Kelele ni nyingi kuliko ukweli

Kelele ni nyingi kuliko ukweli

pambe samanini

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2015
Posts
430
Reaction score
224
Kwanza naomba kumshukuru mwenyezi Mungu mwingi wa rehema na mwenye uhai wetu kwa kutuweka tuwe hai hadi sasa.

Pili nipongeze jitihanda mbalimbali za serikali, asasi za kirai, taasisi za kidini, jumuiya za kitaifa na kimataifa kwa kuwa mstari wa mbele kutafuta suluhu na mstakabari mwema wa taifa letu la Tanzania.

Hata hivyo imenishangaza sana kuona taasisi hizi zinavutana juu ya maoni, mtazamo na ushauri juu ya kushughulikia janga hili lilolikumba taifa letu ambalo kwa muda limesifika kuwa taifa la amani na watu wakarimu kwa watu wote.

Watanzania wenzangu tunatakiwa kujua fika na hakika kuwa Tanzania ni zawadi pekee ambayo Mungu ametupa na tunatakiwa tuiliende kwa nguvu zetu zote bila kuwa na mivutano ambayo kimsingi Haina afya njema sana kwa taifa letu na ustawi kwa watu wake.

Mashabulio yanayoyafanywa na taasisi za kidini juu ya maoni, mtazamo, na ushauri juu ya namna watu wanodai haki Yao na namna ya kudai haki hiyo, ya nataka kuleta udini na kuigawa jamii na taifa letu.

Tusitumie matamshi ya kutisha, kuhamasisha, au mihemko yetu kuharamisha maoni, ushauri wa watu wengine kiasa kwamba sisi ushauri, mtazamo na maoni yetu ni bora sana na pengine tunadhani kufanya hivyo ni suluhu na utatuzi wa janga lililotupata kama taifa. Tusitumie nyumba za ibada na kuwahamasisha waumini wetu kukabiliana na kundi fulani linalodai haki fulani, katika kukabiliana huko ndiko kunasababisha uvunjifu wa Amani na kupeleke machafuko yanayochafua taswira ya taifa letu.

Kama taasisi hizi za kirai, kidini na jumuiya mbalimbali zikifanya hivyo tutabaghaza taifa letu na kuwakosea watanzania ambao wanataka mstakabari mzuri na ustawi wa taifa lao urudi kama ulivyokuwa awali.

Taasisi ya kikristo TEC wao nadhani na kwa uelewa wao walitoa ushauri, mtazamo na maoni yao juu ya nini kifanyike juu ya yaliyolipata taifa letu, na wao wakifahamu fika kuwa hawana vyombo vya dola badala yake serikali yetu ione kama inaweza tumia ushauri huo labda utaponya taifa letu.

TEC wasichukuliwe kuwa ni maadui wa taifa hili na watu wake, kama Kuna pahala tunadhani wamekosea pasi tuwarekebishe, tuwasamehe na ikiwezekana tuwaite na kukaa nao ili kupata uwelekeo unaofanana tayari tutakuwa tunatafuta namna nzuri ya kuponya taifa hili.

Viongozi wetu wa taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali watu wengi wanawaamini sana, na hakika kile mnachokisema na kuwaambia watu wengi, mjue watakifanya kikamilifu, tafadhari tujengeni namna nzuri ya kushughulika na shida zetu, matatizo yetu hayawezi malizwa na dini zetu, bali kumtanguliza Mungu mwenye kuleta dini na watu wake.

Mivutano, kusigana, kuoneshana ubabe, fitina, kisasi na vingine vya namna hiyo hatuponyo taifa, badala yake tunachochea vurugu na kutoweka kwa Amani. Taifa likiharibika na kuanguka hakuna atakayekuwa salama, uwe na dini yako nzuri, msimamo wako imara, n. K wote tutaharibikiwa na kutaabika.
 
KELELE NI NYINGI KULIKO UKWELI
Kwanza naomba kumshukuru mwenyezi Mungu mwingi wa rehema na mwenye uhai wetu kwa kutuweka tuwe hai hadi sasa.
Pili nipongeze jitihanda mbalimbali za serikali, asasi za kirai, taasisi za kidini, jumuiya za kitaifa na kimataifa kwa kuwa mstari wa mbele kutafuta suluhu na mstakabari mwema wa taifa letu la Tanzania.
Hata hivyo imenishangaza sana kuona taasisi hizi zinavutana juu ya maoni, mtazamo na ushauri juu ya kushughulikia janga hili lilolikumba taifa letu ambalo kwa muda limesifika kuwa taifa la amani na watu wakarimu kwa watu wote.
Watanzania wenzangu tunatakiwa kujua fika na hakika kuwa Tanzania ni zawadi pekee ambayo Mungu ametupa na tunatakiwa tuiliende kwa nguvu zetu zote bila kuwa na mivutano ambayo kimsingi Haina afya njema sana kwa taifa letu na ustawi kwa watu wake.
Mashabulio yanayoyafanywa na taasisi za kidini juu ya maoni, mtazamo, na ushauri juu ya namna watu wanodai haki Yao na namna ya kudai haki hiyo, ya nataka kuleta udini na kuigawa jamii na taifa letu. Tusitumie matamshi ya kutisha, kuhamasisha, au mihemko yetu kuharamisha maoni, ushauri wa watu wengine kiasa kwamba sisi ushauri, mtazamo na maoni yetu ni bora sana na pengine tunadhani kufanya hivyo ni suluhu na utatuzi wa janga lililotupata kama taifa. Tusitumie nyumba za ibada na kuwahamasisha waumini wetu kukabiliana na kundi fulani linalodai haki fulani, katika kukabiliana huko ndiko kunasababisha uvunjifu wa Amani na kupeleke machafuko yanayochafua taswira ya taifa letu. Kama taasisi hizi za kirai, kidini na jumuiya mbalimbali zikifanya hivyo tutabaghaza taifa letu na kuwakosea watanzania ambao wanataka mstakabari mzuri na ustawi wa taifa lao urudi kama ulivyokuwa awali.
Taasisi ya kikristo TEC wao nadhani na kwa uelewa wao walitoa ushauri, mtazamo na maoni yao juu ya nini kifanyike juu ya yaliyolipata taifa letu, na wao wakifahamu fika kuwa hawana vyombo vya dola badala yake serikali yetu ione kama inaweza tumia ushauri huo labda utaponya taifa letu. TEC wasichukuliwe kuwa ni maadui wa taifa hili na watu wake, kama Kuna pahala tunadhani wamekosea pasi tuwarekebishe, tuwasamehe na ikiwezekana tuwaite na kukaa nao ili kupata uwelekeo unaofanana tayari tutakuwa tunatafuta namna nzuri ya kuponya taifa hili.
Viongozi wetu wa taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali watu wengi wanawaamini sana, na hakika kile mnachokisema na kuwaambia watu wengi, mjue watakifanya kikamilifu, tafadhari tujengeni namna nzuri ya kushughulika na shida zetu, matatizo yetu hayawezi malizwa na dini zetu, bali kumtanguliza Mungu mwenye kuleta dini na watu wake.
Mivutano, kusigana, kuoneshana ubabe, fitina, kisasi na vingine vya namna hiyo hatuponyo taifa, badala yake tunachochea vurugu na kutoweka kwa Amani. Taifa likiharibika na kuanguka hakuna atakayekuwa salama, uwe na dini yako nzuri, msimamo wako imara, n. K wote tutaharibikiwa na kutaabika.
Tanzania kwanza tofauti zetu zifuate lakini tuzitatue
psamanini@gmail.com
Walio nyuma ya hili swala la Udini na kuwapa wale wanazuoni ya kusema mbele ya umma walikosea sana kwa kweli.
 
Ngoja masheikh wa bakwata na wahadhiri wao waje wakushambulie.
 
Back
Top Bottom