Kenya, Tanzania katika mzozo mpya wa maji

Kenya, Tanzania katika mzozo mpya wa maji

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,273
Reaction score
25,297
KENYA.jpg

Dar/ Nairobi. Ukanda wa hifadhi za Taifa za Serengeti na Maasai Mara nchini Kenya ambao una mojawapo kati ya maajabu manane ya dunia yanayovutia watalii, unakumbwa na tishio la kimazingira kutokana na nchi hizo mbili kuingia katika mgogoro wa kugombania maji.

Ajabu lililopo baina ya hifadhi hizo ni lile la kuhama kwa wanyama waitwao nyumbu.

Mvutano huo mpya unaibua mgogoro kati ya nchi hizo jirani ambazo ni vigogo ndani ya Jumuiya Afrika Mashariki (EAC).

Mgogoro huo unatokana na uamuzi wa Serikali ya Kenya kujenga mabwawa mawili katika Mto Mara ambayo wataalamu wanaonya kuwa yatakausha ukanda huo na kuathiri uzao wa ndege katika Ziwa Natron, huku Tanzania ikipanga kuvuna maji katika mto huo na kuufanya usitiririshe ipasavyo maji yake katika Ziwa Victoria.

Kenya inatarajia mradi huo utasaidia kumwagilia mashamba karibu na chanzo cha mto huo katika Msitu wa Mau na kumaliza tatizo la maji kwa wakazi wa maeneo hayo. Hata hivyo, wataalamu wa mazingira wanaeleza kuwa hatua hiyo itaathiri zaidi upatikanaji wa maji ukanda mzima hasa mwisho wa mto huo na madhara hayo kuathiri hadi Tanzania.

Mto Mara ni maarufu duniani kutokana na wanyama hao kuuvuka hususan uhamaji wao wa kila mwaka kutoka upande mmoja wa nchi kwenda mwingine.

Kati ya Julai na Septemba kila mwaka, idadi kubwa ya nyumbu huwasili katika kingo za mto huo na hujikusanya kwa muda katika eneo hilo na baadaye huanza safari ya kuhamia upande wa pili kwa kuchagua sehemu moja ya kuvukia katika mto huo.

Kitendo cha wanyama hao kuhama kila mwaka kwa kujikusanya kwa pamoja na kujitupa kwenye mto wenye mamba lukuki ili kuvuka upande wa pili, kimelifanya tukio hilo kuwa ni moja ya maajabu manane yaliyopo duniani.

Inakadiriwa kuwa nyumbu takriban milioni 1.5 wakisindikizwa na kundi kubwa la pundamilia, pofu, swala na digidigi huhama kila mwaka kutoka Serengeti Tanzania na kwenda Hifadhi ya Maasai Mara nchini Kenya katika jitihada za kutafuta chakula.

Asili ya mvutano huo wa maji upo katika mpango kazi wa mwaka 2002 wa Kenya unaopanga kuhamisha kiwango kikubwa cha maji kutoka Mto Emala kwenda Ewaso Ngiro katika eneo la chanzo cha maji cha Bonde la Ufa.

Ripoti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Maji ya Mpango wa Uhamishaji wa Maji, Bonde la Mto Mara ya Kenya (2017-2022) inaeleza kuwa umwagiliaji utakunywa kiasi kikubwa cha maji kutokana na kutumia kati ya asilimia 70 hadi 80 ya maji yote. Jambo hilo limewavuta wanamazingira wa Tanzania walioeleza ujenzi huo wa mabwawa Kenya utasababisha madhara makubwa katika mazingira ya Serengeti, huku wakitanabaisha kwamba asilimia 75 ya ndege aina ya flamingo wadogo huzaliwa maeneo ya Ziwa Natron.

Hata hivyo, kaimu mkurugenzi anayeshughulikia masuala ya maji yanayohusu nchi mbili wa Kenya, Gladys Wekesa anasema hadi sasa ujenzi wa mabwawa hayo haujaanza na hawana mpango wa kuhamisha maji yote kutoka Mto Mara na kwamba, mradi huo unafanywa kwa kuzingatia masilahi ya pande zote mbili.

Wekesa alisema Bwawa la Amala ni sehemu ya mpango wa uendelezaji rasilimali maji wakati lile la Norera linalotarajiwa kuendesha mradi mdogo wa umeme wa kilowati 90 litakuwa na ukubwa wa mita za ujazo 450,000.

Alisema mradi huo ulipangwa na kukubaliwa na pande zote mbili lakini anashangaa kuona maofisa wa Tanzania wanageuka.

Hata hivyo, Bakari Mnaya na Mtango Mtahiko wa Mamlaka za Hifadhi za Taifa (Tanapa) pamoja na Profesa Eric Wolanski wa Chuo Kikuu cha James Cook cha Australia wanasema katika ripoti yao kuwa, kutokana na kiwango cha maji kilichopo mahitaji ya sasa yanaweza kutimizwa bila kuharibu hifadhi ya maji.

Katika ripoti hiyo wanaeleza kuwa hakuna uhakika kuwa maji yaliyopo yatatimiza mahitaji ya baadaye hususan kipindi cha kiangazi kikali iwapo nchi zitaendelea kuendeleza miradi mikubwa inayotumia maji mengi.

Mwananchi
 
Issue zingine hakuna haja ya kuzikuza ama kuingia kwenye Mgogoro zaidi ya kutumia busara tu kuzimaliza!
 
Hizo hela wangezitumia kujengea madaraja kwenye mto mara ili wanyama wetu wasiliwe na mamba au kufa kwa maji itapendeza
Wanyama kuliwa ndiyo kunaleta balance huko walipo, binadamu hatutakiwi kuingilia kati mkuu, kila mnyama au mdudu au mmea una nafasi yake, hatutakiwi kuchokonoa huo mfumo aise..
 
Wanyama kuliwa ndiyo kunaleta balance huko walipo, binadamu hatutakiwi kuingilia kati mkuu, kila mnyama au mdudu au mmea una nafasi yake, hatutakiwi kuchokonoa huo mfumo aise..
Wakisha jenga madaraja waruhusu Nyama pori zianze kuuzwa kwenye mabucha kwa bei ambayo ni rafiki kwa wanyonge na walipe kodi, hiyo itasaidia kubalance nature badala ya kuwaachia mamba wanufaike peke yao bila kulipa kodi
 
Wanasayansi au hao wa nature watakukatalia vibaya sana, wanadai ili kubalance hizo nyama pori lazima kuwe na Predators, au wanazidi kusema huko Porini lazima kuwe na Prey & Predators, Mamba lazima wawepo, ku survive kwao wanategemea hao Nyumbu, Pundamilia n.k. n.k. Watakuja kukuelekeza zaidi mkuu.
Sisi tayari tuna wanyama wetu kama Ng'ombe, Mbuzi, Kondoo n.k. n.k. Sidhani kama tunashida na Nyama pori..
 
Sisi pia ni predictors, tena sisi ni notorious predators, mamba wanakula samaki na wanyama wengine watakaokuwa wanakwenda kunywa maji
 
Sisi pia ni predictors, tena sisi ni notorious predators, mamba wanakula samaki na wanyama wengine watakaokuwa wanakwenda kunywa maji
Nakubaliana nawe, tatizo sisi hatuna shida, sisi (binadamu) tuko wengi mno, we are not surviving, ila Mamba, Simba, Chui n.k. those are surviving, their numbers are going down day by day, sisi binadamu kama hatutakuwa makini hawa wanyama watapotea kabisa, ni muhimu sisi kwanza tupunguze kuzaliana ili hao Predators in the wild waweze ku survive, ila kama mwenzangu huoni umuhimu wao hao Mamba basi ilo shauri lingine, ila sioni sababu ya sisi binadamu kula nyama pori, tayari tuna mifugo ya kutosha mpaka inaharibu ardhi!
 
Basi tuache Ugomvi uendelee ili ikitokea vita uone kama hata wanyama watasurvive
 
Hizo hela wangezitumia kujengea madaraja kwenye mto mara ili wanyama wetu wasiliwe na mamba au kufa kwa maji itapendeza

.....Hahaaa the moment daraja linajengwa na kukamilika na nyumbu kuanza kupita juu yake it will no longer the world wonders take it from me....
 
Busara itumike kunusuru magonga na jirani ndo ndugu yako

......Kuchoma vifaranga 6000.....piga mnada ng'ombe wa wananchi wangu....let's wait and see hizi busara za double standards.....
 
.....Hahaaa the moment daraja linajengwa na kukamilika na nyumbu kuanza kupita juu yake it will no longer the world wonders take it from me....
Hiyo word wonder sisi wananchi wa kawaida haitusaidii sisi tunahitaji kitoweo kwa bei rafiki
 
Back
Top Bottom