#COVID19 Kilimanjaro: KCMC yazidiwa wagonjwa wanaohitaji Oksijeni

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,734
6,292
Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini ya KCMC imezidiwa na idadi ya wagonjwa wanaohitaji hewa ya Oksijeni ukilinganisha na mitungi 400 inayozalishwa kwa siku huku mgonjwa mmoja akitumia mitungi 8 hadi 10 kwa siku.Hayo yamesemwa leo Ijumaa Julai 23 na Mkurugenzi Mtendaji Hospitali hiyo, Profesa Gilleard Masenga wakati akizungumza na Mwananchi Digital.

Profesa Masenga amesema kwa siku inatumika mitungi ya Oksijeni zaidi 400 ukilinganisha na uzalishaji wake kwa siku ambayo ina uwezo wa kuzalisha mitungi 400.

"Kwa siku mgonjwa mmoja anatumia mitungi 8 hadi 10 hili tatizo ni kubwa na wananchi msilichukulie kimzaha mzaha ni ugonjwa hatari sana, tuendelee kuchukua tahadhari zote zinazotolewa na Wizara ya Afya," amesema Profesa Masenga na kuongeza,
"Tuna kiwanda hapa KCMC cha kuzalisha mitungi 400 kwa saa 24 na mtambo huu Mungu alitusaidia tukauweka mwaka jana na tuliona hili litatusaidia kwa miaka 20 bila kuwa na shida ya Oksijeni,"

"Matumizi yetu kwa siku yalikuwa ni mitungi 50 hadi 60 lakini ilipofika mwezi wa tatu mwaka jana kwenye wimbi la kwanza la corona tuliona umuhimu wake,"amesema Profesa Masenga.

"Sasa hivi kiwanda kimezidiwa matumizi ni zaidi ya mitungi 400 kwa siku kwa hiyo hali sio nzuri," amesema Profesa Masenga
Amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari za kujikinga na ugonjwa huo wa corona na kufuata maelekezo yote yanayoendelea kutolewa na Wizara ya afya.
 
Hawana malimau ? au wapelekewe huu mtambo🐒

20210724_130839.jpg
 
"Kwa siku mgonjwa mmoja anatumia mitungi 8 hadi 10 hili tatizo ni kubwa na wananchi msilichukulie kimzaha mzaha ni ugonjwa hatari sana, tuendelee kuchukua tahadhari zote zinazotolewa na Wizara ya Afya," amesema Profesa Masenga na kuongeza,

Maneno ya Profesa hapa ndo yanafikirisha yaan
 
Nafikiria itakua ni Propaganda ya kuhamasisha chanjo kwa wananchi, Mbona wimbi limeanza baada ya tetesi za chanjo kuingia Nchini..... Kwa uelewa wangu tu!!
 
Inasemekana wenye dhamana walishapata chanjo walipo wako salama. Ajabu ni kuwa kwa nini wanaendelea kuufanyia siasa ugonjwa huu wakati maisha yakipotea.
Mkuu,
Jf ni home of great thinkers with fact,achana na issue za "Inasemekana" "Unaambiwa" "Nasikia..."
 
Back
Top Bottom