Kazi zipo ila ajira hakuna

Ukweli mchungu,Mimi nimekuelewa Mkulu
Wabongo wamezoea siasa (maneno matamu ya kinafiki). Mimi hadi nimefungua grocery na nikawa nauza mwenyewe - watu wananicheka lakini kuna kitu nilikuwa napata; badala ya kutoka kwenye mishe zangu nikajichanganya kwenye baa za watu nilikuwa naenda kwenye grocery yangu - nachoma mishkaki na inaisha kabisa.
Yaani nikiangalia kazi zilizopo mtaani ni nyingi sana ila watu / vijana hawataki kabisa.
 
Ukweli mchungu,Mimi nimekuelewa Mkulu
10000000000% CORRECT SIR!!!.... Kijana mwenzang usipochukia haya utajuata.... Mana hata mm ni Bachelor degree cjaajiriwa na sina iman na kaujiriwa kabsaaa..... Japo ni ukwel mwanzo mgum xanaa hasa ukizingatia umetoka chuo na huna backup nzur ya financial capital..... Inabidi kutumia akili nying xana kuwa mbunifu ku rise capital,,......


Kwa upande mwngine mazingira wezeshi toka serekalini ni muhimu sanaa ili kuendeleza juhudi za kijana,........
 
neno la kweli sana hili,natamani kuwaambia watu wengi kwamba ajira hamna ila kazi zipo...
 
Matajiri ni wachache sana duniani,ukilinganisha na idadi ya watu waliopo;hii inamaanisha mtu kuwa tajiri au kujiajiri ni kipaji na sio kila mtu anacho,kwa hiyo wanaoshauri watu wajiajiri wajiulize je yeye amejiajiri/ameajiriwa.
 
Matajiri ni wachache sana duniani,ukilinganisha na idadi ya watu waliopo;hii inamaanisha mtu kuwa tajiri au kujiajiri ni kipaji na sio kila mtu anacho,kwa hiyo wanaoshauri watu wajiajiri wajiulize je yeye amejiajiri/ameajiriwa.
Hii ni point ya maana sana.
 
Kufikiri ndio kukoje? au unapofikiri unakuwaje? nahisi labda hata mimi sijui kufikiri, ingawa mleta uzi anasema tufikirie hata mara 1000, je kufikiri mara moja kukoje?
 
Hili jibu sahihi kwa mleta Mada, Wapishe vijana uje ufikirie mtaani mara 1000000, tuone hizo fikra zako.
Jaribu kunielewa - mimi ndiye mleta mada; sina ajira - najishughulisha na mambo yangu kila siku. Na sijawahi kuajiriwa labda kufanya kazi za mkataba mfupi tu.
Kikubwa nashukuru kuna vijana niliwashauri na sasa wamekubali ushauri wangu niko nao tunaendelea kufanya kazi. Waliikuwepo tu mitaani wanazunguka na bahasha lakini kwa sasa wapo wanapiga kazi kama kawaida.
Anayesema haiwezekani yuko sahihi - na pia anayesema inawezekana yuko sahihi.
Unavyofikiri ndivyo ulivyo!
 
Mkuu nina laki tano kweli iko benki sina wazo la biashara...hakika Unaweza ukanipa maujuzi ya kujiongeza
 
Mkuu nina laki tano kweli iko benki sina wazo la biashara...hakika Unaweza ukanipa maujuzi ya kujiongeza
Kuna kipindi nilifundisha kuhusu mpango wa vikundi vya hisa.
Ebu nikupe mfano mdogo ...
Watu 10, kila mmoja ana hela yake ametunza eti iongezeke ndo afanye shughuli fulani. Lakini watu kumi hawa ukiwaunganisha kimawazo ni rahisi wote kupata mitaji yao ndani ya muda mfupi.. hapa natoa mfano wa kile ninachokifanya.
Anza hisa kwa watu 10 Kila mmoja atoe kianzio Tshs. 100,000/= Mtakuwa na jumla ya Tshs. 1,000,000/=
Alafu mjipangie kuwa thamani ya Hisa moja iwe Tshs. 5,000/= Hivyo kwa watu 10; kila mmoja akinunua Hisa 3 mtapata jumla ya Tshs (3 x 5,000/= x watu 10) = 150,000/= - inaweza ikazidi hapo.
Jumla mtakuwa na Tshs. 1,150,000/=. Hiyo hela tangaza kuikopesha kwa riba ya asilimia 10 kwa mwezi.
Baada ya miezi sita tu nakuhakikishia mtakuwa na pesa ndefu sana ambapo kila mmoja ataendesha shughuli zake kwa uhakika zaidi.
Back to your laki tano .... fuga kuku au sungura au bata. Soko liko njenje.
 
Mkuu nyumba za kupanga unafugia wapi kuku au sungura...? Bado natega sikio kukusikiliza
 
Jifunze kuhusu Hisa ...
Mkuu nyumba za kupanga unafugia wapi kuku au sungura...? Bado natega sikio kukusikiliza
Hebu soma hiyo hapo kwanza ... kwa nini umeangalia karibu sana kwenye kufuga tu. Maelezo yangu ya awali yana maana zaidi ya kufuga.

NGUVU YA UMOJA
Siku moja kundi la watu 500 walikua wamehudhuria Semina. Mara msemaji mkuu wa semina hiyo akaanza kumpa kila mtu puto (balloon), na kuwaambia kila mmoja aandike jina lake juu la puto alilopewa.

Kisha maputo yote yakakusanywa na kuwekwa kwenye chumba kimoja.Kisha watu wote wakaambiwa waingie kwenye chumba hicho na kila mmoja atafute puto lenye jina lake ndani ya dakika 5. Kila mmoja akaanza kuhangaika huku na kule akitafuta puto lake bila mafanikio, na chumba chote kikawa na fujo tupu.Baada ya dakika 5 kwisha, hakuna hata mmoja aliyekua amefanikiwa kupata puto lake.

Ndipo msemaji akawaambia basi kila mmoja achukue puto lolote tu na ampe mtu ambaye jina lake limeandikwa kwenye puto hilo. Ndani ya dakika chache kila mmoja akawa ameshapata puto lake.Ndipo msemaji mkuu akasema:
Hii inatokea kwenye maisha yetu kila siku. Kila mtu anahangaika kutafuta furaha yake huku na kule, bila kujua ilipo. Furaha yako ipo kwenye furaha za watu wengine. Wape furaha watu wanaokuzunguka;nawe utapata Furaha yako.Usipende kujitenga… Maisha ni watu…. Bila watu hakuna furaha….hakuna Maisha!

Kuna kitu kinaitwa Cage ... tengeneza cage then mwombe huyo mwenye nyumba sehemu ndogo tu just ft 3 x 4 weka cage yako fugia humo.
 
Endelea kudanganyana - mi natumia laptop yangu na modem.
Mkuu, wewe ni Mtu smart sana, Comment kama hizi huna haja ya Kuzijibu kabisa, Unsoma unapita tu; Jibu vitu vyenye Hoja nzito, hiyo inatosha, Usitake kumfurahisha Kila mtu; Wenye uhitaji tumekuelewa Mkuu;
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…