Kenya wateta unafiki wa Profesa Kabudi kuipa Kenya kisomo dhidi ya ukabila

simplemind

JF-Expert Member
Apr 10, 2009
16,409
9,183
Kinaya kwa Tanzania kuipa Kenya kisomo dhidi ya ukabila


Majuzi katika kongamano la kitaifa la mchakato wa kuunganisha nchi al maaruf BBI (Building Bridges Initiative) kule Bomas, Nairobi kulizuka mgeni wa nchi jirani aliyehutubu na kuacha maswali mengi kwa wadadisi wa kisiasa.

Bwana huyu ni Waziri wa mambo za nchi za nje wa Tanzania Profesa Palamagamba Kabudi. Sambamba na hulka na sifa za watanzania alitowa hotuba ilosheheni ukwasi wa lugha teule ya Kiswahili na mahanjam mengi ya kiabunuasi. Akibwabwaja kama cherahani ya Mjerumani mfano wa baba yao wa taifa Julius Nyerere bwana huyu mwenye macho makubwa ya kung’ara kama bundi ama paka mwanga alisema mengi ambayo ni ya kutatanisha.

Aidha aliwaomba wakenya waache ukabila na kuungana huku akidai kuwa huo ni ujumbe wa kiongozi wake John Pombe Magufuli ambaye alimtajataja zaidi ya maradufu mfano wa nukuu za kitabu kitakatifu.

‘Hebu simameni na kila mmoja ashike mkono wa mwenzake na kusema hatutaki ukabila’ aliropoka bwana huyu kama aliyepandwa na maruhani ya kikwao na kulazimu waliomo kusimama kama wanajeshi kambini wakiwemo Rais Uhuru,Ruto na Raila. Palamagamba alidai kuwa viongozi hao watatu yaani Uhuru, Ruto na Raila ndio wanaosimamia Kenya.

Je, alimaanisha kuwa bila hawa watatu hakuna nchi? Sidhani. Tukitathmini hotuba ya Palamagamba twaweza kusema kuwa imetoka kwa mtu ambaye hastahili kamwe kusema aliyoyasema. Twasema kuwa Tanzania haina sifa ya kuwapa wakenya mawaidha kuhusu utawala bora ama kuhusu athari za kikabila kwani ina changamoto hizo zinazotokota ndani kwa ndani.

Tukipima Tanzania na Kenya twaona kuwa kuna tofauti kubwa za kihistoria na hususan kmaendeleo iwe kisiasa, kijamii na kiuchumi. Ukweli usiofichika ni kuwa siasa za Kenya ni kali kushinda za Tanzania.

Hii ni kwa sababu wakenya wameelimika zaidi na hivyo kujua haki zao mapema kuliko watanzania. Watanzania wameanza kuamka majuzi kutoka katika maisha ya kale kwani hata elimu yao ni duni. Mwalimu Nyerere atalaumiwa kwa kutozingatia elimu kwa watanzania.

Mwalimu Nyerere alihimiza siasa za kichina za ujamaa na kujitegemea huku akiwadanganya watanzania wakae vijiji vya ujamaa badala ya kujikuza kimataifa. Upande wa Kenya Jomo Kenyata aliboresha elimu kwa wakenya bila hiyana , wivu, uoga ama shaka za Nyerere na wengi wakaelimika huku watanzania wakiboresha lugha ya Kiswahili, Matokeo ni kwa wakenya kuerevuka zaidi na hivyo kujua haki zao mapema kuliko watanzania waliokuwa katika maisha ya kishamba ya kilimbukeni.

Ajabu Nyerere sungura mjanja alielimika hadi chuo kikuu lakini hakutaka watanzania wasome akihofia wangetisha uongozi na falsafa yake mbovu ya ujamaa ambayo mwisho aliikana na kukiri alifeli !. Swala la ukabila ni la kidunia.Karibu kila nchi kuna ukabila.Kenya ukabila uko lakini umedhibitiwa kwa sababu wakenya wanajali na kulinda nchi yao ingawa ukabila uko.

Kenya haijakuwa kama Rwanda ambapo karibu watu milioni moja waliangamia katika mauaji ya halaiki ya 1984. Tukumbuke Rwanda ni ndogo na ilihusisha makabila mawili tu ya Hutu na Tutsi ilihali Kenya ina makabila takriban 43. Tanzania ina makabila zaidi ya 100. Twaweza kusema changamoto za kikabila ziko kila mahali lakini huzidi katika nchi yenye makabila machache ama moja lenye nguvu na watu wengi linalotaka kutawala makabila mengine.


Wingi wa makabila Tanzania ambayo mengi ni madogo madogo dhaifu pia hupunguza ukabila tofauti na Kenya ambapo makabila makubwa ni machache lakini yenye nguvu kama wakikuyu na waluo. Ni kinaya kikubwa kwa Tanzania kuwapa wakenya mawaidha ya kuacha ukabila kwani wao pia wana changamoto sufufu za kisiasa ambazo hazijatatuliwa na chama cha kidikteta cha mapinduzi -CCM.

Rais Magufuli anaonekana ni kiongozi wa kiimla ambaye anawahangaisha waandishi wa habari kwani anapenda kusifiwa lakini hapendi kukosolewa. Bwana huyu mfupi wa miwani kama daktari wa kibaniani amelaumiwa na asasi za kulinda haki za binadamu za kimataifa kama AMNESTY kwa kuwatesa , kuwafurusha, kuwafunga na hata kuwaua waandishi wa habari na wakereketwa wa kisiasa.


Swala la sugu la Zanzibar pia ni kero Tanzania kwani wazanzibar wamelalama kuwa hawana haki kwa kunyanyaswa kila uchao hadi kudaI taifa lao huru. Tanzania mpaka sasa wanajikokota katika kutekeleza ama kuwa na katiba ya taifa ilivyo Kenya.Hapa Kenya imekuwa nchi ya pekeeAfrika kuwa na katiba mpya ya wananchi. Ziada ya yote viongozi kwenye utawala wakiongozwa na Rais Uhuru Kenyatta wamewashirikisha wapinzani katika mwelekeo wa taifa kwa mfano Raila Oginga.

Mbona Magufuli hataki kuwashirikisha wapinzani kina Augustine Mrema wa TLP, Freeman Mbowe wa Chadema, Sheikh Shariff Hamad wa CUF alivyofanya Uhuru kwa Raila? Majuzi vyama vya upinzani vilisusia uchaguzi ambapo chama tawala cha CCM kilishinda karibu viti vyote.Kiongozi wa Chadema Freeman Mbowe asema walisusia kwa kunyanyaswa na gandamizi za Magufuli. Kwa hivyo ni unafiki mkubwa kwa kina Palamambanga kuwapa mwaidha wakenya kuhusu uongozi bora na ukabila ikiwa nchi yake inaendeleza uovu huo.Kweli nyani haoni kundule!
 
Tatizo la Kenya ni ukabila. Tatizo la Tanzania ni uvyama. Tena mbaya ni chadema na CCM. Tusipo angalia tutasambaratika Kuliko Kenya. Kabudi kabla ya kuteuliwa kuwa mbunge wa kuteuliwa na kuwa Waziri. Watanzania walikuwa wakimpenda Hasa wapinzan. Sasa mambo yamekuwa kinyume. Kuteuliwa na Rais. Tena wa CCM. Ujui kitu
 
Hongera kwa kuliona hilo lakini pia kuna shida zilitokea huko Kenya hata baada ya kuipata Katiba mpya mpaka mizozo ikawa mibaya. Katiba mpya haifanyi kitu chochote kama hakuna Political Will au utashi wa kisiasa kwenye jambo lenyewe. Ni kama vitabu vitakatifu vipo ( Biblia na Quoran) vinakataza kufanya mabaya lakini yanafanyika tu.

Alafu jambo lingine wenzetu kwa upande wa upinzani wanapaswa kulijua ni kwamba kususia uchaguzi halisaidii sana mana kama kule Znz walisusia uchaguzi kwa hiyo munawalahisishia upande wa chama tawala mambo yao yaende vizuri bila upinzani wowote. Make sure munawapa "tuff time" sio KITONGA style kama inavyotokea.
 
Wakenya ni kweli ukabila umewasumbua kwa miaka mingi tangu wapate uhuru. Tatizo ukweli huwa huchukua upande moja na huwa unauma unaposemwa hadharani.

Sisi hatuna ukabila na tumekuwa hivyo kwa miaka mingi. Nyerere alikuw mzanaki Kawawa alikuwa mngoni.

Magufuli mtu wa Chato, Samia mzanzibari Kassim mtu wa Ruangwa, hatuna asili ya vyama vya kikabila.

Kenya mpaka kuwa na katiba mpya walikufa watu zaidi ya 1000 chanzo kikiwa ni siasa mbovu za kikabila.

Kabudi aliongea kwa nia ya kujenga umoja kulingana na dhima ya jambo lililompeleka kule, tatizo letu wabongo ni lile lile la negative mindset kwenye kila jambo tunaloliongelea.
 
Mwandishi kajitahidi sana kuandika kiswahili, lakini bado ni lugha inayompa shida. Hilo moja.

Pili, nitarudi nikuchambue hatua kwa hatua, bila ya kumsifia Kabuti au huyo aliyemtuma. Nitaitetea Tanzania dhidi ya Kenya katika mambo kadhaa aliyoyataja kama Ukabila, elimu na kupevuka kwa wakenya dhidi ya waTanzania, katiba ya kunukuu kutoka Marekani na ambayo ipo lakini haitekelezwi, na mengine mengi ya upotoshaji kama Mwalimu Nyerere kutoendeleza elimu Tanzania.

Kwa ujumla, kuna machache sana Tanzania inayoweza kujifunza kama mifano toka Kenya.
 
Tatizo la Tanzania wana fikiri wanayo yafanya hayaonekani au kusikika. Yaani viongozi was awamu hii wame pigwa upofu. Na mioyo yao ime kuwa kama ule wa Mfalme Herode. Ila kuna pigo laja
Tatizo la Kenya ni ukabila. Tatizo la Tanzania ni uvyama. Tena mbaya ni chadema na CCM. Tusipo angalia tutasambaratika Kuliko Kenya. Kabudi kabla ya kuteuliwa kuwa mbunge wa kuteuliwa na kuwa Waziri. Watanzania walikuwa wakimpenda Hasa wapinzan. Sasa mambo yamekuwa kinyume. Kuteuliwa na Rais. Tena wa CCM. Ujui kitu
 
Huyu mwandishi kaamua kwa makusudi kuikashifu Tanzania na viongozi wake wakuu hivyo apuuzwe maana haya ni maoni yake binafsi na sio ya Wakenya waliomualika Kabudi.
 
Yaani huu upuuzi wa huyu aliyeandika sijui ni kiluhya au kiluo au kamba sijui kiwaterere warere ndo unaleta hapa. Ile hotuba aliyoitoa kabudi wewe hutawahi itoa mahali popote mpaka unamaliza mwendo wako hapa duniani.
 
Kuna tofauti kubwa kati ya uropokaji wa Magu na Kabudi.

Magu ata pale anapotoka nje ya script aliyoandaliwa unaona it is a spontaneous reaction kutokana na tukio/habari/jibu ambalo limetokea bila ya kupangwa hapo atajibu kutokana na personality yake badala ya nafasi yake. Na mara nyingi intention not to put ppl down hila tu akikerwa ata private inaonekana that’s how he responds na si ajabu baadae anajutia how he handled it.

Kabudi ni mtu mwenye majivuno sio tu kwamba muda wote anaongea kama vile he has high authority bali pia kama vile anaongea na wanafunzi wa chuo darasani. Hili ndio tatizo lake the guy needs public speaking training kujifunza umuhimu wa tone na kuchagua maneno ya kutumia unapoongea na watu wenye different levels of perception, background and social status.

Uwezi ukawa kila siku we ni mtu wa kujifanya unawapa watu elimu au opinion zako ukadhani everyone shares your concluded views, binafsi wala sishangai wakenya kukerwa na ile speech.
 
Kilatha,
Eti kilichomfanya siku ile kuhama kutoka kiswahili na kuzungumza lugha ya malkia Ni nini!!!!!!.Lugha ya kiswahili alizungumza vizuri(ila Kuna mahali alisema NACHUKUA NAFASI HII)..sijui Kwa wataalam wetu wa kiswahili kama alikuwa sahihi watanisaidia...ila msemakweli mpenzi wa Mungu Waziri Yuko vizuri..anajua kujieleza vizuri na kikubwa ana ufahamu Mkubwa wa historia ya mambo mbalimbali...(ila Waziri siku nyingine ukiamua kutumia Kiswahili au lugha ya malkia..tumia mwanzo mwisho
 
Back
Top Bottom