De Javu
JF-Expert Member
- May 5, 2010
- 264
- 33
Kenya ipo mbioni kujenga bandari ya kina kirefu katika mji wa Lamu itakayo gharimu US $22 billions. Jiwe la msingi linategemewa kuwekwa mapema January 2011, Mwai Kibaki anataka ujenzi uanze kabla ya muhula wake wa uraisi unaoisha 2012. Katika ujenzi huo utajumuisha Uwanja wa Ndege wa kimataifa pamoja na reli itakayounganisha Ethiopia kupitia Sudan kusini na baadae nchi zingine za Afrika ya kati. Pia katika mradi huo utajumuisha bomba la mafuta toka bandari ya Lamu hadi Sudan kusini. Kibaki ameahidiwa mkopo alipotembelea China wa KShs 1.2 billions kwa ajili ya bandari. Kampuni ya kijapani pia nayo inautupia jicho mradi wa bomba la mafuta (Lamu-Juba pipeline project). Lini mradi huu utakwisha itategemea na hali ya baadae baada ya kura ya maoni ya kujitenga baina ya serikali ya Khartoum na Sudan kusini itakayo fanyika baadae 2011.