Kingsmann
JF-Expert Member
- Oct 4, 2018
- 4,448
- 16,314
KESHO WATAUANA LIGI KUU
Bingwa wa ligi kuu Tanzania bara msimu huu ameshajulikana, sasa hivi vita imehamia bondeni ambako timu zipo kwenye harakati za kuhakikisha zinabaki mwenye ligi kwa ajili ya msimu ujao.
.
Msimu huu timu mbili za chini (nafasi ya 19 na 20) zinashuka daraja moja kwa moja. Timu nyingine mbili zitakazomaliza (nafasi ya 17 na 18) zitacheza play-off na timu 4 (zilizomaliza nafasi ya 2 na 3 kwenye Kundi A na B) ligi daraja la kwanza.
.
Katika mechi za play-offs, timu mbili zitafuzu kucheza ligi kuu msimu ujao zikijumuika na mbili zilizofuzu moja kwa moja kutoka Kundi A na B za ligi daraja la kwanza.
Ni African Lyon pekee ndio timu ambayo tayari imeshuka daraja hadi sasa, kuna timu nyingine moja ambayo itaungana na Lyon halafu mbili zitakazomaliza nafasi ya 17 na 18 zitacheza play-off.
.
Ukiangalia msimamo, kuanzia nafasi ya 12 kushuka chini, kila timu haiko salama, ikitokea inapoteza mchezo wa mwisho basi inaweza kujikuta inacheza play-off kama wapinzani wake wanapata matokeo ya ushindi.
.
Ratiba inazikutanisha timu nyingi ambazo zinapigana kubaki kwenye ligi, wote wakiwa wanahitaji ushindi. Mechi zinazozihusisha timu ambazo zipo nafasi ya 12 hadi 19 zinamaana kubwa lakini utamu zidi unakuwa pale mechi zinakututanisha timu zote zinazotafuta nafasi ya kubaki kwenye ligi.
MECHI ZA MWISHO: #LigiKuuTanzaniaBara
Mtibwa Sugar vs Simba SC
Yanga SC vs Azam FC
Coastal Union vs Singida United
Mwadui FC vs Ndanda SC
JKT Tanzania vs Stand United
Ruvu Shooting vs Alliance FC
Mbeya City vs Biashara United
Mbao FC vs Kagera Sugar
Tanzania Prisons vs Lipuli FC
African Lyon vs KMC FC.
Credit:Shaffihdauda