Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta (JKUAT) nchini Kenya, Brian Kibet Bera, anauguza jeraha katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta baada kupigwa risasi na polisi kwa kuingia Ikulu ya Nairobi kinyume cha sheria.
Mwanafunzi huyo, mwenye umri wa miaka 25, ambaye alikwea lango moja la Ikulu, alipigwa risasi na kujeruhiwa bega la kushoto na maafisa wa polisi wanaopiga doria kwenye lango hilo baada ya kuchomoa kisu alipoagizwa asimame.
Siku ya Jumapili Jioni Kibet aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook kwamba ataingia Ikulu.
Kwa mujibu wa msemaji wa Ikulu, Kanze Dena Mararo alisema kisa hiki kilitokea siku ya Jumatatu na mshukiwa alipelekwa katika kituo cha polisi Kileleshwa na kusajiliwa katika kitabu cha matukio nambari 39 kabla ya kupelekwa katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta kwa matibabu.
Uchunguzi unaendelea nia yake ya kutaka kuingia Ikulu kinyume cha sheria na hatua zifaazo zitachukuliwa baada ya uchunguzi kukamilika.
"Tunachukua fursa hii kukumbusha umma kwamba Ikulu ni mahali palipotengwa kuwa chini ya ulinzi mkali kwa mujibu wa sheria ya maeneo yanayolindwa (Protected Areas Act) kwasababu hiyo hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kuingia Ikulu pasi na ruhusa na mamlaka yenye jukumu hilo". Alisema Kanze