Kazi za Dr Slaa Kusini zawasisimua wengi

Kwa machache tu.
Dr. ni intelligent
Dr. ni mbunifu
Dr. ni mwenye maono ya kitaifa (vissionary leader)
Dr. ni mchapa kazi
Dr. anamuenzi baba wataifa
Dr. anasoma sana
Dr. anajiamini kusimamia anayoyamini
endelezeni
 
Hakika CCM wataikumbuka siku NEC ilipomengua Dr. Slaa kwa kigezo cha kutokuwa na uzoefu wa kisiasa. Nakumbuka ilikuwa nyakati za baridi, msimu wa uchomaji mahindi watu wa karatu waliposononeshwa na uamuzi wa NEC kumuengua Dr. slaa na kurudisha Patrick Qoroo` ambaye alikuwa amechoka hata kufikiri maneno, aliwahi kusema kijografia wilaya haina maji, hivyo alaumiwe mungu na siyo yeye. Mungu ni mkubwa, kwa kiasi kile kile walivyosononeka watu wa karatu kwa kuenguliwa dr. walicheka, walisherehekea ushindi kwa shangwe na nderemo, miaka minne baadaye, wilaya ikawa yenye maji kijiografia. Nakumbuka hata kwa mbunge wa zamani (jirani yetu) maji yaliingia. Baada ya kujua ukweli nilimlaumu sana baba kwa kuwa alitueleza yote aliyoaminishwa na jirani yetu (mbunge) na kutuaminisha sisi pia.
Hongera Dr. slaa, ila nisamehe kwa kejeli nilizotoa ulipotemebelea shule yetu wakati huo nilikuwa form three (2000), nililishwa maswali na majibu nilipewa, nilisukumwa nikuulize maswali yanoyokera. Nakumbu ulitabasamu, kabla ya kunijibu uliniasa mimi na wanafunzi wengi waliokuwa wanakusikiliza. Ulisema umeanza kuwasha moto wa mabadiliko, nakumbuka neno ulilo tumia la "mindset". Leo nikiangalia mabadiliko ya kifikra na wanachi kujiamini kuhoji matumizi ya serikali zao za vijiji, hakika najiona mkosaji. Ilikuwa suala la muda tu, lakini haikuchukua muda, ni pale nilipobemba dembe mbili na nusu ya maharage kwa umbali wa km 23 niweze kuuza ili nipate pesa ya tuishen ya chemistry nikiwa form five/six.
Wanajamvi mnisamehe, ni msukumo wa hisia,

Thankyou kamanda
 
tatizo lipo dodoma na morogoro kazi kubaka na kunywa pombe haramu waspokuwa makini tutawatenga washenzi hawa
Hakuna haja ya kuwatenga kamanda taratibu tu watkaa sawa si unaona kusini somo limeanza kuwaingia.
 
Back
Top Bottom