Kelele zilizotamba kuhusu njaa ya Tanzania

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
93,472
119,270
Wiki kadhaa zilizopita habari iliyokuwa ina bamba sana ilikuwa ni ile ya baa la njaa nchini. Njaa ndo ilikuwa habari ya mujini. Huku kwenye mitandao ya kijamii ndo usiseme kabisa.

Watu walivyokuwa wanaiongelea hiyo njaa mtu ungedhani nchi imekumbwa na baa kama lile la Ethiopia miaka ile ya 80.
Ila kama ilivyo ada, wengine tulijua kuwa zile kelele zilikuwa ni kama upepo tu ambao sasa ushapita.

Sasa hivi kelele za njaa hazisikiki tena [sasa sijui hiyo njaa imeisha.....kama hata kweli kulikuwa na njaa]. Habari ya mujini hivi sasa ni madawa ya kulevya.

Hivi kweli kama kungekuwepo na njaa kama ambavyo baadhi ya watu walivyokuwa wanataka kutuaminisha, si bado hilo baa ndo lingekuwa habari ya mujini...?

Kulikoni sasa.....? Nani ambaye hajala leo?
 
Mkuu subiri namalizia kuandaa list ya mapapa Wa ngada tutalifanyia kazi swala hilo la njaa uchambuzi Wa kiintelijensia baadae

Tanzania ya Matukio
 
sisi ni watu wa kusahausahau tumeshasahau tugange yajayo haya ya madawa sasa ndo yanayo trend mjini...
 
Wiki kadhaa zilizopita habari iliyokuwa inabamba sana ilikuwa ni ile ya baa la njaa nchini.

Njaa ndo ilikuwa habari ya mujini.

Huku kwenye mitandao ya kijamii ndo usiseme kabisa.

Watu walivyokuwa wanaiongelea hiyo njaa mtu ungedhani nchi imekumbwa na baa kama lile la Ethiopia miaka ile ya 80.

Ila kama ilivyo ada, wengine tulijua kuwa zile kelele zilikuwa ni kama upepo tu ambao sasa ushapita.

Sasa hivi kelele za njaa hazisikiki tena [sasa sijui hiyo njaa imeisha.....kama hata kweli kulikuwa na njaa]. Habari ya mujini hivi sasa ni madawa ya kulevya.

Hivi kweli kama kungekuwepo na njaa kama ambavyo baadhi ya watu walivyokuwa wanataka kutuaminisha, si bado hilo baa ndo lingekuwa habari ya mujini...?

Kulikoni sasa.....? Nani ambaye hajala leo?
NN hakukuwa na njaa baa na Tanzania as a whole haiwezi kupata niaa ya watu kufa kwani ili itokee kuna mabo makubwa lazima yatokee.kuchelewa mvua siyo mojawapo.
 
..nadhani haya ni mambo ya kawaida.

..yanatokea hata nchi nyingine.

..kwa mfano, Marekani alipoapishwa Trump habari ya kubwa ilikuwa ni suala la idadi ya watu waliohudhuria/na kuangalia inauguration
ceremony.

..baadaye wakahamia kwa waandamanaji wa women's march na hoja zao.

..sasa hivi kila mtu amesahau hata waandamanaji walikuwa wanadai nini, wamehamia kwenye IMMIIGRATION BAN.

..Ni kweli humu JF hatuzungumzii njaa kwa sasa hivi. Lakini huko vijijini wale wenye upungufu wa chakula na mvua za msimu ziliwapiga chenga nina hakika wanaishi kwa wasiwasi mkubwa.
 
NN hakukuwa na njaa baa na Tanzania as a whole haiwezi kupata niaa ya watu kufa kwani ili itokee kuna mabo makubwa lazima yatokee.kuchelewa mvua siyo mojawapo.

Aisee!

Sijawahi kuona watu wenye njaa ambao wana muda wa kupiga propaganda kwenye mitandao ya kijamii.

Hilo pekee tu lilikuwa ni uthibitisho tosha kuwa kilichokuwa kinadaiwa hakikuwepo.
 
..nadhani haya ni mambo ya kawaida.

..yanatokea hata nchi nyingine.

..kwa mfano, Marekani alipoapishwa Trump habari ya kubwa ilikuwa ni suala la idadi ya watu waliohudhuria/na kuangalia inauguration
ceremony.

..baadaye wakahamia kwa waandamanaji wa women's march na hoja zao.

..sasa hivi kila mtu amesahau hata waandamanaji walikuwa wanadai nini, wamehamia kwenye EMIGRATION BAN.

..Ni kweli humu JF hatuzungumzii njaa kwa sasa hivi. Lakini huko vijijini wale wenye upungufu wa chakula na mvua za msimu ziliwapiga chenga nina hakika wanaishi kwa wasiwasi mkubwa.

Mzee JokaKuu, sidhani kama baa la njaa linaweza lisiwe habari ya mujini.

Kwa hiyo ukiona tukio linapoteza kiki baada ya siku au wiki chache tu basi jua kuwa hilo tukio zima halikuwa na mashiko.

Sidhani kabisa kama baa la njaa linaweza tu kupita kama upepo.
 
Ngabu hujakumbana na mkono wa D.J Trump au unalala shimoni rudi Mkuu hakuna njaa
 
Njaa ya ukweli haiwezi kufichika achilia mbali kutokuweza kuzungumzika.

mkuu mimi nipo mahali ambapo vyakula vipo vya kununua sana sana labda tupandishiwe bei, ila nilipata kuona video moja jamaa wakilia njaa mbele ya M@GU.

-www.meteo.go.tz walisikika wakisema mwamzoni mwa mwezi kwanza kuwa mvua zimechelewa watu wameshindwa kulima kwa wakati.

-Baadhi ya viongozi walikataza nafaka kutumika kutengenezea pombe au kuchoma maindi.

haya yote yamejenga taswira kuwa kama si vitisho huenda habari zingekuwa zaidi ya hapa
 
Lini wewe umeshinda njaa?
 
Back
Top Bottom