Uchaguzi 2020 Kesho ya WanaCCM ipo miguuni mwao kujitakasa mbele ya Rais Lissu

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Masaa ya Ukombozi yanakaribia tujitwalia Uhuru wetu kwa kura zetu. Kwenye diplomasia ya utawala kuna msemo wa kiswahili wenye maana sana unasema, "Wali wa kushiba huonekana kwenye sahani". Hii inamaana kwamba Lissu anashinda Uchaguzi huu uwe unapenda au hupendi. Sasa kwenye siasa za vyama vingi unapokuwa kiongozi uliyepo madarakani katika uchaguzi ulio mbele yako ambao wewe ni sehemu ya mshiriki, dalili za kuanguka huanzia kwenye chama chako Kisha huja kwenye serikali unayoiongoza.

Ukiona hayo, kidiplomasia huwa tunaanza kutengeneza njia zako za kesho hasa za maslahi yako na ya wakuzungukao, Bahati mbaya wengi kwakibri cha madaraka huwa hawaoni hili. Hapa unaanza kutafuta kitu kinaitwa maridhiano, haijalishi una majeshi, ama una polisi. Ifahamike kuwa kwenye Vita vya madaraka majeshi hukuunga mkono hatua za mwanzo tu kutisha umma na kukujaza kibri kuwa yatakulinda utabaki madarakani, Lakini hali ikivuka kipimo kidogo cha kiusalama, Jeshi la umma hujitenga nawe hukaa kwa waliowengi.

Sasa kwa mtawala anayeiangalia kesho yake na washauri wake wanaoiangalia kesho yao, humshauri mtawala kutafuta njia rahisi na salama ya kupita na kuiona kesho na kuiishi kesho.

Kwa mifano ya karibu kabisa ya walioona upepo wa kuanguka kwa vyama vyao na wakapuuza au wakakwepa kizuizi cha kuiona kesho, ni Joseph Kabila kule Kongo, Hayati Nkuruzinza kule Burundi, Daniel Arap Moi kule Kenya, nk. Na mifano ya waliokomaza shingo yakawakuta ni Laurent Gbagbo kule Ivory coast, Charles Taylor kule Liberia, Yahya Jammeh wa Gambia nk. Ukiachilia mbali Zambia, Malawi nk.

Nitumie fursa hii kuwashauri CCM popote walipo kwa ngazi zote kuanzia Mwenyekiti wao Taifa ndugu Magufuli, hadi akina Chakubanga, waanze kutafuta maridhiano ya kidiplomasia wakati wakijiandaa kukabidhi madaraka wiki hii, Njia nzuri ya kuondoka madarakani ni kuondoka huku ukiijua kesho yako (Kikatiba) kuliko kutumia muda huu kufikiria ma V8 na anasa zingine katika utawala unaoondoka.

Kwamjibu wa Katiba, mkikabidhi madaraka kwa hiyari ya Kikatiba, maslahi yenu yatalindwa Kikatiba. Fikirieni kinyume chake kisha kesho yenu na vizazi vyenu.

Ni ushauri tu, kuanzia wiki ijayo mtanikumbuka na kunishukuru.

Na Yericko Nyerere
 
Umenena kijana yeye mwenyewe amesema tufanye mabadiliko

IMG_20201019_222544.jpeg
 
Farao wa Misri na wafuasi wake ni ngumu kuelewa hili.

Ni wajinga hawa. Mwisho wao wataingia na kujizika wenyewe ndani ya Bahari ya Shamu.

Walishajiapiza kuwa, Mungu [YEHOVA] APENDE ama ASIPENDE; ATAKE ama ASITAKE eti mtu wao MAGUFULI lazima ashinde tu.

Kauli hii ya KUFURU iliyopindukia ndiyo imechora mstari wa mwisho wao.

There's no way out to save themselves.
 
Alijua alichokuwa anakiongea kweli huyu mzee?

Anataka afanye mabadiliko ya kweli? Yepi? Kumbe haya wafuasi wake wanayoyaimba ni magumashi tu, ni uongo tu, right?

For sure kabisa, kuwaelewa CCM na mgombea wao ni lazima kwanza uwe chizi kama wao!
Magufuli CCM atawaacha kwenye atakapowambia nakabidhi nchi kwa lisu usije shangaa likatokea hilo maana akili zake ni dakika mbili mbele.
 
Masaa ya Ukombozi yanakaribia tujitwalia Uhuru wetu kwa kura zetu. Kwenye diplomasia ya utawala kuna msemo wa kiswahili wenye maana sana unasema, "Wali wa kushiba huonekana kwenye sahani". Hii inamaana kwamba Lissu anashinda Uchaguzi huu uwe unapenda au hupendi. Sasa kwenye siasa za vyama vingi unapokuwa kiongozi uliyepo madarakani katika uchaguzi ulio mbele yako ambao wewe ni sehemu ya mshiriki, dalili za kuanguka huanzia kwenye chama chako Kisha huja kwenye serikali unayoiongoza.

Ukiona hayo, kidiplomasia huwa tunaanza kutengeneza njia zako za kesho hasa za maslahi yako na ya wakuzungukao, Bahati mbaya wengi kwakibri cha madaraka huwa hawaoni hili. Hapa unaanza kutafuta kitu kinaitwa maridhiano, haijalishi una majeshi, ama una polisi. Ifahamike kuwa kwenye Vita vya madaraka majeshi hukuunga mkono hatua za mwanzo tu kutisha umma na kukujaza kibri kuwa yatakulinda utabaki madarakani, Lakini hali ikivuka kipimo kidogo cha kiusalama, Jeshi la umma hujitenga nawe hukaa kwa waliowengi.

Sasa kwa mtawala anayeiangalia kesho yake na washauri wake wanaoiangalia kesho yao, humshauri mtawala kutafuta njia rahisi na salama ya kupita na kuiona kesho na kuiishi kesho.

Kwa mifano ya karibu kabisa ya walioona upepo wa kuanguka kwa vyama vyao na wakapuuza au wakakwepa kizuizi cha kuiona kesho, ni Joseph Kabila kule Kongo, Hayati Nkuruzinza kule Burundi, Daniel Arap Moi kule Kenya, nk. Na mifano ya waliokomaza shingo yakawakuta ni Laurent Gbagbo kule Ivory coast, Charles Taylor kule Liberia, Yahya Jammeh wa Gambia nk. Ukiachilia mbali Zambia, Malawi nk.

Nitumie fursa hii kuwashauri CCM popote walipo kwa ngazi zote kuanzia Mwenyekiti wao Taifa ndugu Magufuli, hadi akina Chakubanga, waanze kutafuta maridhiano ya kidiplomasia wakati wakijiandaa kukabidhi madaraka wiki hii, Njia nzuri ya kuondoka madarakani ni kuondoka huku ukiijua kesho yako (Kikatiba) kuliko kutumia muda huu kufikiria ma V8 na anasa zingine katika utawala unaoondoka.

Kwamjibu wa Katiba, mkikabidhi madaraka kwa hiyari ya Kikatiba, maslahi yenu yatalindwa Kikatiba. Fikirieni kinyume chake kisha kesho yenu na vizazi vyenu.

Ni ushauri tu, kuanzia wiki ijayo mtanikumbuka na kunishukuru.

Na Yericko Nyerere
Nyerere aliwahi kusema:
"Watanzania wanataka MABADILIKO. Wasipoyapata ndani ya ccm, watayatafuta nje ya ccm..."

Muda wa mabadiliko ni sasa!
Ni YEYE 2020 - 2025
 
Back
Top Bottom