Kenya: Wazalishaji Maudhui wa Instagram na Facebook kuanza kulipwa na META

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Ni kauli iliyothibitishwa na Rais #WilliamRuto wakati akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa ambapo amesema Serikali yake imefikia makubaliano na Kampuni ya #META kuwalipa wabunifu wa Maudhui

Ruto amesema "Utawala huu umechukua hatua za makusudi kuwekeza katika tasnia ya ubunifu. Nina habari njema kwa wabunifu wetu na wale wanaofikiria kutoa maudhui kupitia #Facebook na #Instagram. Juzi tu, META imeridhia kutenga Pesa kwaajili ya Waandaji maudhui."

Oktoba 2023, META ilithibitisha kuwa inafikiria namna ambayo Wakenya wataanza kulipwa kutokana na uzalishaji Maudhui huku ikianza na wanaochapisha Video kwa jukwaa la 'Reels' kupitia Instagram. Pia, Watumiaji Facebook wenye wachangiaji wengi watakuwa wanufaika

========
 
Back
Top Bottom