Kazi za kujitolea: Hii imekaaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kazi za kujitolea: Hii imekaaje?

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by Konunu Kokojako, Jul 11, 2011.

 1. K

  Konunu Kokojako Member

  #1
  Jul 11, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naomba nifahamishwe kuhusu kazi za kujitolea katika mashirika na makampuni mbalimbali.
  Kuna wengine wanalipa Nauli na Chakula cha mchana,
  wengine nauli tu na
  wengine hawamlipi chochote huyu anayejitolea.
  Hii imekaaje? Namaanisha ni utaratibu sa ofisi yenyewe au maamuzi binafsi ya bosi au kwenye sheria za kazi za nchi yetu ipoje?
  Sijui, naomba mnijuze.
   
 2. Da Pretty

  Da Pretty JF-Expert Member

  #2
  Jul 11, 2011
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 3,050
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Hata mi nimewahi kujiuliza....
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Jul 11, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Tatizo Tanzania kuna ajenda za siri hata kwa yule anayeomba kazi ya "kujitolea".

  Utaona mtu anaomba "internship","volunteering" au hata "practical".Halafu hapo hapo anategemea alipwe fedha akisahau kuwa kupewa fursa pekee ni msaada tosha.Kwa kujitolea, kujishikiza etc, mtu anapata uzoefu.

  Inashauriwa muombaji ajihakikishie kwanza anachoomba ndicho atakachopata na asijishangaze mwenyewe hapo baadae kwa kutokupata alichoficha kama matarajio!

  Kwa upande wa wenye mashirika, kuna sera tofauti baina ya shirika/tasis.Kuna taasisi zenye kutoa kiwango kidogo cha "posho" hasa kama mtu anatoka mbali ili ajikimu - usafiri na chakula.Taasis nyingine hazina utaratibu kama huo.
   
 4. E

  Emeka Onono Senior Member

  #4
  Jul 11, 2011
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 114
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jaman hiv hizo kazi za kujitolea zenyewe zipo? Mana nimejaribu kuomba wee lakin wapi,mwenye kujua wap naweza kujitolea au internship katika mambo ya food and nutrition,hiv/aids,pmtct,maternal and child,lakin pia hata mambo ya library mana nina uzoefu wa miaka 3 katika fani ya library hivyo naweza kumudu majukumu vizuri,hata kufundisha secondary pia masomo ya sayansi,niPM tafadhal
   
 5. m

  mja JF-Expert Member

  #5
  Jul 11, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 311
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ninavyoelewa mimi mara nyingi watu wanojitolea either wanataka kupata uzoefu au wanahitaji kutoa msaada wa kitu fulani (i stand to be corrected), sasa wewe unahitaji kazi ya kujitolea ya nini wakati una uzoefu wa miaka 3 na umaweza kumudu majukumu vizuri????
   
 6. E

  Emeka Onono Senior Member

  #6
  Jul 11, 2011
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 114
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wewe mja,hapo kwa upande wa library ndio nina uzoefu wa miaka 3 na kufundisha uzoefu wa mwaka 1,ila hapo kwenye food and nutrition etc ndio sina uzoefu zaid ya field tu,umenipata mja?
   
 7. E

  Emeka Onono Senior Member

  #7
  Jul 11, 2011
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 114
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wewe mja,hapo kwa upande wa library ndio nina uzoefu wa miaka 3 na kufundisha uzoefu wa mwaka 1,ila hapo kwenye food and nutrition etc ndio sina uzoefu zaid ya field tu,umenipata mja?
   
 8. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #8
  Jul 12, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 892
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  wewe unataka kujitolea hutaki kulipwa?? umesema unauweza kufundisha shule za Lowasa za kata hazina walimu wewe unangangania kujitolea bure wahi tandahimba, nkasi, maswa nk shule hazina walimu.
   
Loading...