#COVID19 KCMC yakumbwa na uhaba wa oksijeni kwa wagonjwa wa COVID-19

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,875
1627028789218.png

Mkurugenzi Mtendaji wa KCMC, Profesa Gilleard Masenga amesema mgonjwa mmoja wa #COVID19 anatumia hadi mitungi 10 kwa siku.

Hospitali ya Rufaa ya KCMC inzalisha mitungi 400 na idadi ya wagonjwa inazidi kuongezeka hali inayofanya hospitali kuzidiwa.

----

Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini ya KCMC imezidiwa na idadi ya wagonjwa wanaohitaji hewa ya Oksijeni ukilinganisha na mitungi 400 inayozalishwa kwa siku huku mgonjwa mmoja akitumia mitungi 8 hadi 10 kwa siku.

Hayo yamesemwa leo Ijumaa Julai 23 na Mkurugenzi Mtendaji Hospitali hiyo, Profesa Gilleard Masenga wakati akizungumza na Mwananchi Digital.

Profesa Masenga amesema kwa siku inatumika mitungi ya Oksijeni zaidi 400 ukilinganisha na uzalishaji wake kwa siku ambayo ina uwezo wa kuzalisha mitungi 400.

"Kwa siku mgonjwa mmoja anatumia mitungi 8 hadi 10 hili tatizo ni kubwa na wananchi msilichukulie kimzaha mzaha ni ugonjwa hatari sana, tuendelee kuchukua tahadhari zote zinazotolewa na Wizara ya Afya," amesema Profesa Masenga na kuongeza,

"Tuna kiwanda hapa KCMC cha kuzalisha mitungi 400 kwa saa 24 na mtambo huu Mungu alitusaidia tukauweka mwaka jana na tuliona hili litatusaidia kwa miaka 20 bila kuwa na shida ya Oksijeni,"

"Matumizi yetu kwa siku yalikuwa ni mitungi 50 hadi 60 lakini ilipofika mwezi wa tatu mwaka jana kwenye wimbi la kwanza la corona tuliona umuhimu wake,"amesema Profesa Masenga.

"Sasa hivi kiwanda kimezidiwa matumizi ni zaidi ya mitungi 400 kwa siku kwa hiyo hali sio nzuri," amesema Profesa Masenga

Amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari za kujikinga na ugonjwa huo wa corona na kufuata maelekezo yote yanayoendelea kutolewa na Wizara ya afya.

Chanzo: Mwananchi
 
Serikali ipige marufuku mikusanyiko isiyo na msingi, pia magari ya abiria yawe level seat aisee na barakoa iwe lazima maana watu wamejisahau kuhusu corona wakati hii delta variant ni hatari mno
Yani hii level seat ukiongea,unafatwa na wenye/ndugu wenye vidaladala wanajazba vibaya mno.
 
Hakuna sehemu jiwe alisema corona hakuna?
Matamshi yake yalifanya watu waache kuchukua tahadhari ikiwemo kuruhusu misongamano na kutokuvaa barakoa, matokeo wizara ikaacha kutoa maelekezo na Sasa watu hawafanyi lolote na matokeo tunaona uhaba wa mitungi ya oksigen
 
Yani hii level seat ukiongea,unafatwa na wenye/ndugu wenye vidaladala wanajazba vibaya mno.
Huku tuendako inabidi kuwa na strictly measures mbona mwanzo walifamya na tukaweza kudhibiti maambukizi kusambaa ikiwemo mashule kyfungwa. Ya Sasa ni hatari Sana na vifo vingi, Bora tu Sasa chanjo itolewe tu kwa ngazi za hospital
 
Yawezekana ikawa sababu pia kumpeleka yule mstaafu mount meru.

Kanisa liko kimya wamejifungia kivyao.

Serikali inasema haitaki msongamano kutamka kufunga milango ya nyumba za ibada wanashindwa.

Papa alifunga milango ya St Peter's huko Roma h
 
Serikali ipige marufuku mikusanyiko isiyo na msingi, pia magari ya abiria yawe level seat aisee na barakoa iwe lazima maana watu wamejisahau kuhusu corona wakati hii delta variant ni hatari mno
Utakuja ambiwa mechi ya watani ni kusanyiko LA lazima...WATU LAZIMA WAINGIE WACHEK MECHI...MAANA KUSANYIKO LA LAZIMA HALINA COVID
 
Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini ya KCMC imezidiwa na idadi ya wagonjwa wanaohitaji hewa ya Oksijeni ukilinganisha na mitungi 400 inayozalishwa kwa siku huku mgonjwa mmoja akitumia mitungi 8 hadi 10 kwa siku.
Vipi sanamu yetu kule 77?
 
Uongozi wa KCMC hospital umesema kwa sasa kuna uhaba mkubwa wa mitungi ya gesi ya oxygen na wagonjwa wanazidi kuongezeka na hawaelewi watafanya nini siku za usoni.

Naye RC Kigaigai wa Kilimanjaro amesema hali ni mbaya mkoani humo hivyo amepiga marufuku mikusanyiko yote isiyo ya lazima.

Source: ITV habari za saa
 
Back
Top Bottom