Kero wanazokutana nazo wafanyabiashara wapangaji kwenye fremu za Magereza Iringa

Captain 666

JF-Expert Member
Nov 5, 2021
654
1,208
Habari wana jamvi.

Jeshi la Magereza mkoa wa Iringa lina mradi wake wa fremu za maduka yaliyopo mkabala na hospitali ya mkoa kuzunguka apartment zao hao Magereza.

Kero kubwa iliyopo ni kitendo cha RPO Iringa kusumbua wapangaji wa maduka hayo hata usiku wa manane kudai kodi kama vile hakuwezi kukucha.

Hili jambo limekua kero na litakuja kuharibu ndoa za wapangaji wa jinsia ya kike.

Hivi kwanini asiache mkuu wa idara akashughurika na mradi yeye akawa anapokea tu taarifa?

Maana sasa imekua kero wapangaji hatuna raha vitisho kila dakika utadhani sisi ni wahalifu.

Atambue kua sisi ni raia na hatulazimiki kutii kila amri yake pasipo kuhoji na atambue kua unapoamua kufanya biashara na raia basi uwe kama raia.

Tunakuomba mkuu wa magereza Tanzania uliangalie hili kwa jicho la kipekee.

Ni sisi wafanya biashara wapangaji wa fremu zenu za maduka hapa Iringa.
 
aisee napendaga kuja kununua nyanya jion hapo kwenye kaukuta ka hospital ya mkoa.nikichoka kwenda mashine tatu
 
Na nyinyi muache usumbufu! Lipeni hiyo kodi yao ya pango kwa wakati ili kuepuka kupigiwa simu usiku. Maana mkipigiwa mchana, hampokei!
 
Habari wana jamvi.

Jeshi la magereza mkoa wa Iringa lina mradi wake wa fremu za maduka yaliyopo mkabala na hospitali ya mkoa kuzunguka apartment zao hao Magereza.

Kero kubwa iliyopo ni kitendo cha RPO Iringa kusumbua wapangaji wa maduka hayo hata usiku wa manane kudai kodi kama vile hakuwezi kukucha.

Hili jambo limekua kero na litakuja kuharibu ndoa za wapangaji wa jinsia ya kike.

Hivi kwanini asiache mkuu wa idara akashughurika na mradi yeye akawa anapokea tu taarifa?

Maana sasa imekua kero wapangaji hatuna raha vitisho kila dakika utadhani sisi ni wahalifu.

Atambue kua sisi ni raia na hatulazimiki kutii kila amri yake pasipo kuhoji na atambue kua unapoamua kufanya biashara na raia basi uwe kama raia.

Tunakuomba mkuu wa magereza Tanzania uliangalie hili kwa jicho la kipekee.

Ni sisi wafanya biashara wapangaji wa fremu zenu za maduka hapa Iringa.
Hapo kero sio huyo RPO ila ni wewe unayedaiwa kodi. Lipa kodi yao halafu uje utuambie kuwa RPO bado anaendelea kukupigia simu usiku, hapo ndio tutakua upande wako
 
Hatukatai kudaiwa . kwa cheo chake atulie ofisini ahangaike na mambo makubwa . hicho kitengo awaachie wasaidizi wake
 
Lipa kodi usimpangia ukusanyaji. Yeye pia amejiwekea malengo. Dawa ya deni ni kulipa
Halafu wewe ndie RPO mwenyewe kumbe.

Gawa majukumu punguza njaa mkuu. Mbona hatuoni commisioner wako akiingilia kazi zako
 
Back
Top Bottom