KAZI ZA POLISI ZATANGAZWA, ni kitambo lakini unaweza kuichangamkia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

KAZI ZA POLISI ZATANGAZWA, ni kitambo lakini unaweza kuichangamkia

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by ntamaholo, Apr 25, 2012.

 1. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #1
  Apr 25, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  Wednesday, April 25, 2012
  [​IMG] Mwenyekiti wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi Nchi za Mashariki mwa Africa ambaye pia ni Inspekta Jenerali wa Polisi Rwanda, Emmanuel Gasana (kushoto) akisaini kitabu cha wageni katika ofisi za wizara ya Mambo ya Ndani jana jijini Dar es Salaam aliopo nchini katika ziara ya kufuatilia utekelezaji wa maazimio ya mkutano wa kumi na tatu wa wakuu wa Majeshi ya Polisi wa EAPCCO, mkutano uliofanyika nchini Rwanda mwezi septemba 2011. Ziara hii ni pamoja na kuimarisha ushirikiano baina ya Majeshi ya nchi za mashariki mwa Afrika. Kulia ni Kamishna wa Operesheni, Paul Chagonja.  [​IMG] Mwenyekiti wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi Nchi za Mashariki mwa Africa ambaye pia ni Inspekta Jenerali wa Polisi Rwanda, Emmanuel Gasana (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Tanzania, Paul Chagonja kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania jana jijini Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dar es Salaam. IGP wa Rwanda yupo katika ziara ya kufuatilia utekelezaji wa maazimio ya mkutano wa kumi na tatu wa wakuu wa Majeshi ya Polisi wa EAPCCO, mkutano uliofanyika nchini Rwanda mwezi septemba 2011. Ziara hii ni pamoja na kuimarisha ushirikiano baina ya Majeshi ya nchi za mashariki mwa Afrika.

  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD]
  TANGAZO LA AJIRA Jeshi la Polisi liko katika mchakato wa kuajiri vijana kujiunga na Jeshi kupitia mashuleni. Tumeamua kuurudia utaratibu ambao ulikuwepo zamani wa kuajiri moja kwa moja toka mashuleni ambao ulikuwepo siku za nyuma kutokana na mahitaji halisi ya Jeshi la Polisi kwa sasa. Hivi sasa Jeshi la Polisi linakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazotokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, ongezeko la uhalifu mpya kama vile wizi wa kutumia mtandao, usafirishaji haramu wa binadamu na kadhalika. Wahalifu wanaohusika na matukio kama hayo, wamekuwa wakitumia mbinu mpya na utaalamu wa hali ya juu. Aidha, Jeshi la Polisi linaendelea na Programu yake ya maboresho. Maboresho haya yanalenga kulifanya Jeshi kuwa la Kisasa zaidi ambalo litatelekeza majukumu yake kwa Weledi huku likiwa karibu zaidi na raia katika utendaji wake wa kila siku. Kutokana na changamoto hizo, Jeshi la Polisi linahitaji kuajiri, vijana wasomi, wenye utashi, ari na nia ya kufanya kazi za Polisi na wenye fikra na mtazamo unaoendana na dunia ya sasa. Vijana hawa watakuwa viongozi na chachu katika kuleta mabadiliko yanayokusudiwa ndani ya Jeshi la Polisi. A: – SIFA/VIGEZO VYA MWOMBAJI
  1. Mwombaji awe Mtanzania kwa kuzaliwa.
  2. Awe na afya njema iliyothibitishwa na Daktari wa Serikali.
  3. Awe hajaoa/kuolewa au kuwa na mtoto.
  4. Awe na tabia njema na asiwe na kumbukumbu za uhalifu.
  5. Awe amemaliza Kidato cha sita mwaka 2012 na kufaulu.
  6. Awe na umri kati ya miaka 18 na 25.
  B: MASHARTI KWA MWOMBAJI
  1. Kila mwombaji awe tayari kufanya kazi mahali popote ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  2. Kila mwombaji awe na ari,utashi na nia ya kufanya kazi ya Polisi.
  3. Kila mwombaji aandike namba yake ya simu na anuani yake ya kudumu kwa usahihi ambayo itatumika wakati wa kuitwa kwenye usaili.
  C: FOMU ZA KUJIUNGA ZINAPATIKANA:
  • Ofisi ya Mkuu wa shule
  • Ofisi za Makamanda wa Polisi Mikoa/Wilaya zilizo karibu
  • Pata fomu hapa(sel-form)
  Imetolewa na; Ofisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi, Makao Makuu ya Polisi, S.L.P 9141, DAR ES SALAAM.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]


  [h=3]Who's Online[/h]
  We have 91 guests online

  Copyright © 2012. Tanzania Police Force.
   
 2. Young Tanzanian

  Young Tanzanian JF-Expert Member

  #2
  Apr 25, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,740
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  hiyo nimeipenda itasaidia kupunguza tatzo la ajira nchini hongera IGP
   
 3. O

  OMEGA JF-Expert Member

  #3
  Apr 25, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 671
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 60
  Mi nemwahi kuliona ili Tangazo nikawashangaa sana,wanataka watu waliomaliza Kidato cha sita 2012 na kufaulu wakati matokeo bado hayajatoka,hata deadline waliyoweka uenda matokeo yatakuwa hayajatoka.Watu wa ajabu sana awa,na jana nilimsikia Kamishna mmoja kwenye kipindi cha polisi jamii -channel ten akijigamba kuwa polisi siku hizi wamesoma na hata yeye amesoma.ni usomi wa aina gani huu
   
 4. O

  OMEGA JF-Expert Member

  #4
  Apr 25, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 671
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 60
  Unaona wenzetu wanaotoka nchi zisizokula rushwa,hata jina lake kifuani kaweka kubwa ili lisomeke vizuri na watu wote walisome,wa Tanzania kajina kiduchu hata kusoma huwezi,this is not accidental it is dellberate,hata yule wa Tandahimba aliyechomewa gari na polisi kama lijina kifuani lingekuwa kubwa kama la IGP wa Rwanda identification ya polisi aliyemtenda ingekuwa rahisi sana.
   
Loading...