Kenya: Mwanafunzi wa Chuo Kikuu apigwa risasi baada ya kuingia Ikulu ya Nairobi kinyume cha sheria

Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Messages
18,789
Points
2,000
Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2015
18,789 2,000
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta (JKUAT) nchini Kenya, Brian Kibet Bera, anauguza jeraha katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta baada kupigwa risasi na polisi kwa kuingia Ikulu ya Nairobi kinyume cha sheria.

Mwanafunzi huyo, mwenye umri wa miaka 25, ambaye alikwea lango moja la Ikulu, alipigwa risasi na kujeruhiwa bega la kushoto na maafisa wa polisi wanaopiga doria kwenye lango hilo baada ya kuchomoa kisu alipoagizwa asimame.

Siku ya Jumapili Jioni Kibet aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook kwamba ataingia Ikulu.

Kwa mujibu wa msemaji wa Ikulu, Kanze Dena Mararo alisema kisa hiki kilitokea siku ya Jumatatu na mshukiwa alipelekwa katika kituo cha polisi Kileleshwa na kusajiliwa katika kitabu cha matukio nambari 39 kabla ya kupelekwa katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta kwa matibabu.

Uchunguzi unaendelea nia yake ya kutaka kuingia Ikulu kinyume cha sheria na hatua zifaazo zitachukuliwa baada ya uchunguzi kukamilika.

"Tunachukua fursa hii kukumbusha umma kwamba Ikulu ni mahali palipotengwa kuwa chini ya ulinzi mkali kwa mujibu wa sheria ya maeneo yanayolindwa (Protected Areas Act) kwasababu hiyo hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kuingia Ikulu pasi na ruhusa na mamlaka yenye jukumu hilo". Alisema Kanze
fb_img_1560261271524-jpeg.1124675
img_20190611_174745_453-jpeg.1124677
 
FRANC THE GREAT

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Messages
1,368
Points
2,000
FRANC THE GREAT

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
Joined May 27, 2016
1,368 2,000
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu akamatwa kwa kuingia Ikulu kinyume cha sheria

1560265315468-png.1124688

Ikulu ya rais, Kenya

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta (JKUAT) nchini Kenya, Brian Kibet Bera, anauguza majeraha katika katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta baada ya kupigwa risasi na polisi kwa kuingia Ikulu ya Nairobi kinyume cha sheria.

Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 25, ambaye alikwea lango moja la Ikulu, alipigwa risasi na kujeruhiwa bega la kushoto na maafisa wa polisi wanaopiga doria kwenye lango hilo baada ya kuchomoa kisu alipoagizwa asimame.

Siku ya Jumapili Jioni Kibet aliandika katika mtandao wake wa Facebook kuwa ataingia Ikulu.


Kwa mujibu wa msemaji wa Ikulu, Kanze Dena-Mararo Kisa hicho kilitokea Jumatatu na mshukiwa alipelekwa katika Kituo cha Polisi cha Kileleshwa na kusajiliwa katika Kitabu cha Matukio nambari 39 kabla ya kupelekwa katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta kwa matibabu.

''Tunachukua fursa hii kukumbusha umma kwamba Ikulu ni mahali palipotengwa kuwa chini ya ulinzi mkali kwa mujibu wa Sheria ya Maeneo Yanayolindwa (Protected Areas Act). Kwa sababu hiyo, hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kuingia Ikulu pasipo na ruhusa ya mamlaka yenye jukumu hilo.'' alisema Bi Kanze.


Ameongeza kuwa uchunguzi unaendelea kubaini nia yake ya mshukiwa huyo kuingia Ikulu kinyume cha sheria na hatua zifaazo zitachukuliwa baada ya uchunguzi kukamilika.

Kisa hicho kimezua mjadala mkali katika mitandao ya kijamii nchini Kenya huku baadhi watu wakihoji kwanini mwanafunzi huyo aliamua kuchukua hatua hiyo.


Wengine kama DiMacharia wanasema huenda alichukua hatua hiyo baada ya kutumia kileo fulani kwasababu mtu aliye na akili timamu hawezi kudhubu kufanya hivyo


Kuna wale walioamua kufuatialia mjadala huo katika mtando wa kijamii wa Twitter ambao wameshangazwa na baadhi ya maoni ya watu wanaompongeza mwanafunzi huyo.

Kwa mfano Danvas Nyabasa anasema Kibet sio mwendawazimu bali ana hasira kama mtu mwingine yeyote anaehisi kunyanyasika kutokana na hali ngumu ya maisha. Nyabasa anasema rais atarajie wageni zaidi ikiwa hataingilia kati kuwasaidia Wakenya wanaozongwa na umasikini na kutoa wito kwa mamlaka kuingilia kati suala hilo.

Nae Cyrus Yegon anasema ''Hii ni ishara wazi kuwa vijana nchini Kenya wanakabiliwana msongo wa mawazo kutokana na ukosefu wa ajira".


Unafahamu nini kuhusu Ikulu ya rais wa Kenya?
  • Ikulu ya Nairobi ndiyo makazi rasmi ya Rais wa Jamhuri ya Kenya lakini awali ilitumika kama ofisi rasmi ya gavana wa Afrika Mashariki.
  • Ikulu ya Nairobi ilijengwa 1907 kama makazi rasmi ya gavana wa mkoloni Mwingereza aliyesimamia kanda ya Afrika Mashariki (British East Africa).
  • Ikulu ya Rais imekuwa makazi rasmi ya kiongozi wa taifa la Kenya tangu uhuru 1963.
  • Ramani ya Ikulu ilichorwa na msanifu majengo maarufu wa Uingereza Sir Herbert Baker anayetambulika kwa kuchora ramani za majengo ya serikali nchini India na Afrika Kusini.
  • Nyakati za ukoloni, Ikulu ilifahamika kama jumba la serikali (Government House) na ilitumika kama makazi rasmi ya magavana wa ukoloni waliotumwa kusimamia Kenya.

Chanzo: BBC
 
mwaswast

mwaswast

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2014
Messages
9,500
Points
2,000
mwaswast

mwaswast

JF-Expert Member
Joined May 12, 2014
9,500 2,000
Nitasema Tena, Wakenya wanajitambua dio Kama hapa kwetu kusifia jiwe Kama Mungu hata wakati maisha ni magumu bado tunaimba sifa na kumwabudu kininga mtu moja. Kudos Nyang'aus.
 
Waterloo

Waterloo

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2010
Messages
16,366
Points
2,000
Waterloo

Waterloo

JF-Expert Member
Joined Nov 30, 2010
16,366 2,000
Kayataka mwache wamlambe shaba
 
Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Messages
18,789
Points
2,000
Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2015
18,789 2,000
Wameona wasimuue kulinda uchunguzi, ingekuwa nchi nyingine huyu Kibet...! Tungesema mengine!
 
Richard irakunda

Richard irakunda

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2018
Messages
3,176
Points
2,000
Richard irakunda

Richard irakunda

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2018
3,176 2,000
Nitasema Tena, Wakenya wanajitambua dio Kama hapa kwetu kusifia jiwe Kama Mungu hata wakati maisha ni magumu bado tunaimba sifa na kumwabudu kininga mtu moja. Kudos Nyang'aus.
Kumbe wewe ni mjinga hivi ?
 
Viatu vya Samaki

Viatu vya Samaki

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2015
Messages
19,376
Points
2,000
Viatu vya Samaki

Viatu vya Samaki

JF-Expert Member
Joined May 11, 2015
19,376 2,000
Kuna Vikenya vitakuja kusema humu kuwa vina vyombo imara vya ulinzi.

Nyang'au, sisi huyo mtu angefia barabara ya kuingia Ubungo....
 
moj6

moj6

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2017
Messages
1,542
Points
2,000
moj6

moj6

JF-Expert Member
Joined Nov 2, 2017
1,542 2,000
Ingekuwa Tz angepigwa chuma ya kichwa,shit hole country
 
Richard irakunda

Richard irakunda

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2018
Messages
3,176
Points
2,000
Richard irakunda

Richard irakunda

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2018
3,176 2,000
Huyo jamaa ujumbe aliouandika kwenye mitandao na kitendo cha kukwea ukuta akiwa na silaha ni sababu tosha kabisa ya kumpasua kichwa

Kiufupi kama jamaa angepenya nadhan now tungekuwa tunatoa pole
Ingekuwa Tz angepigwa chuma ya kichwa,shit hole country
 
M

mbu wa dengue

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2014
Messages
1,058
Points
2,000
M

mbu wa dengue

JF-Expert Member
Joined Jun 2, 2014
1,058 2,000
Huyo jamaa ujumbe aliouandika kwenye mitandao na kitendo cha kukwea ukuta akiwa na silaha ni sababu tosha kabisa ya kumpasua kichwa

Kiufupi kama jamaa angepenya nadhan now tungekuwa tunatoa pole
Lakini mkuu Kama ww ni Askari Kuna haja gani ya kutumia nguvu kubwa ya bunduki kumuua mtu asiye na bunduki?
 
Waziri wa Kaskazini

Waziri wa Kaskazini

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2015
Messages
4,131
Points
2,000
Waziri wa Kaskazini

Waziri wa Kaskazini

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2015
4,131 2,000
Walinzi walikuwa wapi hadi akaruka ukuta?
 
Chillah

Chillah

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2016
Messages
5,017
Points
2,000
Chillah

Chillah

JF-Expert Member
Joined Oct 12, 2016
5,017 2,000
Lakini mkuu Kama ww ni Askari Kuna haja gani ya kutumia nguvu kubwa ya bunduki kumuua mtu asiye na bunduki?
Hivi una zani hizi silaha zipo kwa ajiri ya wakina nani? Ma nuklia magobole nk...
 

Forum statistics

Threads 1,307,094
Members 502,332
Posts 31,601,440
Top