Kero: watu kukaa dukani wakati hawanunui bidhaa

Little Dreamer

Senior Member
Joined
Sep 12, 2017
Posts
184
Reaction score
166
Habari wajumbe!

Leo nimeona niongelee hili suala la tabia ya watu kujijaza dukani hasa wakati wa usiku na hawanunui kitu inavyokwamisha biashara.

Mimi kama mteja nimeshawai ahirisha kwenda kununua bidhaa kwenye baadhi ya maduka coz unakuta watu wamekaa tu na wameziba nafasi ya wateja ambao wanataka kununua bidhaa na utakuta mteja anahitaji huduma ya haraka lakini akipiga mahesabu hata nafasi ya kupata huduma itakuwa ngumu kwa sababu muuzaji anakuwa yupo bize na kuongea na watu ambao sio wateja.

Mimi naamini kuna wateja wengi wafanyabiashara wanawapoteza kwa sababu ya kuendekeza watu wasio na kazi na wanakuja dukani kama sehemu ya kupumzikia, ushauri wangu kwa wauza maduka wasichanganye biashara na urafiki, kwa hali hii ilivo ngumu, mkiendeleza kuyafanya maduka kama hotel mtamtafuta mchawi ila kikulacho ki nguoni mwako
 
Unashindwa hata kununua condom kisa dukani hakuna privacy.
Hili ni tatizo kubwa mno mno Bongo na lina madhara mengi.
1. Kuna kushindwa kununua vitu vya ''private'' kama ulivyosema condom na vingine kama towel za kina mama, kukopa nk.
2. Kina mama wamekuwa wahanga wakubwa wa hili tatizo na wasichana wadogo wanapata wakati mgumu wa kusumbuliwana hao wakaaji wa dukani.
3. Watu wanakuwa hawako free kufanya manunuzi yao na mara wanapoondoka wakaaji dukani wanaanza kuwajadili kwa mazuri au mabaya.
4. Badhi ya wakaa dukani wanatumia hizo fursa kuomba kwa wateja na kuchunguza financial powers za wateja.
 
Mawakala co watu kabisa
 
Habari wajumbe!

Leo nimeona niongelee hili suala la tabia ya watu kujijaza dukani hasa wakati wa usiku na hawanunui kitu inavyokwamisha biashara.

Mimi kama mteja nimeshawai ahirisha kwenda kununua bidhaa kwenye baadhi ya maduka coz unakuta watu wamekaa tu na wameziba nafasi ya wateja ambao wanataka kununua bidhaa na utakuta mteja anahitaji huduma ya haraka lakini akipiga mahesabu hata nafasi ya kupata huduma itakuwa ngumu kwa sababu muuzaji anakuwa yupo bize na kuongea na watu ambao sio wateja.

Mimi naamini kuna wateja wengi wafanyabiashara wanawapoteza kwa sababu ya kuendekeza watu wasio na kazi na wanakuja dukani kama sehemu ya kupumzikia, ushauri wangu kwa wauza maduka wasichanganye biashara na urafiki, kwa hali hii ilivo ngumu, mkiendeleza kuyafanya maduka kama hotel mtamtafuta mchawi ila kikulacho ki nguoni mwako
Haswa inakera jamani,mikitu mwingine Ina enda jirundika hata kwenye maduka ya madawa,mtu una shida binafsi unashindwa kwenda tatuliwa
 
Unashindwa hata kununua condom kisa dukani hakuna privacy.
Hii ishanikuta Sana aisee, noma Sana , hasa wale wenye TV dukan na wanaweka channel za mpira , hii ina-attract Sana wateja hewa kujazana dukan .... Mteja ukienda wanakukodolea mimacho kama yotee daaah
 
Mojawapo za tabia za hovyo sana katika maduka madogo ni hii.
 
Sehemu za biashara watu wamefanya kama kijiwe cha kahawa nani ataingia hapo anunue kondom ni nk
 
Watu na mambo yao hawakai hivihivi
Labda anachora mauzo yanavyoenda dukan
Wengine ndio wazee wachuma ulete unauza sana lakin ufungapo mahesabu jion huoni pesa
Duka likishaanza kufilisika huwaoni wakijazana kukaa dukan
 
Nilipata shida sana kununua pedi enzi hizo ila siku hizi supermarkets nyingi japo kuna dharura unafika uso kauzu unanunua hivyo hivyo
 
Back
Top Bottom