Kero ya Rais kutumia barabara

Hapunguzi gharama hata kidogo ndiyo kwanza gharama imezidi mara 100 kwa mafuta ya zile gari zote ni kubwa kuluko kusafiri kwa ndege.

Kokotoa hesabu hapa ili tupate gharama za uliganifu, usidhani watu wote humu ni mifugo na nyumbu kama wewe na wenzako.
 

Ndugu wewe hujui tu wenzako tunavyoteseka hapa. Wenzio tunaenda mbali na tumesimama saa nzima na bado tu hajapita afu wewe unasema tuunge mkono upuuzi huu!
 
Kwa hili nadhani Rais wangu afikirie upya. Tena namshauri atumie hata helkopta kutoka ikulu kwenda airport kuondoa usumbufu wa foleni za kumsubiri yeye apite
 
hii ni zaidi ya kero,ila safi inanipa hasira zaidi juu ya MASOLEX
 
Kwa ninavyomuhisi Dr Magufuli ni mtu wa calculations. Atakuwa keshalifanyia hesabu hili la usafiri wa barabarani na keshaona madhara yake in practice. Sifikirii kama atarudia tena kwenda Dodoma kwa msafara wa magari kama vile.

Costwise, ni gharama zaidi kwa yeye kutumia barabara. Ukitiilia maanani idadi ya magari pamoja na (security) personnel na maofisa wa serikali, gharama za doria pamoja na traffic police. Na kubwa zaidi ni muda atakaotumia akiwa njiani na atakaoutumia kwa mapumziko atakapofika kwa vile atakuwa amechoka.mno pamoja na jopo lake lote. Kwa kifupi siku nzima inakatika bila ya uzalishaji, na ukitilia maanani mishahara yao mikubwa, utagunduwa ni mamilioni yanakatika kwa siku hiyo moja bila ya uzalishaji.

Tumpongeze kwa kujaribu. Ingekuwa bora zaidi kama serikali ingekuwa na luxury coach litakalochukuwa watu kama 30-40. It's much more comfortable and cost effective
 
We unapoteza mda kuwahi ye anapunguza matumizi ya serikali,two diffrent brains with different goals
 
Loh! Tanzania nchi yanguuuu,,,,wananchi wake hata uwafanyie nn wanalalamika!!
 
Mleta mada muongo na mpuuzi mimi ni askari mtu hawezi simamishwa wakati msafala upo gairo jamaa muongo halafu mpuuzi.

Safi sana mkuu mfahamishe naona kuna watu Kasi hii inawakera maana walizoea kuramba dume sasa mirija inakatwa.
Tena ipo haja ya viongozi wote sasa kutumia barabara kupunguza matumizi huu ni mfano mzuri sana. HAPA KAZI TU mwenye chuki ahame nchi.
 
We unapoteza mda kuwahi ye anapunguza matumizi ya serikali,two diffrent brains with different goals

afu cha kushangaza utakuta jitu linasema eti limepotezewa muda na magufuli,na wkt hata hakuna mahali lilipokua linawahi zaidi ya kuwah wanywa viroba wenzake wakalewe.
 

Acha uongo...magufuli anawateseni ukawa
 
Mimi nililalamika siku magufuli anatumia barabara kwenda dodoma tulikalishwa masaa matatu barabaran,tukisubir msafara wa magufuli huku wengine wakiwahi interview,appointment na doctor,mitihani,matibabu n.rais aangalie njia nyingine ya usafir,kwa bongo barabara bado sana.
 
Mleta mada muongo na mpuuzi mimi ni askari mtu hawezi simamishwa wakati msafala upo gairo jamaa muongo halafu mpuuzi.

Wewe kuwa askari haimaanishi ndiyo kujua lililotokea Chalinze(ambapo mleta mada ndipo amesema), kwani askari kitu gani? Na bado inaweza kuwa ni askari magereza, sasa vinaingiliana hapa(au kwasababu unadhani naye ni askari wa usalama barabarani)?

Kitu kinachozungumzwa kipo sana, hata hapa sijui nani yuko Masaki na anaenda huko na anaenda Msongola hapo kati mmeshawekwa pembeni kama viazi wakati yeye ndiyo kwanzaaaaaa anafanya mambo yake!
 
Sasa ikitokea tunaelekea huko kwa wakoloni kwenda kujitambulisha/mkutanoni 'ITAKUWAJE' au tutaanza safari mwezi kabla ya tukio huku tukitumia gari na meli?.
Sinasikia jamaa kakatazwa kupanda ndege na madaktali.
 

Ana afya yule ya kukaa kwenye gari,sio yule uozo anaejinyea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…