Kazi ya Mungu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kazi ya Mungu!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by JAYJAY, Oct 8, 2010.

 1. JAYJAY

  JAYJAY JF-Expert Member

  #1
  Oct 8, 2010
  Joined: Oct 31, 2008
  Messages: 2,490
  Likes Received: 823
  Trophy Points: 280
  kwenye matuukio mengi yanayopeleka kifo cha mwanadamu kuna kauli nyingi hutamkwa. swali au maswali yanakuja kama unaamini Mungu ndiye anapanga kifo cha mtu
  1. unaamini kwamba anapanga pia namna huyo mtu atakavyokufa yaani ajali, ugonjwa n.k? mfano inatokea ajali ya gari na mtu au watu wanakufa, mara nyingi lawama zinaweza kuwa nyingi mfano dereva alikuwa amelewa, je huoni kwamba hiyo ni kazi ya Mungu kwamba ilimpasa dereva alewe ili asababishe ajali ili waliopangiwa kufa wafe( hii ni kama unaamini kuwa Mungu ndio anapanga namna mtu atakavyokufa)
  Kama unaamini vinginevyo je ni mgongano tuu kwamba siku yako ikifika kuna chochote tu kitatokea na kitautoa uzima wako? au kama unaamini ni kazi ya malaika wa uovu shetani, swali laja

  2.je shetani ana ushirikiano na Mungu katika kupeana taarifa? kwa maana, mfano mtu huyu alipangiwa kufa leo kwa kuchomwa kisu, sasa shetani anamwingia yule mhalifu ambaye anachukua kisu na kumchoma yule mtu ambaye siku yake imetimia naye anakufa, maana kama sio siku yake hangekufa, angejeruhiwa tu na kupona.

  Wadau haya ni maswali yanayonitatiza, hata pale kijiweni kwangu mtaani yalileta changamoto kwelikweli.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Hey people out there, stop talking of ELECTION MATTERS, and start discussing DEATH and its nomenclature!...i
   
Loading...