GE2025 Kennedy Mmari achukua fomu ya ubunge Siha, Kilimanjaro

GE2025 Kennedy Mmari achukua fomu ya ubunge Siha, Kilimanjaro

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Wont be the same

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,564
Reaction score
2,483
Katika kilele cha siku ya kwanza ya mchakato rasmi wa uchukuaji wa fomu kwa ajili ya kugombea nafasi ya Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), jimbo la Siha limeandika historia yake kwa kumpokea mjasiriamali Kennedy Mmari (33) kama mgombea wa kwanza kutia nia. Ni majira ya saa 8:21 mchana, katika ofisi za CCM Wilaya ya Siha, ambapo Mmari alifika kwa utulivu akifuatana na watu wake wachache waliokuwa wakimuunga mkono.

Alichukua fomu rasmi ya kuomba ridhaa ya chama chake kuwania nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Siha katika uchaguzi mkuu ujao fomu ambayo alikabidhiwa na katibu wa jumuiya ya Wazazi wilaya ya Siha Abdalah Chumu baada ya kutimiza masharti ya uchukuaji wa fomu hiyo .

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu, Mmari ambaye pia ni mzaliwa wa Siha, amesema amefikia hatua hiyo baada ya kujipima na kuona ana uwezo wa kuwahudumia wananchi kwa namna bora zaidi, akileta mawazo mapya na mwelekeo wa kisasa katika uongozi.


Source: Clouds TV
20250629_085838.jpg
 
Back
Top Bottom