Mimi kama mdau wa elimu, najitokeza kupaza sauti yangu juu ya ongezeko la mitihani isiyo na mpangilio mzuri kutoka Ofisi ya Elimu ya Sekondari – Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Simiyu. Hali hii imekuwa kikwazo kikubwa kwa ufundishaji na ujifunzaji wa watoto wetu, hasa katika shule zenye miundombinu duni na idadi kubwa ya wanafunzi.
⚠️ Changamoto Zinazojitokeza:-
1. Mitihani Mingi Isiyo na Mpangilio wa Kitaaluma
Mitihani imekuwa ikitolewa mara kwa mara bila kuzingatia muktadha wa mtaala wa elimu. Na malengo ya mitaala,maafisa wanaamini katika mitihani bila kujali uelewa wa mtoto Kwa kile anachofundishwa na walimu wake.
Afisa elimu na wasaidizi wake wamejikita zaidi katika mitihani badala ya kuhakikisha mtoto anaelewa kwa kina kile anachofundishwa kwani mitihani hii imekuwa chanzo Cha mapato kwao Kwa kuwalazimisha wakuu wa shule kuchangia fedha za uendeshaji wa mitihani hii.
2. Athari kwa Miundombinu na Ratiba za Masomo
Shule zenye wanafunzi 200–300 hulazimika kutumia madarasa 5–8 kwa mitihani, hali inayosababisha madarasa ya chini(yadiyo na mitihani )kukosa vipindi kwa wiki 1–3 ambapo pia Walimu 5–8 huondolewa kwenye ufundishaji ili kusimamia na kusahihisha mitihani, hivyo watoto hukosa masomo kwa muda mrefu.
3. Mfano Halisi: Mitihani ya Kidato cha Nne – Aprili 2025
Mitihani ilichukua wiki 3, ikifuatiwa na wiki nyingine 1 ya usahihishaji ,Jumla ya wiki 4 za masomo zilipotea kwa wanafunzi wa madarasa yote katika ufanyikaji wa mitihani hii Wakuu wa shule walilazimishwa kuchangia fedha ili kufanikisha mitihani hiyo, jambo linaloibua maswali kuhusu uwajibikaji wa maafisa elimu. Na pengine wakuu wa shule tunashindwa kuhoji Kwa kuogopa kupoteza madaraka.
4. Kuingilia Mitihani ya Ndani ya Shule
Mitihani ya robo, nusu na mwisho wa muhula hutungwa na ofisi ya elimu kwa shule zote wilaya Kwa mwaka mzima ,hali hii huondoa uwezo wa walimu kupima maendeleo ya wanafunzi wao binafsi na kurekebisha mapungufu yao.kwani ukiajiliwa katika halmsahauri hii Kwa Muda wa miaka miwili Sasa,sahau utungaji wa mitihani,wewe utabaki kuwa msahihishaji tu mitihani ,na wakati mwingine mitihani inakuwa nje ya kile ulichofundisha na pengine ofisi ya elimu halmsahauri ya wilaya ya Busega inapuuza tofauti za miundombinu, idadi ya walimu, na changamoto za kipekee za kila shule kwani kitendo hiki kinaathiri pakubwa sana swala la ufundishaji.
5. Kuvunjwa kwa Ratiba ya Likizo
Tarehe 30 Julai 2025, wanafunzi wa kidato cha nne walifanya mitihani ya mock ya Kanda ya Ziwa.Kabla ya matokeo kutoka au usahihishaji kufanyika, tayari mitihani ya pre-national wilaya imetangazwa kuanza tarehe 01 Septemba 2025 – kipindi ambacho ni likizo rasmi. Hii ni kinyume na Waraka wa Elimu wa 2023 unaopiga marufuku uendeshaji wa shule bila kuzingatia kanuni na miongozo ya serikali.
📢 Wito kwa Mamlaka za Elimu na Serikali Kwa ujumla
1. Halmashauri iache kuingilia mitihani ya ndani ya shule
Shule zipewe uhuru wa kutunga mitihani yao kulingana na uwezo wa miundombinu na mahitaji ya wanafunzi wao jambo Hili itapunguza upotevu wa vipindi kwa madarasa ya chini na kuboresha ufundishaji. Na ikiwa Kuna ulazima wa halmsahauri kutunga mitihani ambayo ni uniform Kwa wilaya nzima basi wafanye mwezi wa 12 ambapo tunajua kuwa Kila mwalimu anapaswa kuwa amekamilisha syllabus na hivyo kupima mambo Kwa uhalisia.
2. Mamlaka izuie ulazimishaji wa michango ya fedha kwa mitihani ya ndani
Wakuu wa shule wanalazimishwa kuchangia mitihani ya mwezi wa 3, 6, 9 na 12 bila tija ya kitaaluma.Mamlaka za mkoa na taifa zichukue hatua kudhibiti tabia hii inayolenga kujipatia fedha badala ya kuboresha elimu.
3. Likizo iheshimiwe kama sehemu ya mchakato wa ujifunzaji
Ofisi ya elimu ikumbushwe kuwa likizo ni muhimu kwa mapumziko ya kiakili ya mwanafunzi na kufanya mitihani wakati wa likizo ni kinyume na miongozo ya elimu na kunaua ari ya kujifunza.
🙏 Hitimisho
Ni wajibu wa kila mdau wa elimu kuhakikisha kuwa mtoto anapata mazingira bora ya kujifunza. Utitiri wa mitihani usiozingatia muktadha wa shule, mtaala, na ratiba ya kitaifa ni tishio kwa ubora wa elimu. Natoa wito kwa mamlaka husika kuchukua hatua stahiki kurekebisha hali hii kwa manufaa ya watoto wetu na mustakabali wa taifa.
Ahsante sana.