Kesho nataka kuwaamini POLISI, nani anipe muongozo?

Kesho nataka kuwaamini POLISI, nani anipe muongozo?

Joined
Dec 11, 2010
Posts
3,321
Reaction score
6,331
Sitaki iwe mbali bali mapema sana kesho asubuhi nataka nitii bila kushurutushwa na mtu yoyote maana wengine wamesha sema kuwa wamechoka na mchoko wao wamesha uhalalisha kwa kupitisha amri, amri ambayo mahakama imedhibitisha kuwa ilikuwa amri ya kipumbavu kutoka kwa mtoto wa mkulima aliyezoea mji na kuanza kupinda.
"...Mtapigwa tu nami nasema mpigwe tu maana sasa tumechoka..." Ndioo, tumesha anza kupigwa na tutapigwa tu!

Kesho asubuhi na mapema nafanya maamuzi ya busara, busara imenituma nianze kuwaamini polisi, walinda usalama wetu na amani yetu, polisi wenye mapenzi mema na nchi yetu, polisi wanao linda na si kuuwa raia wa nchi hii, polisi wanao lipwa kwa kodi za watanzania, polisi wenye mabomu, magari ya maji ya kuwasha na bunduki zinazo tokana na kodi za watanzania, nataka kuwaamini kwa moyo wote. Ninacho hitaji ni muongozo!

Kesho nataka kuwaamini polisi walio kuwa pale uwanja wa ndege wa KIA ambao hawakuona Twiga wetu wakikunjwa shingo kama karatasi na kusokomezwa kwenye ndege ya waarabu, nataka kuwauliza ili niwaamini, Twiga akikunjwa shingo yake huwa anafananaje?! Nataka kuwauliza kama Twiga wale walipiga kelele walivyo kunjwa na kusomezwa kwenye ndege au walifurahia na kukaa kimya.

Kesho nataka kuwaamini Polisi ambao gari yao ilikamatwa ikiwa inasafirisha bangi na wao wenyewe wakaikamata, kesho nataka kuwa amini Polisi walio mchukua mtu akiwa mzima na kumrejesha akiwa mfu, ni kesho tu, nataka kujua kuhusu wale polisi wa Morogoro walio mbambikiza mfanyabiashara wa watu kichwa cha binadamu aliye uwawa wanako kujua wao kwa malengo yao, nataka kuwauliza lengo lao lilikuwa nini, wakati nawauliza nitawatahadhirisha maelezo yao yasije yaka jichanganya na tukio la kitu kizito chenye ncha kali kilicho toa uhai wa Ally Zona kwenye maandamano ya kile chama kilicho kataa kukabidhi ushahidi kwa polisi kwa madai eti polisi ni wahusika wa mlipuko wa bomu kule Arusha, Polisi ndio wenye mabomu iweje iwe wahusika?!.

Kesho nataka kuwaamini Polisi wale ambao waliiba mishahara yao na pesa za wafanya biashara walio kwapuliwa pesa zao na majambazi pale kariakoo, ni kesho tu, nataka kuwaamini polisi ambao hawana historia ya kubambikizia mtu kesi wala kumsingizia raia mwema asiye na hatia maana wengi walioko jela wana hatia zisizo fungamana na mikono ya polisi wala ushawishi wa polisi.

Kesho asubuhi na mapema nataka kuwaamini polisi baada ya kusoma taarifa ya uchunguzi wao makini ulio mtia hatiani Joseph Mulundi yule raia wa Kenya aliye mteka, kumtesa na kumng'oa kucha na meno Daktari Stive Ulimboka halafu akaenda kutubu kule kwa mchungaji Gwajima, kesho ndio kesho maana hata ya Daudi Mwangosi yatakuwa hadharani, nina imani na Kamuhanda maana kazi nzuri ndio imemfanya amepandishwa cheo, si kingine naamni tukio la kulipua bomu bahati mbaya kwa kusaidia kuokoa maisha ya Mwangosi ndio kumempandisha cheo na kupewa hongera na pongezi nyingi na waziri JK.

Kesho ndio siku ambayo huenda sitaamini kuwa polisi wanalipua mabomu japo wamekiri kuwa kulipuka kwa mabomu ni jambo la kawaida, na wao ndio wenye mabomu, yakilipuka ujue ni wao sema tu kwa bahati mbaya! Nataka kuamini kuwa hawahusiki na kulipuka kwa bahati mbaya au makusudi kwa bomu la pale Soweto Arusha kama jinsi ilivyo kuwa bahati mbaya kwa Mwangosi na juzi pale Ubungoo kwenye mkutano wa Mnyika. Nani ataniongoza nataka kuwaamini Polisi kuwa hawahusiki na mabomu?!

Nataka kuwaamini Polisi, sitaki kuamini ile ripoti niliyo isoma kwenye gazeti la "The east african" la tarehe 8 Aprili 2013; ambalo eti ripoti yake inaonyesha kuwa jeshi la Polisi linaongoza kwa uonevu, kutunga kesi za uongo, kubambikiza kesi na makosa makubwa ya uwongo ambayo kisheria hayana dhamana, makosa ya mauwaji, makosa ya kutumia nguvu, na makosa ya ugaidi. Etii kwa mujibu wa ripoti hiyo, jeshi la Polisi linahitaji kusafishwa maana limekuwa ni jeshi la kihalifu. Mimi haya yote sitayaamini na siyaamini. Ninacho hitaji ni muongozo usio kuwa na shaka juu ya jeshi letu la Polisi japo Lwekatare amefutiwa kesi yake ya ugaidi.

Nataka kuamini kuwa FBI wapo Arusha kuchunguza tukio la bomu kama tulivyo tangaziwa na afande wetu wa mkoa kuwa FBI na wataalamu kutoka china wako kazini kule Arusha, sitaamini ile taaarifa ya ubalozi wa Marekani nchini kukana eti kuwa FBI hawapo Arusha, taarifa ya ubalozi wa Marekani niya kichochezi na haina ukweli, kwa kuwa nataka kuwaamini polisi nitaamini taarifa ya polisi wetu sio ile ya wamarekani ambao hata ujio wa raisi wao hawakuamini ulinzi wetu eti wamepekua mpaka viongozi wetu wakuu wa polisi! Wale jamaa hawafai na hapaswi kuaminiwa! Kwa lugha ya mipasho kutoka magogoni modern taarabu wale jamaa ni "vizabi zabina wanao tapatapa"

Nataka kuwaamini Polisi wanao singiziwa kuwa eti wanawaogopa wana siasa wa chama tawala wenye ushahidi wa matukio makubwa ambao wanaweza kuutoa hata mbele za Mungu lakini eti polisi wetu wanakuwa na busara hadi pale Mungu atakapo waita ili wakatooe ushahidi wao huko. Chama tawala hawana shida na polisi ila nataka tu kuamini maneno ya Jk kwa chama tawala "... Na nyinyi muache kuwategemea polisi.." Nataka kuwauliza kama ni kweli Polisi huwa wanawabeba ccm hadi kuitwa PoliCCM au JK aliteleza tu ulimi?! Polisi wana aminika bwana, iweje?!

Kesho ndio kesho, nataka kusikia ili niwaamini polisi. Nataka kusikia kama wanatumia nguvu zilezile za kwenda usiku kwenye nyumba ya Mbowe au Lema kama wamewahi kufanya hivyohivyo kwa walio kwapua hela za Kagoda, Epa, Meremeta, Deepgreen na Kawira?! Nataka kujua pia kama wamesha wahi kuvamia magogoni usiku wa manane kumshurutisha Msafiri ataje majina ya wauza unga ambayo anayo chini ya godoro lake sema anaamua kufanya nayo safari kila kukicha!

Kesho itakuwa historia polisi watakapo kana na kuniambia ukweli kuwa wote wanao ingia depo kule ccp ni wenye sifa na huwa hakuna rushwa bali wanasingiziwa. Majibu yao lazima niyaamini maana nataka kuwaamini.

Naisubilia kesho kwa hamu. Nipe muongozo nisubirieje?! Nilindwe na green guard au red brigade?

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums.
 
Mkuu hata ukiwapa Desa la miaka kumi hawezi kuja na majibu.

Labda siku tutakapo badilisha wapangaji wetu pale Magogoni hapo 2015
 
Polisi na Usalama wa Taifa wanaongoza kwa maovu hapa nchini tofauti/kinyume na kazi zao.
Naomba hiyo kesho tuwe wote
Meno ya Tembo- Polisi
Madawa ya Kulevya- Polisi
Bangi- Polisi
Kupiga mabomu ya kivita- Polisi
Na hii ni kwa uchache tu maana Muda usingalinitosha.
Kutesa na Kujeruhi waandishi wa Habari- Polisi
Kubambikiza kesi za Ugaidi- Polisi
 
Kesho haitofika na kamwe hawatoaminika hadi tutakapowakumbusha majukumu ya kuwaajiri.
 
Juzi wamenisimamisha polisi vituo vitatu tofauti wakidai wamepewa taarifa kuwa gari yangu imebeba pembe za ndovu,utazani katibu anayehusishwa na ujangiri hawamjui!!


Baada ya kunikagua na kukosa hiyo mapishi yao wakaanza kuniomba hela kwa namna ya kipuuzi puuzi na kipinda!!!!
 
mkuu Mohamedi Mtoi naomba uwaamini na waliotimuliwa na maiti pale mwananyamala hosp jana baada ya kumchukua kijana wa watu kwao akiwa mzima.
uwaamini pia na wale polisi waliotaka kumkamatisha mfanyabiashara morogoro fuvu la kichwa cha binadamu.
POLISI CCM I HATE YOU!!
 
Last edited by a moderator:
Yaani nataka pia uwaulize, hivi buku mbili, tatu, tano na kumi ndo imegeuka salamu yao siku hizi? Waulize wakishaipokea wanabaki nayo ama wanawafikisha walikotumwa! Kesho waambie tumechika na salamu zao, tutaanza kuwagonga kama alivyofanywa mmoja pale fire sijui.
 
Polisi na Usalama wa Taifa wanaongoza kwa maovu hapa nchini tofauti/kinyume na kazi zao.
Naomba hiyo kesho tuwe wote
Meno ya Tembo- Polisi
Madawa ya Kulevya- Polisi
Bangi- Polisi
Kupiga mabomu ya kivita- Polisi
Na hii ni kwa uchache tu maana Muda usingalinitosha.
Kutesa na Kujeruhi waandishi wa Habari- Polisi
Kubambikiza kesi za Ugaidi- Polisi

Bahati mbaya zaidi kesho huwa haifiki. Ukienda kesho watakuambia ulisema kesho, na kesho vile vile. Count me there Mohamedi Mtoi, ila nambie tarehe, say tarehe 26 Julai 2013 ndipo tutawalazimisha watuambie.
 
Last edited by a moderator:
Kwa polisi ambao wameshabinafsisha akili akili zao siku nyingi ili waweze kupokea na kutekeleza amri na maagizo ya watawala, kwao itakuwa ngumu sana kutoa maelezo sahihi
 
Nimeipenda fasihi iliyotumika kufikisha ujumbe and it's been delivered clearly.
 
mkuu Mohamedi Mtoi naomba uwaamini na waliotimuliwa na maiti pale mwananyamala hosp jana baada ya kumchukua kijana wa watu kwao akiwa mzima.
uwaamini pia na wale polisi waliotaka kumkamatisha mfanyabiashara morogoro fuvu la kichwa cha binadamu.
POLISI CCM I HATE YOU!!
[MENTION][JFMP3][/JFMP3][/MENTION]

Hili la polisi kuchukua mtu akiwa mzima nakumrudisha akiwa mfu bila maelezo hii nihatari na tukiendelea kuwa kimaya tutakwisha this is serious!
 
Naona umechoka kuishi au unataka kuweka kucha zako rehani. Usishangae ukasingiziwa fuvu la kichwa. Shauri yako. We nenda.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Ukiwa chadema ni sawa na kuwa msomi mwenye phd tofauti na ccm ambayo ukiwa huko hata kama una phd unakuwa na akili kama za drs la 4.
 
Back
Top Bottom