Mr muhuni
JF-Expert Member
- May 26, 2014
- 1,304
- 1,268
Kenya Imezindua Ndege Zake Mpya Aina Ya Boeing 787 Dramliner Zenye Uwezo Wa Kubeba Abiria 234 Kila Moja Ambazo Zitafanya Safari Za Moja Kwa Moja Kutoka Uwanja Wa Ndege Wa Kimataifa Wa Jomo Kenyata (JKIA) Nairobi Hadi Uwanja Wa Ndege Wa John Kenedy (JFK) New York, Marekani. Tiketi Za Kawaida Zinauzwa Ksh. 89,000 ($890). Kenya Airways Itafanikisha Safari Hizo Kwa Ushirikiano Na Shirika La Delta Airlines La Marekani. Mambo Muhimu Kuhusu Safari Hiyo: Safari Hiyo Itachukua Saa 15 Kutoka New York Hadi Nairobi Na Saa 14 Kutoka Nairobi Hadi New York. Kila Ndege Itakuwa Na Marubani 4 Na Wahudumu 12. Safari Zote Zitafanywa Na Ndege Za Kisasa Aina Ya Boeing 787 Dreamliner Ambazo Hubeba Abiria 234 Kila Moja. Ndege Za Kwenda Marekani Zitaondoka JKIA Nairobi Saa 23: 25 Na Kufika JFK New York Kesho Yake Saa 06: 25. Ndege Za Kurudi Nairobi Zitaondoka New York Saa 12:25 Na Kutua JKIA Nairobi Saa 10:55 Kesho Yake.
Source
Ukawa Washington
Source
Ukawa Washington