KESHO NENDA KIJIJINI KAMCHEKI MOTHER.

KESHO NENDA KIJIJINI KAMCHEKI MOTHER.

moyafricatz

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2015
Posts
2,905
Reaction score
4,948
*TUMIA DAKIKA 3 KUSOMA HII*

Lameck alikuwa akiendesha gari kwa kasi sana. Mara akakutana na akina Mama watatu ambao walinyoosha mkono kumuomba lift.

Ingawa alikua na haraka lakini aliwaonea huruma na kusimama, sehemu waliyokuwa ilikuwa ni kichakani na kwakuwa alikuwa peke yake hakuona sababu ya kuwanyima lift.

“Samahani Baba, tunaomba utusaidie tunaelekea, Usangi kwenye msiba sasa tumechelewa na magari hamna…” Mama mmoja aliomba.

Lameck aliwaambia waingie kwani hata yeye alikuwa anaelekea huko huko.

Wale akina mama waliingia kwenye gari aliwasalimia na bila hata kuulizwa walianza kujielezea.

“Tunaenda kwenye msiba, kuna Mama mmoja kafariki huko...” Mama mmoja alianza kuongea na mwingine aliendelea…

"...Ahsante sana mwanangu, ni vijana wachache sana wenye roho nzuri kama wewe, wenzako wametupita kama sisi sio watu, magari mazuri kama haya yenu hata hayasimamagi.

Huko tunakoenda kuzika huyo Mama wa watu kaumwa kateseka lakini mtoto wake mwenyewe wa kumzaa hata hakuja kumuangalia, majirani ndiyo walimchangia kupelekwa KCMC…”

“Yaani watoto wasiku hizi mpaka mtu unajuta kuzaa, yule Mama alivyohangaika kumsomesha yule mtoto, alikua anatembea na mfuko wa viazi kwenda kuuza sokoni, anafanya vibarua mtoto mwenyewe hata akili alikua hana kila siku kufeli anarudia madarasa lakini Mama wawatu alivumilia.”

Mama mwingine aliongea.
“Tena basi alitelekezwa na mume wake.” Aliongea Mama mwingine.

“…Alikua mume basi, alizaa na msukuma mmoja aliyekuja kufanya vibarua akamkimbia na kumuacha na mtoto mdogo, Mama wa watu kalea mwenyewe mtoto huyo huyo mmoja ila kajumba kalekale ka nmatope ndiyo Mama wa watu kafia wakati mwanae yuko mjini anakula maisha…!”

“Mama wawatu kila siku analia hata aletewe wajukuu tu awaone…”
“Nakuambia, kila siku anasema mimi sitaki hata pesa zake aniletee tu wajukuu zangu na mimi nifurahie kuzaaa..”

“Kijana yuko mjini wala hana habari! Hawa watoto jamani! Heri Mama wa watu alivyokufa akampumzike, ameteseka sana, nasikia walishamtoa jicho lapili alikuwa haoni kabisa…”
“Usiniambie..”

“Kweli eee, mimi nilienda, majirani walikuwa wamemchangia KCMC wakamtoa jicho lingine, Kansa sio mchezo…”
“Sema kuishi na watu vizuri ni jambo jema sana maana asingekuwa na majirani angekua ashakufa muda mrefu... mtoto wa kumzaa anaweza asikusaidie lakini wa jirani akakusaidia..”

Kule mbele Lameck alikuwa akibubujikwa na machozi, yeye ndiye kijana walikuwa wakimzungumzia na Mama yake ndiyo alikuwa amefariki, tangu alipoenda mjini miaka 15 iliyopita alikuwa hajakanyaga tena nyumbani, alioa bila hata kumuambia Mama yake na hata alipojua aligoma kabisa kumpeleka mkewe na wanae nyumbani.

Maneno ya wale akina Mama yalimuumiza sana hasa walipozungumzia namna Mama yake alivyohangaika naye wakati akiwa mdogo, picha ya Mama yake akilima vibarua, namna alivyokuwa akitoka jasho, picha za mama yake akinyeshewa na mvua, picha za mama yake akatika ofisi za mwalimu mkuu wakati akimtete asifukuzwae shule, picha za Mama yake akimuwashia kibatari usiku ili asome vyote vilimjia akilini.

Alijiona hanathamani kwani hata baada ya kusikia kifo cha Mama yake alishindwa kufanya kitu amabcho Mama yake alikuwa akimuomba kila mara alipompigia simu. Hakutaka kuileta familia yake, hakutaka mke wake na wanae kuona sehemu alipozaliwa kuona hali ya nyumbani kwao hivyo aliamua kwenda mwenyewe mara moja kumaliza mazishi na kugeuza.

Aliumia zaidi aliposikia kuwa kumbe Mama yake alikuwa na Kansa na alitolewa macho yote, hakua na habari hizo kani ni zaidi ya miaka miwili alikuwa hajawasiliana na Mama yake. Mama yake baada ya kumuona hajibu na hamsaidii chochote alichoka kumpigia simu hivyo hata hakujua kuhusu ugonjwa wake.

Machozi yalianza kumbubujika kama maji, alijihisi kama kizunguzungu na kila alipojaribu kulicontrol gari alishindwa, gari liliacha njia na kuserereka mlimani. Alipoteza fahamu na alipozinduka masaa sita baadaye alijikuta amelala hospitalini, aliambiwa amepata ajali, ndipo alipokumbuka ajali ilivyotokea.

Aliulizia kuhusu kina Mama aliokuwa amewabeba akaambiwa walitoka salama bila hata mchubuko, alimshukuru Mungu kwa hilo, hakuwa akisikia maumivu kokote lakini alipojaribu kunyanyuka alishindwa hata kunyanyua kidole. Lameck alikuwa amevunjika uti wa mgongo karibu na shingo hivyo alipooza kuanzia mabegani kushuka chini.

Alipelekwa hospitali kubwa lakini ilishindikana, walimpeleka mpaka nje ya nchi lakini bado ilishindikana. Ni miaka mitatu sasa bado hajaweza kunyanyuka amelala akiwa hawezi kufanya kitu chochote kile. Mke wake ameshaolewa na mwanaume mwingine na wanae wanakuja mara moja moja kumsailimia katika nyumba anayoishi ambayo mkewe ameajiri kijana kwa ajili ya kumhudumia.

Lameck amebaki mpweke marafiki wote wamemtenga, hata wanae wanapokuja kumsalimia humuangalia kama kituko flani, huishia tu kumuonea huruma, hana mtu wakuongea naye. Amelia mpaka amechoka, anatamani kufa lakini hawezi hata kunyanyua mkono kuchukua sumu ajiue. Kila siku ni kulia na kumuomba mama yake msamaha.

*Me sikuambii ujifunze nini hapo,ila we endelea tu kujifanya "Me kwetu Dar"...*

*Kesho nenda kijijini kwenu kamcheki mother.*
 
Mwenyezi Mungu hakuweka Pepo chini ya miguu ya mama bure tu.

Tuwadhamini wazazi wetu, tuwaheshimu, tuwatunze na kuwajali.

Wametuleta duniani, wamehangaika kwa hali na mali mpaka tumekuja kupata akili na kujisimamia. Tumewazeesha na nguvu zao zimeishia katika malezi yetu. Tangu tunapisafishwa tukijisaidia, tangu tunauguzwa tukiugua... mpaka tumekuja kupata akili.

Na wale ambao wamekwazana na wazazi wao katika njia moja ama nyingine, kubalini kujishusha na muyamalize mpate kumridhisha Muumba wenu. Wazazi ni binaadamu kama sisi, hawapo perfect pia.
 
Iwe ni hadithi, simulizi au kisa cha ukweli. Kuna kitu cha kujifunza kwenye hili bandiko.

Kuna vitu hatuvipi umuhimu au kipaumbele kwa kufikiria tunao muda wote maishani na tutaishi milele.
 
Sawa kaka,
Wengine sisi mama zetu pia huja mjiji kutucheki sisi. So sio lazima kwenda huko shamba.

Pia Lameck akome kuwapa watu lift, kuna wenzio walifanywa kitu mbaya kuliko hata mateso ya yesu.

Unafanya wema kumbe ndo tiketi ya kulichungulia kaburi mapema na kuacha dunia hii tamu.

Sisi tushajiapia Dar hatuondoki mpk Makonda atengue kauli yake. Hata hali iwe mbaya vipi,tutafia na tai shingoni.

Zaidi yeye na baba yake ndo naona wanatuachia Dar na kwenda kwa wagogo huko.
 
Cha msingi sio kwenda mkoani kuwajulia hali. Unaweza hata ukawahamishia jijini kabisa au usiende kijijini.

Tunachoongelea ni ile kuwa na mahusiano mazuri yenye afya na wazazi.
 
Cha msingi sio kwenda mkoani kuwajulia hali. Unaweza hata ukawahamishia jijini kabisa au usiende kijijini.

Tunachoongelea ni ile kuwa na mahusiano mazuri yenye afya na wazazi.
Mama/baba hawapapendi sana Dar kutokana na joto na vurugu zake.

So wakija watakaa km wiki mbili wanarudi. Na huwa wanakuja km kuna event i.e harusi.

Kujali hata mawasilianobya simu kwa dunia ya sasa yenye mitikasi inatosha sana
 
Sawa kaka,
Wengine sisi mama zetu pia huja mjiji kutucheki sisi. So sio lazima kwenda huko shamba.

Pia Lameck akome kuwapa watu lift, kuna wenzio walifanywa kitu mbaya kuliko hata mateso ya yesu.

Unafanya wema kumbe ndo tiketi ya kulichungulia kaburi mapema na kuacha dunia hii tamu.

Sisi tushajiapia Dar hatuondoki mpk Makonda atengue kauli yake. Hata hali iwe mbaya vipi,tutafia na tai shingoni.

Zaidi yeye na baba yake ndo naona wanatuachia Dar na kwenda kwa wagogo huko.

Hauwatamani ndugu zako wengine?

Hautamani kuona Mama anaishi katika mazingira gani? Unamuona kisa anakuja mjini kafungasha zawadi kibao basi kila kitu fresh.

Ngoja nikuambie, sio ujanja kutoenda shamba. Fanya uende ukamuangalie Mom anaishi katika mazingira gani.

Bati linahitaji kubadilishwa? Godoro je, Angalia Mama analala wapi.... Vyombo vyake je? Choo ni kile kile ulikiacha hakihitaji matengenezo.

Go visit your Mama honey. Let her feel the pride of showing off her grown son to the villagers. The boy she put to school with every penny she had, and who made it big and now lives in the City.

That feeling is priceless. All the best.
 
Mama/baba hawapapendi sana Dar kutokana na joto na vurugu zake.

So wakija watakaa km wiki mbili wanarudi. Na huwa wanakuja km kuna event i.e harusi.

Kujali hata mawasilianobya simu kwa dunia ya sasa yenye mitikasi inatosha sana

Huo mstari wa mwisho ndio nilikua nauhitaji. Kujali. Kama una mawasiliano nao hata wakiwa na tatizo au uhitaji wa msaada utajua na kuwasaidia.
 
Hauwatamani ndugu zako wengine?

Hautamani kuona Mama anaishi katika mazingira gani? Unamuona kisa anakuja mjini kafungasha zawadi kibao basi kila kitu fresh.

Ngoja nikuambie, sio ujanja kutoenda shamba. Fanya uende ukamuangalie Mom anaishi katika mazingira gani.

Bati linahitaji kubadilishwa? Godoro je, Angalia Mama analala wapi.... Vyombo vyake je? Choo ni kile kile ulikiacha hakihitaji matengenezo.

Go visit your Mama honey. Let her feel the pride of showing off her grown son to the villagers. The boy she put to school with every penny she had, and who made it big and now lives in the City.

That feeling is priceless. All the best.
Aisee,
Mama na baba walisha tengeneza mji wao tangu ujana wao. Vitu ulivyo vieleza ni vidogo sana vya kunishawishi kwenda kuangalia vikoje kwani vyawezwa kununuliwa tu.

Hata wao wanaweza kuvinunua, hawana shida kihivyo. Kuna kaka zangu na dada zangu ambao wana uchumi mkubwa kuliko mimi.

Hata wakija Dar hawaji kwangu kwani mimi bado bachela. Wanaishia kwa broh.
 
Uende shamba ba mdogo.

Some day ukishakuwa mzazi you will understand better.
 
Mola Wako Anakuamrisha Uwafanyie Wema Wazazi Wako Ili Akulipe Pepo
Familia-Jamii
Anasema Allaah ﺳﺒﺤﺎﻧﻪ ﻭﺗﻌﺎﻟﻰ :
)) ﻭَﻗَﻀَﻰ ﺭَﺑُّﻚَ ﺃَﻻَّ ﺗَﻌْﺒُﺪُﻭﺍْ ﺇِﻻَّ ﺇِﻳَّﺎﻩُ ﻭَﺑِﺎﻟْﻮَﺍﻟِﺪَﻳْﻦِ ﺇِﺣْﺴَﺎﻧًﺎ ﺇِﻣَّﺎ ﻳَﺒْﻠُﻐَﻦَّ ﻋِﻨﺪَﻙَ ﺍﻟْﻜِﺒَﺮَ ﺃَﺣَﺪُﻫُﻤَﺎ ﺃَﻭْ ﻛِﻼَﻫُﻤَﺎ ﻓَﻼَ ﺗَﻘُﻞ ﻟَّﻬُﻤَﺂ ﺃُﻑٍّ ﻭَﻻَ
ﺗَﻨْﻬَﺮْﻫُﻤَﺎ ﻭَﻗُﻞ ﻟَّﻬُﻤَﺎ ﻗَﻮْﻻً ﻛَﺮِﻳﻤًﺎ (( )) ﻭَﺍﺧْﻔِﺾْ ﻟَﻬُﻤَﺎ ﺟَﻨَﺎﺡَ ﺍﻟﺬُّﻝِّ ﻣِﻦَ ﺍﻟﺮَّﺣْﻤَﺔِ ﻭَﻗُﻞ ﺭَّﺏِّ ﺍﺭْﺣَﻤْﻬُﻤَﺎ ﻛَﻤَﺎ ﺭَﺑَّﻴَﺎﻧِﻲ ﺻَﻐِﻴﺮًﺍ ((
((Na Mola wako Ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa he shima)) ((Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma. Na useme: Mola wangu, Warehemu kama walivyonilea utotoni)) [Al-Israa:23-24]
Kumuabudu Allaah ﺳﺒﺤﺎﻧﻪ ﻭﺗﻌﺎﻟﻰ kumeungamana na kuwaheshimu wazazi kwani Allaah ﺳﺒﺤﺎﻧﻪ ﻭﺗﻌﺎﻟﻰ Ameamrisha kuwafanyia wema baada ya kuamrisha kumuabudu Yeye kama Alivyounganisha vile vile katika aya nyingine ya kumshukuru kwanza Yeye kisha wazazi:
)) ﻭَﻭَﺻَّﻴْﻨَﺎ ﺍﻟْﺈِﻧﺴَﺎﻥَ ﺑِﻮَﺍﻟِﺪَﻳْﻪِ ﺣَﻤَﻠَﺘْﻪُ ﺃُﻣُّﻪُ ﻭَﻫْﻨًﺎ ﻋَﻠَﻰ ﻭَﻫْﻦٍ ﻭَﻓِﺼَﺎﻟُﻪُ ﻓِﻲ ﻋَﺎﻣَﻴْﻦِ ﺃَﻥِ ﺍﺷْﻜُﺮْ ﻟِﻲ ﻭَﻟِﻮَﺍﻟِﺪَﻳْﻚَ ﺇِﻟَﻲَّ ﺍﻟْﻤَﺼِﻴﺮُ ((
((Na Tumemuusia mtu kwa wazazi wake wawili. Mama yake ameichukua mimba yake kwa udhaifu juu ya udhaifu, na kumwachisha ziwa baada ya miaka miwili. (Tumemuusia): Nishukuru Mimi na wazazi wako. Ni Kwangu Mimi ndiyo marudio)) [Luqmaan:14]
Mtume ﺻﻠﻰ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻠﻴﻪ ﻭﺁﻟﻪ ﻭﺳﻠﻢ ametupa mafundisho katika Hadiyth zake nyingi kuhusu kuwaheshimu na kuwafanyia wema wazazi wetu:
ﻋﻦ ﺃﻧﺲ ﻭﻏﻴﺮﻩ : ﺃﻥ ﺭﺳﻮﻝ ﺍﻟﻠﻪ ﺻﻠﻰ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻠﻴﻪ ﻭﺳﻠﻢ ﻟﻤﺎ ﺻﻌﺪ ﺍﻟﻤﻨﺒﺮ ﻗﺎﻝ : )) ﺁﻣﻴﻦ ﺁﻣﻴﻦ ﺁﻣﻴﻦ 🙁( ﻓﻘﺎﻟﻮﺍ : ﻳﺎ ﺭﺳﻮﻝ ﺍﻟﻠﻪ، ﻋﻼﻡ ﺃﻣﻨﺖ؟ ﻗﺎﻝ : )) ﺃﺗﺎﻧﻲ ﺟﺒﺮﻳﻞ ﻓﻘﺎﻝ : ﻳﺎ ﻣﺤﻤﺪ ﺭﻏﻢ ﺃﻧﻒ ﺍﻣﺮﺉ ﺫﻛﺮﺕ ﻋﻨﺪﻩ ﻓﻠﻢ ﻳﺼﻞ ﻋﻠﻴﻚ، ﻓﻘﻞ : ﺁﻣﻴﻦ . ﻓﻘﻠﺖ : ﺁﻣﻴﻦ . ﺛﻢ ﻗﺎﻝ : ﺭﻏﻢ ﺃﻧﻒ ﺍﻣﺮﺉ ﺩﺧﻞ ﻋﻠﻴﻪ ﺷﻬﺮ ﺭﻣﻀﺎﻥ ﺛﻢ ﺧﺮﺝ ﻭﻟﻢ ﻳﻐﻔﺮ ﻟﻪ، ﻗﻞ : ﺁﻣﻴﻦ . ﻓﻘﻠﺖ ﺁﻣﻴﻦ . ﺛﻢ ﻗﺎﻝ : ﺭﻏﻢ ﺃﻧﻒ ﺍﻣﺮﺉ ﺃﺩﺭﻙ ﺃﺑﻮﻳﻪ ﺃﻭ ﺃﺣﺪﻫﻤﺎ ﻓﻠﻢ ﻳﺪﺧﻼﻩ ﺍﻟﺠﻨﺔ، ﻗﻞ : ﺁﻣﻴﻦ . ﻓﻘﻠﺖ : ﺁﻣﻴﻦ ((
Kutoka kwa Anas na wengineo kwamba Mtume ﺻﻠﻰ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻠﻴﻪ ﻭﺁﻟﻪ ﻭﺳﻠﻢ alipanda katika minbar na akasema🙁(Aamiyn, Aamiyn, Aamiyn)). Akaulizwa: Ewe Mjumbe wa Allaah, mbona umesema Aamiyn? Akasema: ((Amenijia Jibriyl na kuniambia: "Ewe Muhammad, amekhasirika yule anayekusikia (unatajwa) na hakuswalii". Akasema: "Sema Aamiyn", ndio nikasema Aamiyn. Kisha akasema: "Amekhasirika unayemfikia mwezi wa Ramadhaan na ukaondoka naye hakughufuriwa" (dhambi zake). Akasema: "Sema Aamiyn", ndio nikasema Aamiyn. Kisha akasema: "Amekhasirika yule anayekuwa mkubwa kisha wazazi wake wawili au mmoja wao bado yu hai, na wasiwe sababu yake kuingia Peponi". Akasema: "Sema Aamiyn", ndio nikasema Aamiyn)) [Tuhfat Al-Ahwadhiy 5:550]
Hadiyth nyingine:
ﻋﻦ ﺃﺑﻲ ﻫﺮﻳﺮﺓ، ﺭﺿﻲ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻨﻪ، ﻋﻦ ﺍﻟﻨﺒﻲ ﺻﻠﻰ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻠﻴﻪ ﻭﺳﻠﻢ ﻗﺎﻝ : )) ﺭﻏﻢ ﺃﻧﻒ، ﺛﻢ ﺭﻏﻢ ﺃﻧﻒ، ﺛﻢ ﺭﻏﻢ ﺃﻧﻒ ﺭﺟﻞ ﺃﺩﺭﻙ ﻭﺍﻟﺪﻳﻪ ﺃﺣﺪﻫﻤﺎ ﺃﻭ ﻛﻼﻫﻤﺎ ﻋﻨﺪ ﺍﻟﻜﺒﺮ ﻭﻟﻢ ﻳﺪﺧﻞ ﺍﻟﺠﻨﺔ ((
Imetoka kwa Abu Hurayrah ﺭﺿﻲ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻨﻪ kwamba Mtume ﺻﻠﻰ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻠﻴﻪ ﻭﺁﻟﻪ ﻭﺳﻠﻢ amesema: ((Amekhasirika, amekhasirika, amekhasirika, mtu ambaye wazazi wake wawili au mmoja wao wamefikia umri mkubwa (wa uzee) naye yu hai bado na haingii Peponi [kwa sababu ya kutowafanyia wema])) [Ahmad: 2:346]
Kuwafanyia wema wazazi kunaendelea hata kama mzazi mmoja au wote wawili wamefariki, wema huo unaweza kuuendeleza kwa kuwaombea Du'aa, kuwatolea sadaka, kuwafanyia Hajj na kadhalika, na yote
yamethibiti katika Sunnah.
Kwa hiyo kama tunavyoona umuhimu wa kuwaheshimu wazazi wetu na kuwafanyia wema, basi tujitahidi kutekeleza amri za Mola wetu ili kupata Ridhaa Yake na Atulipe Pepo.
 
Aise. Angefika msibani so wangemswalika sana huko waombolezaji. Nazani wangemwitia mwizi.

Kila jambo hutokea kwa malengo. Kupata ajali yaweza kuwa funzo kwa ajili take..Wewe na Mimi. Na nduguze wengine na hata Watoto wake.
 
Me bi mkubwa wangu ni rafiki yangu wa karibu sana na ndio maana nazidi kufanikiwa kila siku japo anaishi mbali na mimi kidogo.
 
Dah!you story unaweza kulia aisee
 
Wengi huwa tunajisahau sana tukishafika mjini na kuwa na maisha bora,tunaona wazazi si kitu tena
Mtu anakaa mjini hana hata mawasiliano ya wazazi wake,wanahasahu shida zote na kujitoa kote kwa wazazi sababu yetu.
Kiukweli wazazi wengi wanapata shida sana huko vijijini,hatuwajali,muda wa kwenda kuwaona tunajifanya hatuna kwa kisingizio cha kutafuta maisha.

Mungu atujaalie kheri tuweze wafantia wema wazazi wetu kama walivyotufantia sisi tulipokuwa watoto[emoji120][emoji120]
 
Aisee,
Mama na baba walisha tengeneza mji wao tangu ujana wao. Vitu ulivyo vieleza ni vidogo sana vya kunishawishi kwenda kuangalia vikoje kwani vyawezwa kununuliwa tu.

Hata wao wanaweza kuvinunua, hawana shida kihivyo. Kuna kaka zangu na dada zangu ambao wana uchumi mkubwa kuliko mimi.

Hata wakija Dar hawaji kwangu kwani mimi bado bachela. Wanaishia kwa broh.

Pamoja na mambo yote hayo, bado kuna umuhimu wa kwenda kuwasabahi au kuwajulia hali wazee mkuu. Tena wewe una bahati hauna vitu vingi vua kwenda kufanya wala wazee hawahitaji pesa yako, wewe tu wakuone, inawapa raha sana.

Kama anavyoshauri Karucee fanya hivyo kwa ajili yao jata kama kwako haina umuhimu sana, wape furaha ukipata fursa mkuu.
 
Back
Top Bottom