Hivi karibuni tumesikia kuwa kuna utaratibu wa kuhama mtandao mmoja kwenda mwingine ukitumia Namba ileile, kwa kweli mimi binafsi sijui sababu za msingi za kuhamia mtandao mwingine,
Ninawaomba sana wahusika wa TCRA waelezee umma faida za huo utaratibu na hasara zake. Je endapo nimeridhika na utaratibu wa kumiliki namba tofauti za mitandao tofauti (nikibaki na utaratibu niliozoea) je nitaathirika kwa kiasi gani? Utaratibu huu una lengo gani na una faida gani kwa mtumiaji au serikali?
Namba wakati mwingine huwa zinafanana na hutofautishwa na aina ya mtandao je ikitokea mtu mmoja anatoka mtandao mmoja na kuhamia mwingine ambako kuna mtu anayemiliki namba inayofanana ambayo ilikuwa ikitofautishwa na namba za mwanzo je uhamaji huu hautasababaisha mwingiliano wa mawasiliano?
Mimi binafsi na watu kadhaa niliojaribu kuwauliza wengi hawajui kitu gani kinaendelea. TCRA pamoja na mashirika ya simu hebu tuambieni ni kitu gani hiki?