KERO: Idara ya maji Moshi mnachotufanyia wakazi wa mji mdogo wa Himo sio vizuri

Mtoto halali na hela

JF-Expert Member
Aug 10, 2012
30,558
2,000
Kama kichwa cha habari kinavyosomeka, natumaini kuna baadhi ya watendaji wa Idara hii wamo humu fikisheni ujumbe huu kwa wahusika.
Tumelalamika kwa muda mrefu sasa tokea September 2018 wakazi wa mji mdogo wa Himo Kilimanjaro juu ya ukatwaji wa huduma ya maji ifikapo saa 1 usiku na kurudishwa saa 7 ama saa nane mchana, na kero hii ni kwa tunaoishi chini ya shule ya sekondari ya himo ndio tunakumbwa na kadhia hii. Tukipiga simu ama kufika ofisini mnadai hakuna mgao wa maji kama ni hivyo mbona mnatufanyia hivi? Maji yanahitajika sana kwa maendeleo ya mwananchi mmoja mmoja na jamii kwa ujumla, wengine pia wanategemea maji haya haya kufanyia ujenzi ina maana fundi atafika site asifanye kazi kisa maji kwenye tenki yamekwisha? Badilikeni maana tumetumia pesa kupata huduma hii pia tunalipa bills kwa wakati, #MUWSA tupeni majibu yanayofaa juu ya hili

Sent using Jamii Forums mobile app
 

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
6,507
2,000
Bado mnategemea maji ya Masaera nasikia yatafungwa kwani huko Pofo mna mradi mwingine.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom