Kesho naenda kukutana na Waziri,Kuna ulazima wa Kumuita Mheshimiwa napoongea naye?

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,651
14,318
Kuna watu nlishakataa kuwaita waheshimiwa maana sioni wanachofanya hasa cha kustahili heshima yangu. Kesho nina appointment ya kuongea na waziri flan. Lakini huyu ni mmoja ya watu wa hovyo kabisa katika Tanzania hii. Namfahamu vizuri na ulimi wangu unakataa kabisa mimi kumuita mheshimiwa.

Sioni sababu ya kumuita mheshimiwa na naona ni kama kuwadhalilisha wanaopaswa kuheshimiwa. nauliza kwa wadau JE NI LAZIMA KUMUITA HUYU BWANA WAZIRI MHESHIMIWA? MI NINGEPENDA KUMUITA NDUGU WAZIRI XXXX . Nadhani utangulizi wa ndugu ni mzuri maana ndugu yako ni ndugu tu hata kama ni kichaa /mwendawazimu ni ndugu tu.

Naomba mnisaidie katika hili tafadhali.
 
unachosema ni kweli, kuna wabunge na mawaziri bogus kabisa. ni aibu hata kumuita mtu wa na namna hiyo kuwa ni mheshimiwa ni bora tu kumuita bwana flan au bibi flan kuliko mheshimiwa maana ni makange kabisa. mi mtu kama nape na pia kuna rais mmoja aliyemaliza muda wake aliuwa ni wa naman hiyo sikuwah kumuita mheshimiwa maana uozo wake ulikuwa mwingi sana kiasi kwamba hata ningemuita mheshimiwa angeona kama ninamsanifu tu.
 
Wanavyopenda kuheshimiwa nakushauri kama unataka tatizo lako lipatiwe ufumbuzi muite tu mheshimiwa hata kama ikibidi kumuita mtukufu waziri ili ufanikiwe malengo yako maana hakuna namna nyingine, wanapenda kusifiwa sana
 
ha ha ha...kuna watu ni ngumu kuwaita mh kwa matendo yao ya hovyo unashindwa na unaona utapata dhambi bure tu kuwaita mheshimiwa. maana kuna dhambi ya kusema unafiki au uongo. ni bora ukwpe dhambi nyingine ambazo si za msingi. kuna watu hata ukiniwekea Bomb kichwan ukanambia niwaite mheshimiwa nitakataa kata kata... ni bora tu ulilipue hilo bomb kuliko mimi kuwatukanisha watu kwa kuwaita hawa watu wa hovyo waheshimiwa.
kisheria inasemaje lakini? ni lazima kuwa adress kwa hilo neno mh? kama yule mwingine anayetaka aitwe Dr wakati hata degree yake ilikuwa bora degree? mi siwezi maana sasa hapo ni kuwadhalilisha watu wenye phd.


Eti mj january dogo mpiga dili tuu unamwita mhh bora niseme Mh mange kimambi
 
Mkuu kwa kuwa siyo appointment rasmi (siyo ya kiofisi),hakuna haja ya kumuita Mheshimiwa. Muite tu jina lake ama mlivyozoena. Tena kama ni Nape muite kabisa lile jina lake,NNAUYE. Duuh jina sijui la wapi hili.
 
Wengi wa wanaopenda kutanguliziwa hilo neno Mh, have got nothing to deliver, perfomance yao kwenye majukumu ni negligible ila wanataka kuitwa hivyo kwa lengo la kukufanya uwe na kamoga fulani hivi na kwao ni kama defensive mechanism tu, na wengine wanafichamia kwenye hiyo title lakini mambo yao ni ya hovyo, sijui dhamira zao huwa haziwasuti!!
 
Back
Top Bottom