Kenya: Mchungaji awatimua kanisani waumini wenye shahada ya kwanza

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,128
49,863
Mchungaji wa Kanisa la Neno nchini Kenya, James Ng’ang’a amewaacha watu wengi midomo wazi baada ya kutoa onyo kwa waumini wake waliohitimu shahada ya kwanza kuwa waache kuhudhuria kanisani hapo endapo hawatamsikiliza mafundisho yake.

Tamko la Ng’ang’a linakuja wakati ambapo mijadala inaendelea kuhusu mapendekezo ya Serikali ya Kenya kudhibiti makanisa, na kuwataka wachungaji kuwa na elimu ya msingi ya Thiolojia.

Kwenye video iliyochapishwa mitandaoni, Ng’ang’a, anaskika akirusha maneno na matamshi mazito kuhusu washirika wake wenye shahada.

“Wenye shahada msije ninapohubiri, nendeni kwenye makanisa yenu mnayohudhuria ibada fupi za dakika mbili, hamuwezi kutawala mambo ya kiroho. Hao wasomi tuheshimiane, Daudi hakujifunza na hata manabii aliowapaka hawakujifunza,” amesema.

Ng’ang’a pia alishutumu watu waliosoma kwa kuumiza ulimwengu, haswa kuhusu masuala kama vile mapenzi ya jinsi moja.

“Watu wasomi wameharibu dunia. Hao ndio wameleta suala hili la mapenzi ya jinsi moja. Majaji waliidhinisha, na sisi sote tuliona na kushuhudia. Kisha mnasema wahubiri ambao hawajasoma hawaweziku hubiri nchini Kenya, aje? Kwa nini?” ameshagaa.

Mwananchi.

===

Dini zinazidi kuonekana ni Fix Kadiri muda unavyoenda.

Waliozileta dini walishazipotezea ila wapokeaji Sasa wanakaza Kwa mambo wasiyoyajua.
 
punda afe mzigo ufike!!
 
Ameona wasomi watamuharibia maokoto bora abaki na vilaza ni rahis kuwa buruza atakavyo na kuwarubuni kwa urahisi
 
Back
Top Bottom