kalamu ya chuma
JF-Expert Member
- Jan 22, 2014
- 214
- 62
Siku kadhaa tu zimepita toka Rais Magufuli kujitokeza hadharani na kusema wameingia deal na Uganda kujenga Bomba la Mafuta litakalopitia ukanda wa kaskazini ukianzia Jijini Mwanza hadi Tanga na hivyo kuipiku Kenya ambaye ni Rafiki mkubwa wa Uganda hasa UHURU KENYATTA na Museveni. Kwa kinachoendelea ni kwamba kampuni ya Mafuta ya TOTAL iliona hali ya kusafirisha mafuta kama wadau wakubwa kaskazini mwa kenya si salama na hivyo kuigeukia Tanzania Kama mbadala wa uhakika kiusalama. Kenya juzi kupitia wizara ya madini imeunda kikosi kazi cha kuhakikisha kinaishawishi upya Uganda ighaili ujenzi wa Bomba la Mafuta hapa kwetu na badala yake iendelee na mipango yake kama ilivyopanga kwani wanaona ni aibu nchi yetu kuipiku Kenya.
Kwa maana hiyo imeundwa task force ya kuwakutanisha Uhuru Kenyatta na Museveni ili kumaliza deal hilo, my take tusinyamazie mipango hii tusimame imara na kupigana kiume kwani wamezoea kujifanya wanajua kila kitu, walianza na Kilimanjaro wamekuja Olduvai sasa wanakuja na bomba, hapana kataeni hili mlioko serikalini maana Wakenya kwa kutake over wanaweza kutuyumbisha kama walivyofanya ujenzi wa barabara ya lami Serengeti.