Msema yote
JF-Expert Member
- Mar 19, 2013
- 448
- 301
Habari wadau!..
Vugu vugu la ukuaji wa teknolojia kwa nchi afrika wenzetu kenya wameamua kufanya kwa vitendo, Wakenya wote kwa pamoja wameweka tofauti zao za kiasiasa pembeni na kushiriana na serikali yao kuhakikisha maadhimio yao ya kuwa na mji wa kisasa wa teknolojia unakamilika ndani ya wakati.
Mji huu ambao umepewa jina la Sillicon Savannah utakuwa mji wa teknolojia, kama ulivo mji wa Sillicon Valley wa Marekani ambapo makampuni yote makubwa ya teknolojia yanapatikana hapo, kuanzia Google, facebook, ebay, Amazon, Octopus, Twitter, Instagram, whatsAap, Yahoo, eblogger, hp, YouTube, Android, Cisco, Intel na mengine mengi.
Mji wa wa Sillicon Savannah pia unategemewa kuwa na makumpuni kama hayo pia kutakuwa na sehemu na vituo vikubwa vya kuhifadhi nyaraka (Data Center), sehemu za kujifunzia na kukutana na wataalam mbali mbali (Hub), sehemu za kurudisha nyaraka mbali mbali zilizopotea (Data Recovery Store), Makampuni ya kutengeza program (Software Companies) ,Vyuo vikuu vya teknolojia, Shule za kimataifa (Internation Schools) Hospitali kubwa na za kisasa, Mahoteli Makubwa Viwanda vya kugundua na kuunda bidhaa mbali mbali za teknolojia kama octopus na intel za sillicon valley marekani.
Sillicon Savannah unategemewa na serikali ya kenya kufungua fursa za kiabiashara na ajira kwa wakenya, kwani mradi huu unategemwa kutoa ajira 200,000 (Laki mbili) ukikamilika, Mradi huu ni tumaini kwa wakenya wengi sana hasa watu wa fani za sayansi.
Mradi huu unajengwa kilomita 60 toka mji wa Nairobi unategemewa kuwa kituo kikubwa cha teknolojia afrika, serikali ya kenya inategemea kukamilika kwa mradi huu mwaka 2030 na shughuli zote kuwa tayari, ikiwa ni pamoja na uwepo wa taasisi kubwa za utafiti wa sayansi
PICHA MJI WA SILLICON SAVANAH UTAVOKUWA
VIDEO MJI WA SILLICON SAVANNA UTAVOKUWA
Maoni: Ni wakati sasa kwa wataalam wataalam wa fani mbali mbali za sayansi tanzania kushirikiana, kuungana na kusihirikisha serikali ili tuwe na mipango madhubuti, tuwe na makampuni yanayotambulika kimataifa, tufanye vitu serius, serikali ishirikishe wadau mbali mbali katika hili kwani lengo ni kujenga Tanzania nzuri leo na kesho kwa vizazi na vizazi