Kero ya Mabasi ya Mikoani kuchochea udini

Magari ya kwenda mikoa kama Tanga, Mtwara, Kilwa nayo hupiga sana kaswida lakini mbona wasio waislam hawalalamiki 🥲
 
Kama nyimbo za Injili zinakukera,utakuwa na matatizo.
Waislamu wengi tu wanazipenda nyimbo za Injili.
Na hata baadhi ya Qaswida zinapendwa na Wakristo kulingana na maudhui yake.
Na ni umakini gani unaoupoteza,kwani we ni dereva?
 
Hata wamiliki wengi wa mabasi hayo wa imani Fulani, lakini hatuna nongwa tunasafiri tuu.
 
Huko Bara, wakristo wengi,
Ni kawaida, jaribu kupsnda boti za kwenda zenj, utajua ninachokwambia
 
Hivyo sio vyombo vya serikali mbona hulalamiki baadhi ya mabasi ya mwendokasi kuweka kaswida na mawaidha? Nenda Zanzibar kila gar ya abiria utakayopanda imeweka kaswida ama mawaidha na watu hatulalamiki tunaona fresh tu.

Ukiona unakereka tafuta earphone utundike masikioni utakuwa ume solve tatizo.
 
Sisi waabudu mizimu tunataka kipaumbele pia
 
Kwa hiyo unataka wakuwekee bongo fleva? At least ungelalamika kelele tu ingemake sense
 
Hivi mnatakaje? Bus mmiliki ni muislam, nje imeandikwa Kun fuya Kun, Ndani zinapigwa injili, lawama kwa nani?
 
Uliwaambia wapige vigodoro wakakataa? Hata hivyo hizo nyimbo humtaja Mungu zaidi, au haumpendi Mungu.
 
Sijui huwa mnapanda bus gani maana ninayopanda mie wanapiga kwaya na kaswida,nyimbo za kiislam za kutosha
 
Huwezi kuchagua nyimbo za kwenye basi kama basi sio VIP. Pale zinapigwa kwa chagua la dereva. Ubaguzi tunautengeneza vichwani mwetu. Maana hata zikipigwa bongo fleva mtu mwingine anaweza sema ni kelele, yeye anapenda reggae za jamaica au muziki wa afrika kusini. Tuvumiliane
 
Ukipata jibu la kwa nini Yesu anaeabudiwa na wengi ni yule jamaa alieigiza picha ya Yesu njoo tujadili kuhusu dini, kabla ya hapo tambua tu Dini ni Biashara za watu walianzisha kwa maslahi yao na walifanikiwa kwa 100%. Zamani mtu akiwa mjanja ni mjanja kweli na alikuwa anaogopwa kukerwa. Ndio maana ukiend akijijini kukawa na Tajiri mmoja utakuta anasikilizwa sana na ushauri wake unaonekan awa maana. Ndivyo ilivyokuwa hata zamani waliojanjaruka mapema ndio walifuatwa wanasema nini.
 
Mabasi ya kwenda Tanga mengi yanapiga nyimbo za kiarabu

Hii umesababisha watu wasio waumini wa kiarabu wamekuwa wakizikwepa hizo basi

Iko hivi maudhui ya kiislam hayasikiliziki kwasababu siku zote yanahimiza chuki

Mkuu sasa nyimbo za kiarabu ndio za kiislamu kwani? Wagalatia bana munavituko sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…