Ichwampaka
Senior Member
- Nov 19, 2018
- 134
- 109
Wanaharakati,
Kuna inshu moja inanikera sana katika serikali ya awamu hii mpaka nataka nihamie vyama vya upinzani. Kila unapopita ni ujenzi wa miundombinu unaendelea hadi imekuwa kero. Leo najipitia njia ya makaburini Sinza mara pap imefungwa ujenzi unaendelea, nikazunguka njia ya Bagamoyo Mwenge, hovyo kabisa, ujenzi unaendelea, nikatoboa kimtindo njia ya Kijitonyama kule ujenzi unaendelea hivi ni haki kweli? kila mahali kunaboreshwa tu, wala wananchi hatujaombwa hata kuchangia.
Nikatokea njia ya Mtogole duu hawana hata aibu barabara haina hata mashimo ni lami tu unateleza, hivi ni sawa kweli? Kule ubungo kuna dudu moja la ajabu linajengwa sijawahi kuliona; hivyo haya sio matumizi mabaya ya fedha zetu kweli? Kwanza hizi hela mnapata wapi? Corporate tax ni ile ile tena sehemu nyingine mmepunguza hadi 25%, VAT ni ile ile, national budget support si nasikia kama haipo kabisa? mbona Rais haendi nje ''kutembeza bakuli'' mnapata pesa wapi watu nyie?
Nasikia hata huko porini nako hawalali ni kazi kwenda mbele, ndugu yangu yupo Sanga Sanga huko anasema hawalali eti ''Standi Geji''inajengwa, jamani tuoneeni huruma. Sasa funga kazi ni huko ''Stella Joji'' nasikia maji yanakusanywa ili kuzalisha umeme nasikia umeme utakuwa wa kumwaga hata sigara tutakuwa tunawashia umeme, taa, vibatari, majenerata yatapelekwa makumbusho.
Halafu hayo madege mabomba my dear hayo, na sijui mabasi ya angani (ea basi) ukiangalia angani kila dakika 20 yanapita, nyie serikali vibaya hivyo wenzenu hata jua hatulioni vizuri sababu ya anga kujaa hayo mabomba my dear na ea basi.
Serikali tunaomba mtuondelee hizi kero, nawakilisha