Dam55
JF-Expert Member
- Oct 8, 2015
- 5,669
- 12,044
Habari wandugu.
Ukiangalia duniani kote kwa sasa kuna kazi ambazo mtu ukifanya unajikuta unadharaulika sana katika jamii.
Lakini kiukweuli kazi hizi ni za muhimu sana, ambapo kama kungekosekana watu wa kuzifanya basi tungekuwa na hali mbaya sana.
Hapa nitatumia mifano miwili kuwaonenyesha umuhimu wa kazi hizi.
_ kazi za machinjioni.
Kwa jamii kubwa ya watanzania mtu akisema anafanya kazi machinjioni( kuku, ng'ombe n.k) watu humdharau sana na kuonekana kama vile si kazi ya maana.
Kimsingi katika maeneo kama hayo kuna majukumu tofauti tofauti, ambayo mtu ukimwambia unahusika nayo atakudharau sana mfano utakuta kuna wachinjaji, wasambazaji wa nyama, wafanya usafi n.k kila mtu na jukumu lake.
Lakini licha ya kuwadharau huko hebu tujiulize je ingekuwaje kama tusingekuwa na watu hawa majukumu haya yangefanywa na nani au kila mtu angekuwa akichinja mwenyewe?
_ wafagia barabara,
Hawa nao ni watu muhimu sana japo wanakosa heshima stahiki kwa kazi yao ya msingi wanayo Fanya.
Hebu tujiulize kama hawapo watu hawa hali ya barabara zetu katika hii miji ingekuwaje?
Unapita unakuta barabara safi unadhani bila ya uwepo wao nini kingetokea??
Licha ya kudharauliwa lakini bado pia wanalipwa mishahara midogo sana ambayo haiendani na kazi wanayo ifanya na umuhimu wake.
Madaktari. Walimu n.k kila siku wanalalamika kuongezwa mishahara lakini mbona hawa hawakumbukwi au ndio kusema kwamba umuhimu wao hauonekani.
Wito wangu kwa serikali za mikoa ziangalie namna ya kuwatunza vizuri hawa watu ikiwa ni pamoja na kuongeza mishahara yao.
Tukiwatumia vizuri hawa tutakuwa na miji safi bila shaka yoyote.
Hizo ni baadhi tu ya kazi ambazo nimejaribu kuzieleza hapo.
Karibuni muongezee na nyingine.
Samahani kama mada ni ndefu sana.