Kero: Dada muuza duka, ''chenji ikibaki nakunywa soda''

msemakweli2

JF-Expert Member
Jul 28, 2013
1,627
1,880
Nashangazwa sana na tabia za dada huyu, hapa nyumbani kwangu jirani kuna duka ambalo anauza binti flani hivi,yaani siko huru kwakuwa nikitoa noti ya elfu kumi tu nikinunua kitu utasikia 'inayobaki nakunywa soda'.

Nimeshamfokea mara kadhaa lakini anaendelea na tabia hiyo mpaka wakati mwingine inanibidi niende duka la mbali ili kuepuka kero hiyo, au wakati mwingine nalazimika kujificha mahali then namuagizia mtu aniletee bidhaa ninayohitaji.

SIJUI NIMFANYAJE IMEKUWA KERO KWANGU KWA SASA
 
nashangazwa sana na tabia za dada huyu, hapa nyumbani kwangu jirani kuna duka ambalo anauza binti flan hivi,yaani siko huru kwakuwa nikitoa noti ya elfu kumi tu nikinunua kitu utasikia inayobaki nakunywa soda,nimeshamfokea mara kadhaa lakini anaendelea na tabia hiyo mpaka wakati mwingine inanibidi niende duka la mbali ili kuepuka kero hiyo,au wakati mwingine nalazimika kujificha mahali then namuagizia mtu aniletee bidhaa ninayohitaji.SIJUI NIMFANYAJE IMEKUWA KERO KWANGU KWA SASA


Hata mie muuza duka hapa jirani anatabia hizo, ukipata majibu naomba unifowadie.
 
Yani umenikumbusha muuza duka wa karibu na home alikuwa kila nikienda ananiambia "dada nimekunywa Baltika moja nilipie basi"...namkaushia kau...siku hizi kaacha...
 
Mzinga wa lazma, utake usitake......
Pole, ila haiwezi ikatokea tu from no where mtu akaanza mazoea ya hivo lazma umechangia kiasi chake.
Cha muhimu lipia kreti kabisa ili awe anakunywa taratibu, chenji zako akupe
 
Mzinga wa lazma, utake usitake......
Pole, ila haiwezi ikatokea tu from no where mtu akaanza mazoea ya hivo lazma umechangia kiasi chake.
Cha muhimu lipia kreti kabisa ili awe anakunywa taratibu, chenji zako akupe

Eti hili ni la kuombea ushauri, dah.

BTW mama mchungaji semina tunaanza lini jamani.
 
Jamaa alikuwa ana complain kuhusu haya haya kwa mwenye mali na mwenye biashara alimuita na kumshushua mbele yangu na kumwambia aache tabia hiyo mara moja kwani anamgukuzia wateja.

Hii tabia wesichana baadhi wanayo kama kwenye salon na kiosk
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom