Kazi za Dr Slaa Kusini zawasisimua wengi

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Katibu mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa ameelezwa kuwa mpiganaji asiyechoka kutokana na kazi kubwa anayofanya huko kusini tangu CHADEMA ianze operesheni Okoa Kusini wiki moja iliyopita.

Taarifa kamili zinasema Dr Slaa amekuwa akihutubia mikutano mitatu kila siku ambapo kwa siku zote hali chakula chochote mchana kutokana na kubanwa na muda.

Baada ya mikutano Dr Slaa anaongoza mikutano ya ndani mpaka saa 6 usiku na kisha anakuwa wa kwanza kuamka na kuwaamsha vijana wake waanze siku nyingine ya mapambano.

Imedaiwa pia kabla ya kila mkutano Dr Slaa anazindua matawi katika mitaa yote ya eneo husika.

Source: Kamanda Mwesilwa Perfect aliyeko kikosi kinachoongozwa na Dr Slaa katika operesheni okoa kusini.

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
[h=3]Dkt.Slaa Akisalimia Wananchi[/h]



Dkt. Slaa akizongwa na wananchi wa Kijiji cha Namahinga, Masasi aliokuwa akisalimiana nao
Picha Na Kurugenzi ya habari CHADEMA
 
Mbiu ya "Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke" inatekelezwa na kila kiongozi.
 
Slaa ni baba wa ukombozi wa tanganyika, baada ya nyerere slaa ndio shujaa wa taifa. mungu amjalie maisha marefu
 
Dr Slaa ni mtu mwenye heshima sana na bidii ya kazi.

Hakuna mtu ndan ya ccm anayeweza hata kusogelea.

Ukitaka kucheka jaribu kumfananisha na W.Mkama, yule babu anayejua misamiati ya kiingereza tu, wakati chama kinazama kwenye kilindi.

Big up Dr Slaa, una hazina ya heshima nyingi toka kwangu.
 
Nilibahatika kumjua vizuri arumeru..hata huku ilikuwa hivyo vivyo..
 
Gracias Dr. we ndo rais wangu. Eti Zitto anataka kuwa rais,hatutakubali hadi aachane na unyinyiem
 
Back
Top Bottom