Pole sana mkuu, ila faini ilitakiwa 50,000 tu. Mimi yalinikuta majuzi tuu nilikuwa natoka JKT Jitegemee pale getini naelekea mbagala, kuna mdada akaja kwenye gari langu anaburuza mguu anachechemea, akawa anaomba msaada. Akaniambia ameteguka mguu anahitaji msaada walau mpaka stendi ya daladala. Katika kumwuliza anakokwenda akasema anaenda kwa Azizi Ali, basi nikampa lifti kwa sababu tunaenda njia moja. Tulipofika kwa azizi ali, nikapaki gari kwenye parking ya daladala ili ashuke, ndani ya dakika moja, mdada wa watu anajaribu kushuka taratibu kwa sababu ya kuumwa mguu, jamaa wakapaki noah yao kuniblock. walinisumbua sana mpaka tukapelekana kwenye gereji yao kule keko, nikaishia kulipa 50,000.
Ila nimewanotice vizuri na mmoja wao nimegundua ananifahamu tunatoka sehemu moja, najua siku tukikutana kwenye anga zangu lazima nitalipiza.