Kenyan-Tanzanian
JF-Expert Member
- Nov 7, 2006
- 302
- 2
Guys nimemaliza kuongea na mkulu mmoja wa Pentagon sasa hivi. Kuna tatizo kubwa laweza kutokea. Inasemekana jamaa wamehold matokeo ya central na upper eastern katika vituo kama kumi ili waweze jua wanarigg vipi baada ya matokeo ya maeneo ya Raila kutoka. Mkuu anaongea hana raha, imenitisha kidogo.
Nimefahamishwa kuwa tayari ODM ina wabunge 109 mpaka sasa, hivyo ina maana tayari wameshalishika Bunge maana nusu ya Bunge ni Wabunge 105. Kuna wabunge 12 wa kuteuliwa kutokana na idadi ya viti vya kila chama. Hivyo bado ODM imeshajihakikishia viti 6 (ndio nafasi za Nyaga, Mumbi etc).
Sasa sijui itakuwaje! Ina maana jamaa waliachia matokeo ya Raila yatokeeeeee, kisha wajue cha kufanya. Isitokee fujo tu maana kumwapisha Rais aliyewekwa kwa nguvu ni hatari.

Zitto,
heshima kwako mkuu,
waambie hao ODM nao wasianze kulialia sasa. Wakae macho usiku mzima kuhakikisha kuwa kura haziibiwi. Ikiwezekana watume vijana kutoka Nyanza au Rift valley au western ambako ni chini ya masaa 4 kuendesha kutokea anywhere ili wakalinde kura zao.
Kukata tamaa hivi wakati wana nafasi ya kulinda kura zao ni kosa na wasijemlaumu mtu. SORRY but they gat to stand up walinde kura zao
Hivi hebu nielimisheni hapa maana katiba ya Kenya siijui. Rais akitoka kwenye chama ambacho hakina majority ya bunge inakuwaje? Mfano sasa hivi ODM wana zaidi ya 51% ya viti vya ubunge, itakuwaje akishinda Kibaki ataongozaje? Katiba yao inasemaje?

He is still the president. Atakuwa na wakati mgumu sana lakini bado ataapishwa. Kibaki akishinda inasemekana hapa kwamba ataunda pengine alliance na chama zingine kama ODM- Kenya ya Kalonzo. Msisahau kwamba huku ma MP wengi wa ODM watakua wagumu kuibiwa kama hapo awali alivyofanya Kibaki awamu yake ya kwanza kwasababu walipitisha Political Parties Bill wenyewe ikawa sheria kwamba mtu haezi kuiba MPs kutoka kwa chama kingine bila kuandika rasmi kwa mwenyekiti wa chama hicho hajatoa idhini.
"Rais bila wabunge wakutosha ni mahabusu wa Upinzani", Raila aliwahi kusema huku akiomba wakenya wampatie wabunge wakutosha
Tanzanian-Kenyani:
Lakini sheria hii ilikuwepo tayari hata wakati Kibaki anawa-poach ma-MPs wa Kanu kuingia katika Govt. of National Unity; hata bila kumwarifu Uhuru.
Tatizo kubwa ni kwamba wabunge wengi wanapenda sana uwaziri.
Pengine safari hii kama ikitokea patakuwepo na discipline kubwa ndani ya ODM, ili wabunge wao wasirubuniwe na kupewa uwaziri kama rushwa.
Kenya wana mfumo wa ajabu sana katika Katiba yao. Kule Mkuu wa shughuli za serikali Bungeni ni Makamu wa Rais ambae anateuliwa na Rais na wala hathibitishwi na Bunge. Hawajawahi kutest kitakachotokea sasa (kama Kibaki akishinda). Huko nyuma Moi alikua anapata minority votes za Urais lakini anapata wabunge wengi na hivyo anahitaji support kidogo sana ya nje ya wabunge wa chama chake. Mtakumbuka Raila alivyomwokoa na chama chake cha NDP wakati huo.
Hali ingekuwa tamu sana Tanzania ambapo Waziri Mkuu anatoka chama chenye wabunge wengi. Hivyo ikitokea kwa mfano CCM ikashinda Urais 2010 lakini CHADEMA ikawa na wabunge wengi, Waziri Mkuu atatoka CHADEMA na hivyo kushirikiana na Rais kuunda Serikali. Mfumo huu una afadhali kwani hauleti vurugu. Mfumo wa Kenya ni vurugu tupu ndo hupelekea Rais kuwanunua wabunge wa upinzani.
Mfumo kama wa Tanzaia ndio umechukuliwa na nchi nyingi sana za Eastern Europe kama Poland, Latvia, Lithuania, ZCheck Republic etc. Ni mfumo ambao unakuwa na Rais mwenye nguvu na pia Waziri Mkuu mwenye nguvu. Rais anakuwa na mamlaka zaidi na foreign affairs, finance na economy na Waziri Mkuu mostly domestic issues apart from currencies.
Hata hapa nyumbani ndio aina ambao Mwalimu aliutaka. Mnakumbuka Sokoine na Salim walikuwa very powerful PMs katika domestic dockets.
Naona nimejieleza sana. Ngoja niishie hapo. Ila kama Kibaki akishinda Kenya without majority in Parliament kutakuwa na crisis na kwa vyovyote vile ODM watampigia vote of no confidence na kumtoa. Nionavyo mimi!
Zitto
ni mfumo unaotaka kufanana na eastern europe kama poland lakini si sawa
Mfano Poland Waziri Mkuu naye anagombea na anapigiwa kura na ndiye anayeunda serikali yani anachagua mawaziri pia kuongoza serikali.
NA huyu waziri mkuu lazima afikishe asilimia fulani ktk senate ili aongoze lasivyo lazima aunde coalition na vyama vingine ndipo apate kuongoza.
Rais pia naye anagombea kivyake na kazi yake kubwa nikutia saini tu na hana nguvu sana kama waziri mkuu.
Tunawapongeza wenzetu mliopo East Africa, hasa Zitto na KT, maana sasa hivi ni saa 7 kasoro za usiku huko nanyi bado mnatupasha tu, ahsanteni sana. Ngoja nipunguze kunywa hizi nanihii maana naanza kusinzia sasa na hii habari ya ushindi kupungua na wizi wa kura tena inaanza kuleta minyoo tumboni!