KENYA : Madaktari wanaogama waongezewa mishahara baada ya kuzungumza na Rais

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
20,415
2,000
Serikali ya Kenya imekubali kuwaongezea Madaktari kwa dola 550 za kimarekani madaktari wenye mapato ya chini na kuifanya mishahara yao ifikie dola 1,970 za kimarekani kwa mwezi, ikiwa ni hatua ya kumaliza mgomo wao uliodumu kwa mwezi mmoja kote nchini humo

Hatua hiyo imetolewa kufuatia mkutano kati ya Rais Uhuru Kenyatta na wawakilishi wa Chama cha madaktari cha Kenya KMPD huko Mombasa

Kwenye mkutano huo, wawakilishi hao wameahidi kuupatia ufumbuzi wa haraka mgomo huo, wakisema watajadiliana na wenzao wa chama hicho kabla ya kujibu pendekezo lililotolewa na serikali

Mgomo huo umekwamisha huduma za afya kwenye hospitali za umma kote nchini Kenya, na umesababisha vifo vya wagonjwa 20.

Chanzo : CRI kiswahili
 
bily

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
8,040
2,000
Hongera zao ni hatua nzuri migomo ni njia sahihi katika kukabiliana na mtawala au bosi wako kazini . I salute you doctors.
 
Belo

JF-Expert Member
Jun 11, 2007
12,561
2,000
Kenya wana uchaguzi mwaka huu so huenda hii issue ikamsaidia Uhuru Kenyata kwenye uchaguzi
 
Hwasha

JF-Expert Member
Aug 22, 2015
1,271
2,000
Hatakama udaktari ni wito hawa jamaa wanajitambua sana.Hongera zao kwa kufanikiwa kupata kile walichokisimamia.
Ni kweli wanajitambua.Raha ya mgomo huu ni pale Dakatari anapopelekewa taarifa ya kifo cha mama yake mzazi aliyemsomesha kupata udaktari huu kwa shuluba kubwa ya kufanya kazi za ndani au kukimbizana na polisi kwa biashara ya gongo ili mwanae msomi aje agome kupata fedha kubwa Zaidi yake.

Shikamoo pesa.
 
kalimbwane

JF-Expert Member
Dec 21, 2016
710
1,000

Uposahihi kabisa hii inachagizwa na uhalisia wa mwanadam kutokuishi milele. Wakati ukifika hata kama wewe ni Dr. Utakufa tu, kwahiyo kufa kwa mama mtoto Akiwa kwenye mgomo nisawa tu. Haki kwanza uwajibikaji baadae.
 
Hwasha

JF-Expert Member
Aug 22, 2015
1,271
2,000
Uposahihi kabisa hii inachagizwa na uhalisia wa mwanadam kutokuishi milele. Wakati ukifika hata kama wewe ni Dr. Utakufa tu, kwahiyo kufa kwa mama mtoto Akiwa kwenye mgomo nisawa tu. Haki kwanza uwajibikaji baadae.
Ukifa unaondoka na fedha ulizozitafuta kwa gharama ya kifo cha mama
? Fedha ni muhimu lakini si kila kitu,kuna wakati tunahitaji zaidi ya fedha.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom