Kenya yampoteza Dr. Mpango.

fakalava

JF-Expert Member
Jul 16, 2015
4,459
6,027
Kenya yampoteza Dk Mpango

ecdf6086dabe1f5cb7c923da737f3f42.jpg

Dr. Mpango.

By Nuzulack Dausen, Mwananchi ndausen@mwananchi.co.tz


Katibu Mtendaji wa Tato, Sirili Akko alisema kodi hiyo itasababisha sekta ya utalii kuyumba kwa sababu gharama hizo mpya zitahamishiwa kwa watalii, ambao kwa kukwepa gharama zaidi watakimbilia kwa washindani wenye bei nafuu

Dar es Salaam. Wakati Tanzania ikianzisha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika utalii, Kenya, ambayo ni moja ya nchi zilizotajwa kama mfano kuhalalisha hatua hiyo, imefanya kinyume chake; imeondoa kodi kwa watalii wanaotembea hifadhi na mbuga zake ili kuiinua tena sekta hiyo.

Katibu Mtendaji wa Tato, Sirili Akko alisema kodi hiyo itasababisha sekta ya utalii kuyumba kwa sababu gharama hizo mpya zitahamishiwa kwa watalii, ambao kwa kukwepa gharama zaidi watakimbilia kwa washindani wenye bei nafuu.

“Vile vile kwenye huduma na bidhaa kampuni za utalii kama zilivyo nyingine zinalipa VAT na hazipatiwi marejesho. Ningependa tujifunze kutokana na makosa ya jirani zetu wa Kenya kuhusu VAT ambayo ni moja ya sababu kubwa ya biashara ya utalii kuyumba,” alisema.

Mkurugenzi Mwendeshaji wa TTB, Devotha Mdachi alisema anaungana na wadau wa sekta binafsi kuwa utalii utapitia kipindi kigumu baada ya kuanzisha VAT, ikizingatiwa Kenya ambao ni washindani wakuu wameamua kuiondoa na kuongeza bajeti ya matangazo.

Chanzo: Mwananchi online.
Kenya yampoteza Dk Mpango
 
Back
Top Bottom