Kenyan Doctors Go on Strike Over CBA Promise.

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,950
_93264851_kenyastrikingdoctors.jpg

Wahudumu wa matibabu waliogoma kutokana na kukosa nyongeza ya mishahara

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amekutana leo na wataalamu wa kimatibabu, ambao wamekuwa wakigoma kwa zaidi ya mwezi mmoja, ili kutafuta suluhu ya maandamano hayo ambayo yamelemaza shughuli za matibabu nchini humo.

Madaktari na wafanyikazi wengine wa afya, wanasema kuwa mamlaka kuu nchini humo, bado haijatimiza makubaliano yao ya nyongeza ya mishahara na mafao mengine walioafikiana mwaka 2013 walioahidiwa.

Mgomo huo umeathiri pakubwa sekta ya afya nchini Kenya, huku baadhi ya wagonjwa wakifariki kwa sababu ya kutohudumiwa kimatibabu.

Chanzo: BBC Swahili


--------------

UPDATE:
--------------

Madaktari wakataa nyongeza ya mshahara iliyopendekezwa na Serikali:

Doctors have rejected President Uhuru Kenyatta’s pay rise offer and insisted on the implementation of a collective bargaining agreement struck in 2013.

The doctors, through the Kenya Medical Practitioners, Pharmacists and Dentists Union (KMPDU), announced Friday that they will continue with their strike until their demands are met.

Union officials met in Nairobi to deliberate on the President's offer before making the announcement.

President Kenyatta initiated the dialogue that took six hours, with the government offering a monthly salary of Sh196,989 for the least-paid doctor, up from the current Sh140,244.
 
Mwezio akinyolewa we tia maji, huu mgomo upo mbioni pia hapa bongo
 
Tz hawajiamn wanahis wakigoma ndo watakosa hata hcho kdogo, maana baba yao hasikilz maoni ya watu anafanya kjacho kichwan mwake!

Kuna WALIOSITISHIWA AJIRA zao June mpaka leo lakn hakna hata anaedai haki yake wamebaki kuumia na kulalamika kwenye mitandao tu!
 
na ninawashangaa wabongo wenzangu wanaowabishia wakenya kuwa wametupita kila kitu, wakenya wana akili sana na pia wana uchungu na nchi yao, hata kama mtu ataiba hatojisahau kabisa kiasi cha kuita mabilioni ya shilingi eti vijisenti, wakenya watatuacha mbali sana zaidi na zaidi mana utashi mkubwa sana.
 
Tanzania tatizo ni kwamba 98% ya income ya wafanyakazi ilikuwa inatokana na posho hewa, mishahara hewa, wanafunzi hewa, mafao hewa nk na ndio maana ukiitisha mgomo wale wachache wasioiba wanazidiwa nguvu na wengi wenye 'maslahi hewa'. Kama JPM akiweza kumaintain hii kasi nina uhakika mwaka kesho ukiitisha mgomo wote wataweka zana za kazi chini.
 
Ni haki yao kudai maslahi zaidi lakini omba sana kwa Mungu unaemwamini isitokee mgomo huku una ndugu/rafiki mgonjwa!ni jambo la kushangaza serikali uchwara za kiafrika hazionagi umuhimu wa kuongeza marupurupu kwa wafanyakazi wake hadi ifikie hatua watu wagome.si ajabu hata hapa kwetu wanasubiri wagome ndiyo waanze vikao vya kuwaongezea mishahara,kwanini wasijifunze hapo jirani paliposhaunguwa nyumba kabla na kwetu hakujaungua?this is ridiculous
 
Madaktari wa kenya pamoja na mgomo walijipenyeza kinamna kuhudumia wagonjwa.
 
Tanzania wengi ni ndumilakuwili wapo pande zote Mbili, Kwa hiyo mgomo haudumu watu wapo kwenye mgomo wengine wanafanya kazi officen, na kuwapiga vijembe waliogoma kuingia officen wanataka wenzio wafukuzwe. Mgomo hauwezi kudumu.
 
Back
Top Bottom