Keissy alianzisha tena bungeni

 
I trully like that guy at some points na hasa kuwaambia ukweli hao jamaa wa kijani na Zanzibar yao.

Wazanzibari wanapaswa kutambua kuwa baada ya kumpindua Sultan mwarabu sasa wanatawaliwa na Tanganyika kwa kisingizio cha muungano!
 
Na ukwel unaumaga sana.... Na ndo mana wameumia sana cha msingi nao zanzibar waanze kuchangia.... Mana ni mzigo jamani
 
Watanganyika hawapendi kusikia ukweli kuwa wanabebeshwa mzigo mzito wa kuilea Zanzibar!!
 
Wazanzibari wanapaswa kutambua kuwa baada ya kumpindua Sultan mwarabu sasa wanatawaliwa na Tanganyika kwa kisingizio cha muungano!

Wazanzibari wanalitambua hili sana tu. Tatizo nguvu za mtutu wa bunduki. Zanzibar na Palestina ndio yale yale.
 
Kessy yuko sahihi na kama tatizo ni kupoteza kiti kimataifa hata Tanganyika ilipoteza kiti chake cha Tanganyika.kinachofanyika hapo ni ujinga tu, wa ccm lakini Kessy yuko sawa
 
Uko sawa mkuu maana hata Tanganyika haina kiti UN.
 



Mkuu Umeona ehh mijitu inatamkishwa halafu nayo inakwenda kama migombe tuu inachukua 96% ya misaada yote kwa ajili ya muungano halafu wanasema Tanganyika iko wapi ----- kabisa.

Yaani kama ulivyogusia inalalamika tuu lakini hakuna anayetaka tanganyika irudi na kama wangetaka wangemshauri huyo kilaza wao apeleke hoja ama afungue kesi kama mchungaji Mtikila.

Acheni kubwabwaja FUFUENI TANGANYIKA YENU KWANZA HALAFU NDO MUZUNGUMZIE KUBEBANA wajinga ndo waliwao
 
Kuna ubaya gani wakichangiwa wakilipiwa ndo faida za muungano hizo kwa zanzibar kama na nyie mnaona vipi basi tuungane na zimbabwe ili watulipie tupate zaidi
 
Ukitaka pesa ni lazima utumie pesa.

Change ya radar wangepewaje Wazanzibari wakati mkopo wa kuinunua utalipwa na Tanganyika? Misaada ya nje Zanzibar inapewa 5% wakati hata gharama za ubalozi huko nje wanachangia 0%. TRA haikusanyi hela ya Zanzibar kuleta Tanganyika. Kuvunja Mwungano haiwezekani, usalama ni muhimu kuliko chochote. Kwa maelezo ya Lukuvi mwungano ukivunjika, IS wataichukua Zanzibar ndani ya siku 1 halafu watasumbua pwani yote ya Afrika Mashariki. Gharama ya kupigana vita kuwaondoa IS au Boko Haram au Al Shabab Zanzibar, itakuwa kubwa kuliko kuihudumia Zanzibar.

Ili kuondoa chuki na chokochoko na kujenga mwungano wa maelewano, Zanzibar ni lazima ichangie gharama za mwungano, hata kama ni kwa kiasi kidogo. Kutokuchangia kabisa inaweza kuchukuliwa kuwa ni kiburi na jeuri.

 
Kama huyu mzanzibar mmoja anasema eti Zanzibar ipongezwe kwa kukabidhi kiti chake UN mikononi mwa Tanzania Bara. Ivi hili ni jambo la kifahari? MZanzibar kweli anaongea jambo hili na kuona ni sifa? mi nadhan huyu ndiyo kwenda kupimwa akili

Zanzibar ilipoteza kiti lakini ipo , utalinganisha na Tanganyika iliyopoteza kiti UN na kuuuwawa kabisa..!!!?
 

Sijuwi unatumia nini kufikiri, hayo maneno sikusema mimi rudi kwenye mada kuu kuna mchangiaji kutoka Zanzibar jana bungeni baada ya Kessy kusema Zanzibar haichangii muungano, mchangiaji huyo alikuja juu na kusema ''Keissy hajui historia kwani Zanzibar ilipoteza utambulisho wake katika kiti cha Umoja wa Mataifa na kuiachia Tanzania, jambo ambalo nchi hiyo ndogo inastahili kupongezwa''

Ndoma mana sasa nasema Ivi kuna baadhi ya watu hasa wazanzibari kwamba Zanzibar kukosa kiti chake UN na kuiachia Tanganyika ama Tz bado wanaona Zanzibar ipongezwe kwa kukosa mamlaka yake hayo? ndo nimesema kwamba huyu jamaa anafaa kupimwa akili.
 
Tanganyika kwa namna fulani inaitumia Zanzibar kama koloni lake bila ya kuweka kila kitu wazi. Na hii ndiyo sababu ya kutokubali uwepo wa serikali tatu au moja. Ukiweka serikali tatu, Tanganyika haitakuwa na mamlaka makubwa juu ya Zanzibar kama ilivyo sasa. Kwa mfumo wa sasa, japo mawaziri wa Mwungano hawaendi Zanzibar lakini wana mamlaka makubwa sana juu ya Zanzibar.

Rais wa Jamhuri akiitisha Baraza la Mawaziri anawaita mawaziri wa Tanganyika, na kule Zanzibar anayetakiwa ahudhurie humo ni Rais wao tu ambaye hadhi yake haiwi tofauti na ile ya Mawaziri (siku hizi naambiwa huwa haji). Ni kwenye Baraza hili la Mawaziri ndiko masuala ya ulinzi wa Taifa, mambo ya nje, uchumi, Elimu ya juu, n.k. yanajadiliwa. Na uamuzi wake lazima uwaguse Wazanzibari. Kuna Mawaziri wachache kwenye Wizara fulani waliotoka Zanzibar lakini hawapo katika wizara hizi kama wawakilishi wa Wazanzibari.

Kutokana na ukweli huo ni kwamba kwa vile Tanganyika inaitumia Zanzibar kama koloni lake kwa mgongo wa Mwungano, ni lazima ibebe gharama fulani za kulihudumia koloni lake. Kule Afrika nadhani mnashuhudia kila mara Ufaransa inaenda kuzima maasi kwenye makoloni yake ya zamani. Kama Ufaransa inagharamia mpaka leo makoloni yake, hali inategemewa iwe vipi kwa Tanganyika ambayo mpaka leo inaitumia Zanzibar kama koloni lake kwa siri?

Ukweli unaweza kuwafanya wazanzibari wachukie lakini ukweli ni lazima usemwe, na ukweli huu uwe hamasa kwa Wazanzibari kupigania kuwa washirika wa Mwungano kuliko kuwa koloni kwa mgongo wa mwungano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…