The Quonquerer
JF-Expert Member
- May 14, 2009
- 777
- 111
Ndugu yangu nilikuwa gizani enzi za ujima na baba wetu wa taifa, wakati haturuhusiwi kuona nchi za wenzetu zilizoendelea zikoje na kabla shule haijapanda. Hivi sasa nimetembea na kuona kwa wenzetu na kugundua kuwa sisi ndio tulikuwa gizani. Ownership sio tatizo, mradi watu walipe kodi na kushindana fairly...kwa taarifa yako wakati wa Mwinyi kabla ya PSRC, Ma SU mengi yalikuwa yakitegemea ruzuku ya serikali kusurvive, sasa swala kuu ni kuwa je ni kazi ya serikali kubeba mashirika au kuongeza juhudi na tija kwenye huduma za jamii?
Nafikiri wengi tutakubaliana kwanza kuwa jukumu kuu la serikali ni kuhakikisha kuwa watu wake wanaishi kwa amani(ulinzi na usalama), kuendeleza miundo mbinu (barabara, umeme, maji n.k.), elimu na afya kwa raia wake na kukusanya kodi kwa uhakika. Sasa enzi za Mwalimu serikali ilikuwa bize kuyainua haya ma SU huku ufanisi ukiwa hoi, ukusanyaji kodi ilikuwa ni kichekesho . Pamoja na matatizo yote mi na imani tuko kwenye right track hivi sasa angalau shule na vyuo vimeongezeka, barabara zinajengwa na uchumi unakua. GDP ya TZ between 1961 na 1985 Nyerere alipotoka hardly change angalia sasa tulipo. Mafisadi ndio tatizo sasa na hili ni jukumu letu wote watanzania kulipa vita kama tunavofanya hapa JF.
Ili kuiendeleza nchi yetu ni muhimu tushirikishe wageni regardless kama ni wakenya (albeit foreign own) haijalishi hiyo, mradi hawa wanalipa kodi na kutupa ajira watanzania ndio kitu cha muhimu. Na uchumi wetu unakua, watoto wetu wanaenda shule, barabara zetu zinajengwa na hospitali. Hivi ndio vitu vya kuboresha sio longolongo kuhusu nania anamiliki makampuni ya Kenya na bla bla nyingine ambazo hazina tija...
Haya ni mawazo yangu, Nawakilisha
WaMzizima:
Hivi kuna mkuu anakataa vitegauchumi kutoka nje? Hata shareholding zao hazituhusu pia. Mmachinga kama Smatta anataka kudanganya kuwa hisa za makampuni yote ya wakenya ni za Wakenya yaani wakikuyu, wapokot na wajaluo..hii si kweli na hata ikiwa it's none of our business, ila aache uongo na arrogance. Ikitokea kampuni ikawa ya mkenya ni wale wanasiasa kina Biwot ambao waliwaibia wakenya wenzao, sasa unadhani ni wakenya wangapi wameathirika na wizi huo, ambao mpaka ni maskini choka mbaya. Unemployment rate ya Kenya iko at 40%, hivi hao kweli ni watu wa kujifunza kwao!?
Ukimwambia aende TIC huyo hawezi, ni kuuza bidhaa feki tu. Iwapo sheria za nchi zinafuatwa, yaani ajira kwa mgeni mwiko hasa kwa zile kazi zinazoweza kufanywa na mtanzania, mbona sioni tatizo! Kina Smatta wanachotaka ni free movt of labor, free land kwa wakulima wa jembe (kukimbia ukame), na kutembea na vipande vyao Tanzania..kitu a ambacho wameula wa chuya! I am for free movt of capital myself ili mradi walipe kodi na wasilete vinarua wao kuganga njaa!