshi kadhaa walikamatwa na kupitia kibano kikali baada ya kufanya jaribio la kumpindua Nyerere!
Baadhi yao ni Luteni Zacharia Hanspope, Kapteni Maganga, Kapteni Kadego na Wengine.

Kwenye huo mpango wao alikuwepo Komandoo Tamimu ambaye aliuwawa na vyombo vya ulinzi maeneo ya magomeni baada ya kujaribu kutoroka akiwa anakamatwa

Bavicha mnajifanyaga mna akili kumbe vilaza wa mwisho hata historia ya nchi yenu hamuijui!

Tanzania haijawai kuwa legelege kwenye kudeal na wahalifu haijalishi wewe ni nani
Irrelevant
 
Acha upotoshaji wa makusudi, hao watu walishatimuliwa jeshini hivyo ni raia wa kawaida tu na wanakuwa treated kama raia, ndiyo maana waliweza hata kuomba kazi ya ulinzi kwa bwana Mwamba.
Jiulize kwa nini wakiuguwa kaxini wanatimuliwa CDF Mabeyo analo lakujibu kwa nini ameruhusu makomandoo kuchezewa na vichwa vya panzi akina kingai matata msemwa goodluck. Yeye na sirro lazima wapandishwe kizimbani
 
Na wao makomando kwa nini hawakuvunja koromeo hata polisi mmoja? Mbona yule tajiri wa Mara alichakaza risasi wasiojulikana kwa ujinga kama huu huu waliofanyiwa hawa makomando? Na baadaye alionekana hana kosa
 
Ndugu zangu!

Kwa wale tunaofuatilia kwa ukaribu hii kesi pendwa, tutakumbuka maelezo muhimu kutoka kwa mashahidi wa pande zote mbili.

Kwenye kesi ya msingi, tulisikia ushahidi wa ACP Kingai akimtaja Luteni Denis Urio kuwa alitumika kama mtego kwa sharti la kuripoti kila hatua.

Kwa maelezo yake, Urio alihusika 'kumtafutia' Mbowe wasaidizi aliowahitaji. Ikawa hivyo.

Hapa tulitegemea kuwa Urio 'amemchoma' kwa kuripoti mipango yake inayoitwa ya ugaidi.

Lakini kwenye ushahidi wa kesi ndogo uliotolewa na Komandoo Ling’wenya (mtuhumiwa), yeye kamtaja Urio kuwepo kwenye moja ya mahabusu za hao wanaoitwa magaidi na amemshuhudia akipitia mateso kama hao wengine.

Hii inatupa mwelekeo gani? Kwanini mtu aliyetajwa kufanikisha ukamatwaji wa magaidi naye anakula kichapo?

Urio yupo upande gani?

Japo si mmoja wa mashahidi katika hii kesi ya msingi, lakini sasa ni rasmi ameingizwa na itabidi apande kizimbani.

Ushahidi wake unaweza kutusogeza hatua nyingi kuelekea kuufahamu ukweli, tunamhitaji Luteni Denis Urio kizimbani bila kukosa.

Ncha Kali.
Shahidi anasema Urio aliteswa je Urio mwenyewe akiletwa na akasema hajateswa vipi ushahidi wa watuhumiwa wote utakuwabatili?
 
Back
Top Bottom