Keissy alianzisha tena bungeni

Kashishi

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2010
Posts
1,147
Reaction score
641

Chanzo: Gazeti la Mwananchi

 
Kama huyu mzanzibar mmoja anasema eti Zanzibar ipongezwe kwa kukabidhi kiti chake UN mikononi mwa Tanzania Bara. Ivi hili ni jambo la kifahari? MZanzibar kweli anaongea jambo hili na kuona ni sifa? mi nadhan huyu ndiyo kwenda kupimwa akili
 
WaZanzibar hawapendi kusikia ukweli ............. na hii ni kwa kuwa Watanganyika wamekuwa waoga kusema ukweli!! Sasa kumbe ZNZ wanataka tuwalipe fadhira kwa kuachia kiti cho cha umoja wa mataifa!!?? Wapo BUngeni wanapiga kelele za usawa katika muungano kumbe hata kuchangia ghrama za posho wameshindwa.

Anyway, Keissy ana point kubwa sana, itakuwaje Rais wa Zanzibar awe makamu wa Rais wakati anachaguliwa na wazanzibar peke yao! Kama ikitokea Rais akafa nani atakuwa Rais kwa mapendekezo yao!!? Hapa unaweza kuta Rais anakufa halafu Rais wa ZNZ anarithi kwa mujibu wa katiba na kuwa Mkuu wa nchi wakati amechaguliwa na watu laki 5 tu kule visiwani.

Sioni kwa nini mtu anazungumza na kuchangia au kuhoji kitu muhimu halafu analazimishwa kumba msamaha .......... kwa kweli CCM ni laana tuliyopewa na Mungu Tanzania!!
 
Tanganyika buzi la zanzibar....,hatutaki kuchunwa tena.......... Hatutaki,rudini kwenuuuuuuuuuuuuuuuuuu nyie wazanzibar .tanganyika sio shamba la bibi..ipo siku mtarudi kwenu,ipo siku mtarudi mende msipende .nyie watu waugunja mnapenda sana vya bure mnachuna tuuuuuuu
 

Kaka nimekuelewa sana kuliko maelezo ila sasa kuna mizuka ya CCM hapa inaishia kuropoka tu bila kueleza wanaropoka nini.....mimi najiuliza kwani ccm bila Zanzibar imekufa ama???!!!! Leo nilimsikia John Komba anamnanga Jaji Warioba kwamba alishatoa rasimu yake kwa hiyo akae kimya sasa na wao watoe rasimu yao then zipimwe na wananchi ni ipi rasimu bora???!!!mimi nilishangaa sana huyu John Komba ni mbumbumbu wa aina gani na amesomea wapi??aliyewapa haki hawa waliokaa bungeni sasa na kutoa rasimu yao kupingana na ya Warioba ni nani na kwa sharia ipi???!! kuna mtu akanistua kwamba John Komba alighafilika akasema siri za ndani za CCM ambazo actually hakutakiwa kuzisema hadharani.maana ukweli ni kwamba CCM wana rasimu yao ambayo ndiyo iliyojadiliwa kwenye bunge lao haramu na watakayoipigia kura kwa kulazimisha.......Mimi sielewi hili chama chakavu linatupeleka wapi watanganyika sisi???!!!
 
Kessy yupo sahihi. Tena anatakiwa apongezwe kwa kuwasemea watanganyika ambao siku zote wanashindwa kuongea ukweli kuhusu utata wa muungano. Mwenye busara yeyote lazima ajiulize,hivi zanzbar wanachangia sh ngapi kwenye gharama za muungano. Jibukeshatoa Benno Ndulu gavana kwamba hawachangii kitu!. Kingine pia tujiulize,tunapomufanya rais wa zanzbar kuwa makamu wa kwanza wa rais,hivi tuna akili kweli? Ikitokea rais wa Tanzania bahati mbaya kafa,huyo makamu wa kwanza ndiye atakua rais. Sasa kichekesho ni kwamba huyo makamu kachaguliwa na watu laki kadhaa wa Zanzbar tu,watanganyika wote milioni 44 hawajamchagua wala hawajashirikishwa kumpata! Haya ni maajabu na mbunge Kessy ana ujasiri wa kuyaelezea haya na tumemuelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…