Kwa kweli TBC pamoja na matatizo hayo lakini wanajitahidi sana, maana taarifa yao ya habari naipenda zaidi kuliko ya vituo vingine. Actually nafikiria kumfikisha TIDO mahakamani kwa kudanganya umma maana wakati anapewa ukuu wa TBC alisema tumpe miaka miwili au mitatu wenyewe tutaipenda TBC. Hivyo mm nilikuwa nasubiri hiyo miaka ipite ndo nianze kuangalia TBC1. Sasa mwaka jana December kwa bahati mbaya nika tune TBC 1 duu ubora ule niliouona sikuamini tangu siku hiyo naangalia taarifa ya habari ya TBC1 na hata vipindi vingine. Nataka nimshtaki TIDO kwa kuninyima huo uhondo maana nimekosa mambo mengi ya TBC1........
Pia kuna watangazaji wawili wa michezo Enock Bwigane na Pendaeli Omari wale vijana ni wazuri sana tena - nawapa hongera vijana kazi yenu ni nzuri
Ushauri: TIDO najua unatembelea hapa, tafadhali zingatia maoni ya wadau mbalimbali- tuko pamoja