Kelele mitaani tishio kwa wananchi

Kelele mitaani tishio kwa wananchi

Elias Msuya

Senior Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
173
Reaction score
671
WhatsApp-Image-2024-02-03-at-3.04.51-PM.jpg

Licha ya Sheria ya Mazingira, 2004 kukataza upigaji wa kelele unaosababisha kero kwa Wananchi, bado suala hilo limekuwa kero katika maeneo mbalimbali nchini.

Sheria hiyo kifungu cha 3 inatafsiri kuwa kelele ni kila uchafu zi usababishwao na sauti ambayo kwa asili inakataliwa au ile iwezayo kusababisha athari mbaya kwa afya ya binadamu, maisha au mazingira; pia ni pamoja na sauti iwezayo kubainishwa na Kamati ya Taifa ya Viwango vya Mazingira.

Vyanzo vya kelele chafuzi vimetajwa kuwa ni shughuli mbalimbali za kibinadamu ujenzi, nyumba/kumbi za starehe, shughuli za viwanda, nyumba za ibada, vyombo vya usa¬ri, magari ya matangazo.

Baadhi ya wananchi jijini Dodoma eneo la Kizota wameilalamikia baa iitwayo The Last Choice Park inayopatikana katika Mtaa wa Mkonongo barabara inayoelekea Shule ya Msingi Sokoine katika barabara kuu inayoelekea Singida.

“Tumeshalalamika kwa mwenyekiti wa mtaa, lakini hakuna hatua iliyochukuliwa, ndio maana tunalalamika kwa vyombo vya habari. Kinachofanyika hapa ni upigaji wa muziki hasa nyakati za jioni hadi usiku wa manane, kelele hizi zinatuathiri kiasi cha kushindwa kulala,” alisema mwananchi aliyejitambulisha kwa jina la John Masika.

Mmoja wa wamiliki wa baa hiyo aliyetambulika kwa jina la Sylivester Philipo alikanusha kupiga kelele, akisema hajawahi kusikia malalamiko.

“kelele zilizopo ni za kawaida tu na wala hatujawahi kupata malalamiko. Huwa hatukeshi, sana sana tunakwenda mpaka saa 7 usiku,” alisema.

Kero kama hiyo pia imeelezwa kwa kuwepo katuika Mtaa wa Rada Kata ya Majohe Kichangani jijini Dar es Salaam, ambapo wananchi wanalalamikia glosari iliyozinduliwa hivi karibuni na kugeuka kuwa kero kwa wananchi.

“Hapa mchana ni duka la kawaida, lakini ikifika usiku wanafunga spika na kupiga muziki hadi saa 9 usiku matokeo yake tunashindwa kulala. Tumeshalalamika kwa mjumbe wa nyumba 10, lakini hakuna hatua zinazochukuliwa,” amesema Juma Mohamed anayeishi katika mtaa huo.

Juhudi za kumpata mwenye baa hazikufanikiwa.

Kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira, 2004 Kifungu 106(5) Si ruhusa kwa mtu yeyote kupiga kelele au kusababisha kelele kuzidi kiwango kilichoainishwa au kitakachobainishwa kuhusiana na upigaji kelele.

Litakuwa ni kosa kwa mtu yeyote kumwaga uchafu au kupiga kelele bila kuzingatia njia iliyobainishwa kuwa ni bora katika Kanuni zinazoweza kutungwa na Waziri.
 
Back
Top Bottom