Kero za mama mwenye nyumba

sanjally1

Member
Joined
May 9, 2015
Posts
70
Reaction score
66
Salaam wana jf,jaman naombeni mnisaidie ushauri jinsi gani naweza kuitatua kero hii ya swala la umeme kati ya sisi wapangaji na mwenye nyumba wetu,huduma ya umeme imepotea ghafla mwezi uliopita trh 16,tukiuliza kila mpangaji anapewa taarifa tofauti juu ya kinachoendelea,mie nimeambiwa tanesco walikata umeme kwa sabab mwenye nyumba aliugawa ktk nyumba za jiran kinyume cha sheria,mwengine kaambiwa button za luku hazifanyi kazi hivyo mpaka mafundi wa tanesco waje kurekebisha ndo tutaendelea kupata huduma ya umeme,kihistoria hapo mtaan majirani wametueleeza kwamba huyu mama mwenye nyumba ni kawaida yake kuwafanyia visa wapangaji ili wahame mapema kabla ya muda wao kuisha ili apate wapangaji wapya wamlipe pesa aendelee ku make living,tupo wapangaji wawili na wote ni wanafunzi wa vyuo,suala la kutokuwepo kwa umeme linatuathiri sana kitaaluma ukiangalia pia mitihani ya mwisho inaanza wiki ijayo,tufanye nini ili turudishiwe huduma ya umeme kwa sabab swala la kukatiwa umeme na tanesco ni la uongo,huyu mama hajanunua tu umeme na anataka tuchange laki 2 kama faini ya tanesco ili turudishiwe umeme la sivyo tutabak bila umeme mpaka mikataba iishe tuhame kwake,yeye anadai hana pesa na bado hajajipanga kulitatua hilo swala
 
kuna mama huwa wanajifanya wahuni sana. nenda serikali ya mtaa unaweza saidiwa. poleni sana
 
Refer makubalian katika mkataba wenu, zungumzeni nae, ikishindikana nenda serikali za mtaaaa. Usiongee mae kiuoga, zungumza nae kama mtu mzima mwenzie, kinyume na hapo, ata take advantage ya udogo wenu na nidhamu yenu hiyo kuwa peleka.

Akishindwa rudisha umemex awape kodi yenu, mkaende kwingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…