Kenya kutumia dola million 2.15 kununua chakula cha mifugo, TZ tunajifunza nini?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,885
FB_IMG_1488806817095.jpg

Serikali ya Kenya yatangaza kutumia dola za Kimarekani milioni 2.15 kuwapa wafugaji kununua chakula cha mifugo hadi ukame utakapomalizika nchini humo.

Toa maoni yako.

Source Eatv
 
Kwamba kuna umuhimu wa kuwasaidia wakulima na wafugaji pale matatizo yanapotokea, na si njaa tu. Hata kama homa ya miguu inaua ng'ombe serikali inapaswa kuwasaidia wafugaji kwa hali na mali, hii inawapa nguvu ya kuendelea na uzalishaji.
 
vtu vyengine ni natural selection.....ng'ombe washakua wengi ardhi inajaribu kuwapunguza na swala la mifugo kufa hata porini wild beast wanakufa kila siku au wanapunguzwa na carnivores...
 
vtu vyengine ni natural selection.....ng'ombe washakua wengi ardhi inajaribu kuwapunguza na swala la mifugo kufa hata porini wild beast wanakufa kila siku au wanapunguzwa na carnivores...
Sure thing, wanasiasa wanatafuta kura tu
 
vtu vyengine ni natural selection.....ng'ombe washakua wengi ardhi inajaribu kuwapunguza na swala la mifugo kufa hata porini wild beast wanakufa kila siku au wanapunguzwa na carnivores...
Kutokana na jiographia kuna sehemu ambazo si za wafugaji, sehemu za Pwani kama Mombasa, Z'bar na Pemba hazina historia ya ufugaji. Kama mifugo inakuwa mingi kwanini tusiipunguze kwa kutafuta njia za kisasa za kuweza kuwasafirishia nyama ndugu zetu wa maeneo haya?
 
Huku tunatumia pesa kama izo kulipa wanasheria wa serkal kuongeza juhudi za kumuweka lisu jera na kuweka mafuta kwenye defender kumsafirisha lisu kutoka singida hadi dar
 
Naamini huo ni mtaji wa kisiasa tu kuelekea uchaguzi mkuu wa Kenya. Hata kwetu ikifika 2019 matatizo kama haya au matetemeko hakuna atakaye ambiwa serikali haikuleta hilo tatizo ila wataambiwa tulikuwa tunasaka hela kwa sababu mafisadi waliziiba so sasa hivi zipo watapewa na huduma zote muhimu.

Sishangai kwa hao wa Kenya maana kipindi hiki wanasiasa ndio wanakuwa watumwa wetu kweli.
 
View attachment 477432

Serikali ya Kenya yatangaza kutumia dola za Kimarekani milioni 2.15 kuwapa wafugaji kununua chakula cha mifugo hadi ukame utakapomalizika nchini humo.

Toa maoni yako.

Source Eatv
Ninamtafuta huyo aliyetamka hayo maneno nimtumbue. Haujui mimi ndiye chairman wa eacommunity? Mimi ninataka kujenga barabara wewe unasema ununue chakura cha Ng'ombe na mbwa? Wewe hebu potea
 
Back
Top Bottom